Brazil: Wanawake wanaoua watoto wao baada tu ya kuzaliwa

Ilustração de uma mulher com bebê no colo
Maelezo ya picha, Wanawake wengi nchini Brazil hushutumiwa kwa mauaji na pia kwa kosa la kuficha mwili wa mtoto aliyesemekana kumuua.

Ana Carolina Moraes da Silva alikuwa amelala pamoja na binti yake wa miaka 2. Lakini akaamka akitaka kwenda chooni bila kujua kwamba ni mjamzito, alianguka na ujauzito ukatoka.

Alipoamka, alihisi kondo la nyuma linaangukia mtoto. "Niliona mtoto ambaye hana uhai, amejaa damu na kila kitu kikawa ni chenye kuogopesha."

Kilichofuata baada ya hapo, alichukua kanga akamfunga nayo binti yake vizuri na kumuweka kwenye mfuko wa plastiki kama zawadi iliyotoka kwa mama hadi kwa binti yake na kumtupa mtoto huyo mchanga aliyetoka kujifungua tu kwenye jalala la takataka nje ya jengo.

Familia hiyo ilikuwa inaishi ghorofa ya 6 ambapo kulikuwa na mabomba yanayokwenda hadi kwenye jalala ghorofa ya chini. Binti huyo hakunusurika.

"Niliogopa sana, Nilimtupa mtoto wangu, Nilimpoteza binti yangu, lakini wananishutumu kwa kumuua. Sijui kwanini sikupiga simu na kutafuta usaidizi kwa serikali. Yaani kipindi hicho sikuwa nafikiria chochote. Mungu amenisaidia kutoshikwa na wazimu lakini siwezi kusahau kilichotokea. Ni kama hakuna nilichowahi kufanya kabla chenye maana. "

Aliyekuwa mwanasarakasi mwenye umri wa miaka 31, aliandika barua kwa BBC News Brazil akielezea kile kilichotokea Juni 27, 2018, siku ya kifo cha binti yake wa pili.

Kuna kurasa 10 zilizoandikwa kwa mkono kwa wino mwekundu kutoka gereza la 18, huko Sao Paulo, ambapo Ana Carolina amefungiwa tangu Julai 3, 2018, alishutumiwa kwa mauaji na pia kwa kosa la kuficha mwili wa mtoto aliyesemekana kumuua.

Carta de Ana Carolina Moraes da Silva para el reportaje de la BBC
Maelezo ya picha, Mama mmoja aliandika kile kilichotokea kwa wino mwekundu baada ya kushutumiwa kumuua mtoto wake

Kina mama wanaoua watoto wao wachanga wanaweza kuhukumiwa kwa makosa ya mauaji kwa kukusudia au kwa kumuua mtoto wake.

Tofauti kati ya makosa hayo mawili ni kwamba kumuua mtoto wake kunaweza kusababishwa na shinikizo fulani kulingana na sheria ya 123 ya Brazil, ama wakati wa kujifungua au muda mfupi tu baada ya kujifungua.

Dibujo de una mujer con las manos en la cabeza
Maelezo ya picha, Sheria iliyopitishwa miaka 80 iliyopita ya kuhukumiwa kwa kosa la mauaji ya mtoto wako nchini Brazil bado inazua gumzo hadi hii leo

Lakini kwanini wanalilia kuhukumiwa kwa kosa la mauaji ya mtoto wako? Hii ni kwasababu adhabu ya kosa hilo ni kifungo cha miaka 2 hadi 6 huku kosa la mauaji ya kukusudia kifungo chake kikiwa ni miaka 20 gerezani au hata zaidi kulingana na uzito wa kesi.

Ukweli ni kwamba tangu kupitishwa kwa sheria hiyo, takriban miaka 80 iliyopita, hakujakuwa na maridhiano kuhusu sheria hiyo. Kesi yake inaweza kuchukua muda gani? Kama kuna ushahidi na kama kunahitajika ripoti ili kuthibitishwa kwa mauaji.

"Yote hayo yanatokea kutoka kwa fikra za madaktari walio kwenye ulingo wa sheria na sheria za uhalifu," amesema mwanaanthropolojia na wakili Bruna Angotti.

Hili lina maanisha kwamba mwanamke anayeshutumiwa kumuua mtoto wake mchanga anaweza kuonekana ama kuwa muhalifu zaidi au kinyume chake kulingana na mtazamo wa mama atakaopewa.

Nini kinachopelekea vifo vya watoto hao?

Angotti amezungumzia kesi saba mahakamani na zingine 179 ambazo hukumu yake ilitolewa kati ya mwaka 2005 na 2015 na pia alishiriki kwenye majopo matatu ya majaji.

Majopo hayo yaligusia kuwa adhabu zilizotolewa ni kati ya kifungo cha miezi sita hadi miaka kumi na saba unusu gerezani, ingawa adhabu ya kosa hilo la uhalifua inatolewa kwa kuzingatia vigezo kadha wa kadha.

