Mzigo wa madeni: IMF yaendelea na juhudi za kuinasua Zambia kutoka madeni ya Uchina

Chanzo cha picha, AFP
Oparesheni za SGR sasa zitakuwa zikiendeshwa na shirika la Reli nchini Kenya kutoka kwa kampuni ya China ya Africa Star Railways (Afristar) baada ya kuanza kwa utaratibu wa kuipokeza majukumu hayo .
KRC tayari imetwaa majukumu mengine kama vile utoaji wa tiketi ,kutoa usalama na kutoa mafuta kwa treni za SGR.
Mwenyekiti wa shirika hilo Omuodho Awitta ameiambia radio ya Spice Fm kwamba watakamilisha kabisa kuchukua majukumu hayo Mei mwaka wa 2022 .
Awitta amesema shirika hilo limekuwa likijitayarsha kusimamia oparesheni zote za SGR na mwanzo wanafanya utaratibu huo awamu baada ya nyingine .
" Badala ya kuchukua majukumu haya katika kipindi cha miaka 10 tunafanya hivyo ndani ya miaka 5' amesema Awitta .
Mnamo Mei mwaka wa 2020 Ubalozi wa Uchina nchini Kenya ulikanusha ripoti za vyombo vya habari kwamba serikali ya Kenya ilihimizwa kukomesha kuendeshwa kwa oparesheni za reli na kampuni ya Uchina .

Ilidaiwa katika ripoti za vyombo vya habari kwamba mapato ya reli yalikuwa yamepungua kwa ajili ya Wachina kuruhusiwa kuendesha oparesheni za reli .
KRC ilitoa taarifa kwa kusema kwamba mazungumzo na Afristar yalikuwa yakiendelea vizuri na masuala mengi yalioibuliwa yalisuluhishwa.
Uchina imekuwa ikilaumiwa barani afrika kwa kuzitega nchi nyingi za Afrika kupitia mikopo na hivi punde kujipata mashakani hasa kuhusiana nan a mzigo w amadeni ya Uchina ni Zambia inayodaiwa zaidi ya bondi ya dola milioni tatu na dola nyingine milioni tatu inayodaiwa na kmapuni za Uchina .
IMF imesema mazungumzo ya kuweza kuikwamua Zambia kiuchumi yanaendelea vizuri na waziri wa Fedha wa taifa hilo Bwalya Ng'andu amesema nchi yake imejitolea kupata usaidizi wa IMF katika mpango huo.
IMF imesema inalenga kuutekeleza mpango wa kifedha wa kuirejesha nchi hiyo uthabiti wa kuweza kugharamia bajeti yake bila kuteemea fedha za mikopo iliposhindwa kutekeleza malipo ya baadhi ya pesa inazodaiwa .

Kampuni na mashirika yanayoidaiwa Zambia zimekaribisha tangazo la hatua zinazopigwa lakini zimehofishwa na kasi ya pole pole ya majadiliano hayo.
Lusaka iliitisha msaada hazina hiyo mwezi disemba mwaka jana na kuitisha kupewa afueni ya deni mwezi januari chini ya mpango wa pamoja unaoungwa mkono na mataifa yenye chumi thabiti ya G20 ili kuzisaidia nchi maskini duniani kushughulikia mzigo wa madeni .












