‘Red, red wine': Maana ya alama za uchaguzi Afrika

Bobi Wine adjusting his red beret

Chanzo cha picha, AFP

Katika mfululizo wa barua kutoka kwa waandishi wa Afrika, Joseph Warungu anaangazia kwanini rangi nyingi na alama huwa ni jambo muhimu katika kutafuta mamlaka barani Afrika haswa katika msimu wa uchaguzi.

Short presentational grey line

Unakumbuka 'red red wine?' Simaanishi chupa ya mvinyo ambayo inayoweza kutoa hisia zako.

Ninazungumzia Red Red Wine… wimbo maarufu wa rege ulioimbwa na wanamuziki kutoka Uingereza UB40. Wimbo huo ulishika chati namba moja Marekani na Uingereza mnamo mwaka 1983.

Miaka thelathini na saba baadae, wimbo huo wa Red Red Wine unaweza kuwa na sababu kubwa kwa mwanamuziki wa Uganda ambaye ameamua kuwa mwanasiasa pia Bobi Wine.

Mbunge Bobi Wine ambaye jina lake la asili ni Robert Kyagulanyi ambaye anataka kuwania nafasi ya urais huwa anapenda kuvaa kofia nyekundu.

Lakini sasa Bobi Wine anaweza kuivaa kofia yake nyekundu baada ya uchaguzi , kwa kuwa tume ya uchaguzi imepiga marufuku kwa chama chake kutumia rangi hyo, kwa sababu chama kingine kimedai kumiliki rangi hiyo

1px transparent line

Nguvu ya rangi na alama katika kampeni za uchaguzi haziwezi kupuuziwa katika mataifa ya Afrika.

"Alama ikiwa rahisi , inakuwa rahisi kwa vyama kuwafikia wafuasi wake.

Wengine huwa wanadhani ni muhimu kuwa na ishara inayowahusisha watu na matumaini na maisha kwa ujumla, alisema Dkt Isaac Owusu-Mensah, mhadhiri kutoka idara ya sayansi ya siasa chuo kikuu cha Ghana.

Alitumia mfano wa vyama viwili vikuu ambavyo ambavyo vinawania uchaguzi mwezi Desemba chinini Ghana.

"Chama cha upinzani cha NDC kina alama ya mwamvuli ikimaanisha . unaweza ukajifunika na mwamvuli haswa wakati wa shida," alisema Dkt Owusu-Mensah.

"Wakati kwa upande wao NPP wao wana alama ya tembo , ambaye ni mkubwa. Hivyo wanaweza kuondoa tatizo lolote ambalo liko mbele yako.

Wakati upo kwenye changamoto , inabidi uwe chini ya tembo basi utakuwa vizuri tu."

'Nyekundu ni kwa ajili ya maisha'

bobi

Chanzo cha picha, AFP

Dkt Mshai Mwangola, kutoka Kenya, anasema rangi za Afrika Magharibi zinaonekana zina maana kidogo katika kutoa ishara ya jambo.

Kwa mfano ukiihusisha rangi nyekudu na chama cha Labour nchini Uingereza lakini chama cha conservative Republican cha Marekani - na British Conservatives wanatumia bluu kama chama cha Democrats, cha Marekani.

"Barani Afrika, watu wanafahamu rangi hizo kuwa zina maana kubwa…tunajali sana kusoma kuhusu masuala ya kisiasa katika nyanja mbalimbali," alisema Dkt Mwangola.

Hii ikimaanisha kuwa hata bendera za taifa katika mataifa mengi ya Afrika kulikuwa na harakati za kupata uhuru na watu wengi waikufa, kama vile Kenya.

"Alama ya rangi nyekundu ikiwa ina maanisha damu ambayo ilipotea; rangi nyeusi huwa inawakilisha watu weusi katika taifa hilo na kijani ni inawakilisha mazingira au ardhi ambayo walikuwa walikuwa wanaipambaniawa," alisema.

Hayo ni maoni ambayo yalitolewa na Dkt Owusu-Mensah.

2px presentational grey line

Siku za Uchaguzi barani Afrika

  • Guinea:Oktoba 18
  • Seychelles: Oktoba 22-24
  • Tanzania: Oktoba 28
  • Ivory Coast: Oktoba 31
  • Ghana: Desemba 7
  • Jamuhuri ya Afrika ya Kati: Desemba 27
  • Niger: Desemba 27
  • Uganda: 10 Januari - 8 Februari 2021
2px presentational grey line

Tume ilichagua matunda mawili ambayo yanafahamika - rangi na machungwa na ndizi.

Lakini raia wa Kenya bado wanasoma maana yake.

Kampeni iliona jinsi wanasiasa walivyopambana, wakiwa na madai ya ajabu kuhusu ndizi na rangi ya rangi ya machungwa.

L: A "yes" voter with a banana R: A "no" voter with oranges during campaigning ahead of Kenya's 2005 referendum on a new constitution

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Wakenya wakifurahia ishara ya matunda mwaka 2005

Mwisho wa siku chama cha oranges kilishinda na kura ya maoni ilikataliwa.

Banana ikashindwa.