Pia kuna yanayofanana, wengi wa wanawake hao walikuwa wanaishi peke na hawakukubali hali zao au walificha mimba zao ama wanazalia nyumbani.

Nyingi ya kesi, ni mara ya kwanza wanawake hao wanatekeleza uhalifu, ni maskini, na mara nyingi wamekuwa waathirika wa dhulma za nyumbani.

"Badala ya kumzika mtoto, kwa mfano, wanaifungia maiti sehemu, anamuweka juu ya mashine ya kuosha nguo au chini ya kitanda," amesema Angotti.

Na kifo cha mtoto mara nyingi husababishwa na kunyongwa, wanakoseshwa pumzi, wanashambuliwa, wanazamishwa majini au mtoto anatupwa.

Ukosefu wa takwimu za kutosha

Katika sheria ya kimataifa, kifo cha mtoto kinachukuliwa kuwa mauaji ya aina hiyo kikitokea ndani ya saa 24 baada ya mama kujifungua. Lakini baada ya hapo hadi mwaka mmoja huchukuliwa kama mauaji ya mtoto wako.

Takwimu za matukio hayo ni nadra sana na wakati mwingine sio sahihi kwasababu kesi hizo mara nyingi huwa hazirekodiwi na pia miili ya watoto waliokufa wakati mwingine huwa haipatikani.

Una mujer acostada en una clínica de abortos

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Inasemekana idadi kubwa ya wanawake wanaojitapa kwenye shutuma za kuua watoto wao wanayopitia yanafanana kwa kiwango kikubwa

Mratibu wa kliniki ya wanawake wajawazito, Iaconelli aliitwa na shangazi wa msichana mmoja kwenda katika hospitali ya kuzalia kina mama Sao Paulo.

Mwanamke huyo kijana alikuwa amefikishwa chumba cha wagonjwa mahututi akiwa na maumivu ya sehemu ya chini ya tumbo. Bila kujua sababu ya tatizo hilo.

Alikuwa ameficha ukweli kuwa amekunywa dawa akitaka kuavya mimba ya miezi minne.

Daktari aliyemtibu hakujua kama ni mjamzito na moja kwa moja alichofanya ni kumpa dawa ya kutumia.

Baada ya muda, msichana huyo aliomba funguo ya kuingia chooni ili ajisaidie na alipoingia akajifungua mtoto wa kike ambaye hakuwa anapumua kwasababu bado alikuwa amejishikilia kwenye kondo la nyuma.

Alichofanya ni kumchukua na kumuweka ndani ya dude la takataka, akarejesha kifunguo na akaondoka hospitalini. Lakini akaitwa tena hospitali na alipotia guu tu, polisi alikuwa anamsubiri.

Mujer acostada con los ojos abiertos

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wanawake wanaoua watoto wao kwa kiasi kikubwa hupitia ugonjwa wa sonona

Jaribio la kujitoa uhai

Katika kisa cha aliyekuwa mwanasarakasi wa viungo Ana Carolina, wakili wake aliomba mahakama imchukulie kama mtu ambaye hawezi kuwajibika yaani asiyeweza kuchukua msalaba wa matendo yake kwasababu ya matatizo ya kiakili aliyokuwa nayo kabla ya kupata ujauzito.

Hata hivyo, hakuwahi kutafuta tiba na hivyo basi alikosa ushahidi wa kuthibitisha hilo.

Akiwa gerezani, muda mfupi baada ya kifo cha binti yake, Ana Carolina alijaribu kujitoa uhai kwa kutumia uma na kifuniko cha alumini cha kontena ya chakula.

Lakini kulingana na sheria, hakimu alitoa hukumu yake kwa kuzingatia kosa la mauaji na kujaribu kuficha ukweli kwasababu alifahamu kwa kiwango fulani kitendo alichokuwa anatenda.

Na mwili wa mtoto aliyetupwa kwenye jalala la takataka na Silva, ulipatikana siku iliyofuata na mtu aliyekuwa anachukuwa taka hizo kwa ajili ya kuzichakata upya.

Wazo la kwamba mwanamke mjamzito moja kwa moja ni mama lipo kwa mitazamo tofauti tofauti, wakati mwingine bila hata ya wengine kufahamu kwamba mwanamke huyo anahitaji usaidizi ili aweze kufahamu hilo.

Mwanaanthropolojia na wakili Bruna Angotti anaelewa kwamba haki haizingatii kizungumkuti kilichopo katika suala la mauaji ya mtoto wako kwasababu ya vigezo vingi vinavyoandamana na suala hilo. Lakini kwake. hukumu inastahili kulenga msamaha kwa kuzingatia kwa karibu afya ya mama, ndani na nje ya hospitali na hatua za kiusalama.