Space X: Wataalamu wa anga za mbali waondoka kutoka kituo cha Nasa

Roketi iliyorushwa kutoka kituo cha anga cha Kennedy katika jimbo la Florida Marekani

Chanzo cha picha, Reuters

Muda wa kusoma: Dakika 2

Wana anga za mbali wanne- watatu kutoka Marekani na mmoja kutoka China- wameanza safari kutoka katika jimbo la Florida kwa ajili ya uchunguzi katika kituo cha kimataifa cha anga za mbali (ISS).

Walisafiri kuelekea katika obiti katika roketi na kondena lenye muundo wa capsule vilivyotolewa na kampuni ya SpaceX.

Ni mara ya pili tu kwa kampuni hiyo kutoa hiyo.

Shirka la anga za mbali la Marekani Nasa limesema kuwa sasa linaingia enzi mpya ambayo safari za wana anga za mara kwa mara za kuelekea katika uzio wa chini wa dunia zinaendeshwa na wafanyabiashara.

Wataalamu hao wanne wanaokwenda katika kituo cha angaza mbali cha kimataifa -ISS- ni Wamarekani Michael Hopkins, Victor Glover and Shannon Walker, na mtaalamu wa angaza mbali mwenye uzoefu mkubwa kutoka Shirika la angaza mbali la Japan (Jaxa) mwana anga Soichi Noguchi.

Kwa kushiriki katika safari hii, Noguchi anakuwa ndiye mtu wa tatu pekee katika historia kuondoka duniani katika aina tatu tofauti za vyombo vya anga za mbali, ambapo awali alisafiri kwa kutumia vyombo vya Soyuz na kingine kilichofahamika kama shuttle hardware.

Crew 1

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Wataaamu wa anga za mbali wakizipungia mono familia na marafiki zao

Roketi hiyo ya wahudumu aina ya Falcon na kifaa cha ndani ambacho ndimo wanapokuwa wanaanga upande wa kushoto wa picha kiliondoka katika kituo cha Kennedy Space Center majira ya saa moja na dakika ishirini na saba za jioni kwa saa za Florida.

Itachukua muda wa zaidi ya siku moja kukifikia kituo cha kimataifa cha angaza mbali. Inatarajiwa kuwa kitatua kwenye uzio majira ya saa kumi alfajiri Jumanne.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Presentational white space

Kikosi hicho kitakapowasili, , kitajiunga na mwana wa Nasa, Kate Rubins ,Sergey Ryzhikov na Sergey Kud-Sverchkov shirika la anga la Urusi (Roscosmos).

Kuwa na watu saba kwenye kituo cha juu cha umbali wa kilometa 410 kitaogeza mara tatu kiwango cha sayansi ambayo inaweza kuoneshwa katika mazingira yake maalum .

Soichi Noguchi

Chanzo cha picha, EPA

Space X imesaini mkataba na Nasa wenye thamani ya zaidi ya pauni bilioni 2.3, kutengeneza, kujaribu na kurusha chombo cha anga.

Kama sehemu ya mahusiano, kampuni ilifanya maonesho mwezi Mei ambayo wanaanga Doug Hurley na Bob Behnken walikwenda kwenye kituo cha anga za mbali na kurejea duniani wakiwa salama.

Nasa ina makubaliano kama hayo na kampuni ya anga Boeing, ingawa huduma zake ziko zaidi ya mwaka zikiifuata Space X.

Presentational white space

Shirika hilo limesema mtindo wake mpya wa usafirishaji kwenda kwenye obiti karibu na dunia inaokoa mabilioni ya dola katika gharama za ununuzi.

Inakusudia kutumia fedha hizo kufadhili matarajio yake ya Mwezini na sayari ya Mars. Ili kufikia mwisho huo, Nasa inakaribia kujaribu roketi mpya kubwa ambayo itatumika kuwarudisha wanaanga kwenye uso wa mwezi, lengo ambalo linatarajia kufikiwa mnamo 2024, au muda mfupi baada ya mwaka huo.

Hopkins, Glover, Walker na Noguchi watasalia ISS kwa miezi sita.

Nasa ilisitisha safari zake za anga mwaka 2011. imekuwa ikinunua nafasi kwa wanaanga wake kwenye vyombo vya anga vya Soyuz ya Urusi.