Makundi ya kisiasa ambayo yalipata ushindi katika uchaguzi huo yalichukua jina la chungwa kuwa jiana lao jipya la chama chao kipya cha siasa.

Leo Orange Democratic Movement (ODM), inaongozwa na waziri mkuu wa zamani Raila Odinga, ni chama kikuu cha upinzani nchini Kenya.

Alama za 'uchawi ' zilipigwa marufuku

Lakini sio alama zote zinazokubaliwa katika uchaguzi kama tulivyoona katika uchaguzi wa mwaka 2018 nchini Zimbabwe.

Tume ya uchaguzi ya Zimbabwe (Zec) ilipiga marufuku aina zote za nembo zilizokuwa zikitumiwa na wagombea, wakiwemo baadhi ya wanyama na silaha.

Ungeweza kuwa na silaha kama nembo yako lakini sio duma au chui.

Kwa busara yake , Zec huenda ilitambua kwamba kuna chaguzi nyingi barani Afrika ambazo watu hawashindi kwa kura bali kwa "uchawi" , ambao kwa kawaida huiywa wizi wa kura.

Kwahivyo mamba na bundi - ambao wanausishwa na uchawi nchini Zimbabwe - walipigwa marufuku katika orodha ya nembo za wanasiasa na vyama.

Tikiti maji lina sharubati (juisi) na ni tunda tamu. Lakini nchini kenya lina maana yake ya kisiasa nchini Kenya: mwanasiasa ambaye hana msimamo thabiti - kijani kibichi na mgumu nje, mwekundu na anayeweza kupondwa ndani kwa urahisi.

Sio mtu wa kuaminika. Kwahiyo huwezi kupata bango la kampeni lenye alama ya tikiti maji (watermelon).

Dkt Owusu-Mensah anadai kwamba alama za kisiasa zina nguvu sana, mara kwa mara huchukua nafasi ya utambulisho halisi wa wamgombea.

1px transparent line

"Nimetoka tu hivi karibuni katika jimbo la kaskazini mwa Ghana ambako tuliwahoji watu kuhusu ni nani ambaye watamchagua katika uchaguzi ujao.

Takriban 95% yao walitumia alama zao tu za tembo na mwavuli . Hawakuwa kutaja majina ya wagombea au vyama vyao ."

Nilipokuwa ninakuwa kijini kwetu katikati mwa Kenya, nilifikiri kuwa jina la mbunge wetu aliyehudumu kwa muda mrefu lilikuwa ni "Tawa" ikimaanisha taa kwa lugha yangu.

Hiyo ilikuwa ni kwasababu taa ndiyo ilikuwa alama yake katika kila uchaguzi. Wakati alipoingia kijijini kwetu na wafuasi wake eneo lote lilijaa watu waliopaza sauti wakishangilia "Tawa! Tawa!"

Lakini naweza kusema kuwa, taa yake ilikuwa haina mwangaza. Haikumulikia elimu yetu na changamoto za kisiasa. Haikuleta umeme kwenye eneo letu wala kuboresha barabara ambazo zilikuwa hazipitikikatika msimu wa mvua.

Dkt Mwangola anaafiki kuwa huku tukiwa wazuri sana katika kupata maana ya rangi na alama barani Afrika, tunashindwa kwa kutofuata rangi hizo.

Uganda's President Yoweri Museveni dressed in yellow - 2016

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Rais wa Uganda akiwa amevalia mavazi ya rangi manjano alipokuwa katika kampeni mara ya mwisho

"Sisi kama wapiga kura haturudi nyuma na kuwawajibisha wagombea kuhusu alama zao. Kama mtu alikuwa na alama ya taa au alikuwa ni shoka, trekta au simba, sijali tena.

Hatuwajibishi hata vyama vya kisiasa kwa alama zake.

Serikali ya Uganda inatambua kikamilifu nguvu ya alama za chama .

Mwaka mmoja uliopita , iliamua kutangaza kuwa kofia nyekundu ni sehemu ya nguo za sare rasmi ya jeshi kwa hivyo mtu ambaye si mwanajeshi akiivaa anaweza kufungwa jela.

Licha ya kwamba Bobi Wine anaonekana kupuuza uamuzi huo pia.

Dkt Mwangola anaamini kuwa Bobi Wine huenda alichagua rangi zake kuwasilisha hasira kwa ajili ya kukabiliana na rangi ya manjano ya chama tawala cha NRM , kinachoongozwa na Rais Yoweri Museveni ambaye anagombea muhula wa sita madarakani.

" Rangi ya Manjano ni ya mwangaza wa jua na furaha. Wale wengine wanasema : 'Hapana, tuna hasira!'… imepingwa na nyekundu ya ari na utashi wa kufanya mambo ," anasema.

"Manjano ni kuhusu mafanikio, lakini rangi nyekundu ni kusema : 'mafanikio kwa ajili ya nani ?'"

Kama wapiga kuwa wa Uganda wanaiona rangi nyekundu ifikapo Januari ijayo, Bobi Wine atakuwa akinywa Mvinyo mwekundu- red wine katika Ikulu.

Presentational grey line