Mahojiano ya Oprah: Mke wa mwanamfalme Harry , Meghan Markle 'hakutaka kuwa hai'

Meghan Markle
Muda wa kusoma: Dakika 3

Mke wa mwanamfalme Harry, Meghan Markle amesema wakati mwingine alipata maisha kuwa magumu sana katika familia ya kifalme na 'hakutaka tena kuwa hai'Katika mahojiano ya kibinafsi na yenye hisia kali ya runinga, Meghan alimuambia Oprah Winfrey kwamba hakupata usaidizi wakati alipouitisha .

Amesema kibaya zaidi ilikuwa wakati mtu mmoja wa familia hiyo alipomuuliza Harry jinsi mtoto watakayemzaa atakuwa na 'ngozi nyeusi' .

Prince Harry pia alifichua kwamba babake Prince Charles aliacha kuzipokea simu zake alipogundua kwamba alikuwa na mpango wa kujiondoa kutoka familia ya kifalme .

Mahojiano hayo na Oprah yaliongojewa sana yalipeperushwa usiku nchini Marekani

Wakati wa mahojiano hayo maalum ya CBS ya saa mbili ambayo yatapeperushwa siku ya jumatatu saa tatu usiku katika runinga ya ITV nchini Uingereza na pia kwenye ITV Hub kwa hisani ya Harpo Productions/CBS, wawili hao wamezungumzia masuala mbali mbali ikiwemo ubaguzi wa rangi ,uhusiano wao na vyombo vya habari ,afya ya kiakili na mambo katika familia ya kifalme.

Pia walitangaza kwamba mtoto wanayemtarajia hivi karibuni ni msichana.

Wawili hao walihamia Carlifornia baada ya kujitoa kutoka majukumu ya familia ya kifalme Machi mwaka wa 2020 na ilitangazwa mwezi jana kwamba hawatarejea kama wanachama wa familia ya kifalme .

' Sikuwa nikilindwa'

Mahojiano ya Oprah na Meghana na mwanamfalme Harry

Meghan amesema alianza kuhisi upweke wakati vikwazo vilipowekwa kuhusu aliyoweza kufanya akifichua kwamba wakati mmoja hakuweza hata kuondoka nyumbani kwa miezi kadhaa Wakati mmoja alianza kuhisi kwamba 'hangewahi kuwa mpweke zaidi ya hapo' alimuambia Oprah

Alipoulizwa na Oprah iwapo aliwahi kufikiria kuhusu kujidhuru ama kuwa na mawazo ya kujiua Megan alijibu ' Ndio ..hilo lilikuwa bayana sana wazi sana na la kuogofya . sikujua ningemwendea nani'. Meghan alisema alihisi kuzongwa na picha ya hafla rasmi waliokuwa wamehudhuria na Harry katika Ukumbi wa Royal Albert Hall alipokuwa mja mzito

" Mwanzoni kabla ,tulilazimika kwenda katika hafla hiyo nilikuwa nimezungumza na Harry kuhusu suala hilo asubuhi hiyo' Meghan amesema

Winfrey alimuuliza : " Kwamba hutaki kuishi tena?'"Ndio ," Meghan alithibitisha

Alisema alihudhuria hafla hiyo na Harry usiku huo kwa sababu alihisi hakutaka kusalia mpweke na alikumbuka Harry akimshika mkono wakiwa katika hafla hiyo .

Wakati wa mahojiano Familia ya kifalme ilishtumiwa kwa kukosa kuliwaza Harry na Mkewe huku Meghan akisema hali 'ilianza kuwa mbaya ' baada ya wao kuoana Mei 2018

Familia ya ufalme ilikuwa na wasiwasi kuhusu ngozi ya mwanangu

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Familia ya ufalme ilikuwa na wasiwasi kuhusu ngozi ya mwanangu

" Niligundua kwamba sikuwa tu nikilindwa lakini pia walikuwa tayari kusema uongo ili kuwakinga baadhi ya watu wa familia ya kifalme .

" Lakini hawakuwa tayari kusema ukweli kunilinda pamoja na mume wangu'Alikuwa akizungumza kuhusu uvumi kwamba alimfanya mke wa kakake Duchess of Cabridge kulia kuhusu tofauti waliokuwa nayo kuhusu marinda yenye maua -habari ambazo zilisababisha taarifa nyingi za uvumi kuchapishwa .Meghan amesema ni kinyume kilichofanyika na Catherine baadaye aliomba msamaha na kumletea maua na kijikaratasi chenye maandishi ili kuomba radhi .

Mwanamfalme Harry

Akijiunga na mkewe na Oprah kwa sehemu ya pili ya mahojiano hayo Harry alizungumzia uhusiano wake na watu wengine wa familia ya kifalme .Alisema uhusiano na bibi yake ,Malkia 'ulikuwa mzuri sana' na wawili hao huzungumza kila mara Hata hivyo uhusiano kati yake na babake ,Mwanamfalme Charles wa Wales umevurugika .

Harry anasema anahisi 'kufelishwa' na babake. Aliongeza kwamba ataendelea kumpenda lakini 'kuna kuumizwa kwingi' kulikotokea'Kumhusu Mwanamfalme William alisema 'wapo katika njia tofauti' Pia alifichua kwamba familia yake ilikuwa imekoma kumpa msaada wa kifedha