Uchaguzi wa Marekani: Waandamanaji wanaomuunga mkono Trump wazua ghasia katika miji ya Marekani

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelfu ya wafuasi wa Rais Donald Trump wanaodai kulikuwa na wizi wa kura wamekutana katika miji tofauri ya Marekani mwishoni mwa Juma na kusababisha ghasia walipokabiliana na waandamanaji wanaompinga.
Mjini Washington DC, zaidi ya watu 20 walikamatwa na wengine wanne walichomwa visu, kulingana na polisi.
Bw Trump alishindwa katika uchaguzi wa tarehe 3 Novemba na Bw Joe Biden lakini bado hajakubali kushindwa.
Wajumbe ambao kulingana na mfumo wa Marekani ndio wanaomchagua rais wanakaribia kuidhinisha ushindi wa Bw Biden leo Jumatatu.
Bw Biden alichaguliwa kwa kura 306 na Trump 232 katika kura za wajumbe - Electoral College, na kupata zaidi ya kura milioni saba kuliko hasimu wake wa Republican katika kura za wananchi.
Katika mji mkuu wa Marekani, polisi waliwatenganisha waandamanaji kwa kuwaweka pande mbili, mkakati ambao ulihusisha kufungwa kwa mlango la Black Lives Matter Plaza ambako waandamanaji waliokuwa wakipinga hatua ya Trump kukataa kushindwa walikuwa wamekusanyika.
Waandamanaji wanaomuunga mkono Trump , wakiandamana chini ya kauli mbiu waliyoiandika kwenye mabango inayosema "acha kuiba ", waliungwa mkono na wajumbe wa kikundi cha mrengo wa kulia kinachojiita Proud Boys, waliokuwa wamevalia mavazi ya rangi za manjano na nyeusi, wengi wao wakiwa wamevalia fulana za kujikinga na risasi.
Bw Trump alisababisha utata kwa kusema kuwa kikundi hicho kinapaswa " kujitokeza na kuwa kuwa chonjo" wakati wa mdahalo wa uchaguzi wa urais uliofanyika mwezi Desemba, ingawa baadaye alilaani "wanaharakati wote wanaotetea maslahi ya wazungu".
Kadri giza lilivyokuwa likiingia , waandamanaji wa Proud Boys na Antifa dhidi ya Trump , walikuwa wametenganishwa na polisi kwa kiasi kikubwa walikuwa wakirushiana matusi makali. Hatahivyo ghasia za hapa na pale ziliibukaa na kuzimwa na polisi.
Matukio ya kuchomana visu yalitokea karibu na baa ya Harry iliyopo katikati mwa Washington DC , lakini haikufahamika wazi waliodungwa visu walikuwa ni wa kundi gani, kuliongana na Gazeti la Washington Post.
Watu wanane walipelekwa hospitalini, wakiwemo maafisa wawili wa polisi , kulingana na televisheni ya CNN.
Waandamanaji wa kikundi cha Make America Great Again (MAGA) ,wanaomuunga mkono Bw Mr Trump, walinaswa kwenye kamera za video wakichana ishara ya vuguvugu la Black Lives Matter katika Kanisa, kuimwagia mafutra ya petroli na kuichoma moto.
Jumapili Mchungaji wa kanisa la Ashbury church alilinganisha kuchomwa kwa bendera hiyo na kuchomwa kwa msalaba.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
"Kuona kitendo hiki kwenye video kumenifanya nijizatiti kupambana na ushetani ambao kusema kweli ameibua kichwa chake kibaya " Mchungaji Rev Ianther Mills alisema katika taarifa yake

Chanzo cha picha, Reuters

Chanzo cha picha, Reuters
Maandamano pia yalifanyika katika Olympia,mji mkuu wa jimbo la Washington, Atlanta na St Paul, Minnesota.
Maanamano ya Washington DC yaliwajumuisha maelfu ya wafuasi wa bw Trump lakini walikuwa ni wacheche kuliko waliishiriki tukio swa na hilo tarehe 14-Novemba.
Washiriki wachache walikuwa wamevalia barakoa licha ya kuwepo kwa sheria za kukabiliana na corona ambazo zinawataka watu kuvaa barakoa wakati wanapokuwa katika maeneo ya umma.
Kulikuwa na hotuba ya Bw Trump akimsamehe Mshauri wa zamani wa masuala ya usalama , Michael Flynn, na Sebastian Gorka, afisa mwingine wa zamani wa White House.

Chanzo cha picha, Reuters
Bw Gorka alimuomba Bw Trump kutoacha kampeni yake ya kisheria - kuhusiana na madai ya wizi wa kura -ili kuhakikisha matokeo yanafutwa.
Trump alipata pigo kujbwa Ijumaa wakati mahakama ya juu zaidi ilipokataa kubatilisha matokeo ya uchaguzi katika majimbo manne yenye ushindani mkubwa ambako Bw Biden alishinda. Bw Trump hadi sasa ameshindwa zaidi ya kesi 50 zinazohusiana na uchaguzi.
Kelele za shangwe zilisikika wakati helikopta ya Trump , Marine One, ilipopita juu ya waandamanaji ikiwa imembeba Trump ambaye alikuwa anaelekea katika uwanja wa soka kutazama mechi ya jeshi la wanamaji huko West Point, New York.
Awali Bw Trump alitweet ujumbe kwa wafuasi wake:












