Je Umma unapaswa kumhukumu Kanye west kwa afya yake ya akili?

Chanzo cha picha, Reuters
Kama muimbaji na mzalishaji wa muziki wa mitindo ya kufokafoka, ameweza kutoa muziki ambao umeuza zaidi na muziki ambao umependwa wa enzi yetu.
Ndoa yake na nyota wa tamthilia ya Televisheni ya maisha halisi imemfanya kuwa sehemu ya mojawapo ya wanandoa maarufu duniani.
Ni baba na mbunifu mwenye mafanikio asiyeogopa kuzungumza wazi au kuwa na mahusiano ya kimapenzi.
Wakati mmoja alimshutumu rais wa zamani wa Marekani George W Bush kuwa mbaguzi katika matangazo ya moja kwa moja, na akasema rais wa sasa ana "nguvu za mnyama aitwaye dragon".
Aliwashangaza na kuwashitua watu wengi baada ya kumuaibisha mwanamuziki Taylor Swift jukwaani. Hivi karibuni alitangaza , sio mara ya kwanza, kwamba anagombea urasi wa Marekani .
Yote haya na mengine mengi yamemfanya kuwa mtu ambaye Umma unapenda kufuatilia maisha yake.
Hiki ni kitu muhimu ambacho hatukifahamu kumuhusu Kanye West - utendaji wa ndani wa mawazo yake.
Kwamba hilo linapaswa kubakia kuwa jambo lisilojulikana ni kitu ambacho kitakumbukwa katika uzinduzi wa kampeni ambapo suala hili lilijadiliwa na kufuatiwa na misururu ya ujumbe wa tweeter.
Mkutano wa kampeni, na ujumbe uliotumwa kwenye mitandao ya habari ya kijamii, vimeibua maswali. Baadhi ya watu wamekua wakimkejeli. Tabia zake zimekua ziliitwa "za mtu asiyeeleweka".
Lakini je ni matendo gani aliyoyafanya hivi karibuni?

Chanzo cha picha, EPA
Hali ya West ni ngumu na isiyoeleweka kutokana na ukweli kwamba amekuwa wazi juu ya afya yake ya akili.
Mwaka jana, alisema kuwa ana ugonjwa wa bipolar unaomfanya mtu kuwa na hisia au kufanya mambo kupita kiasi akijielezea kuwa alikua katika hali ya "hisia za kufanya mambo kupita kiasi " na akaomba watu wamuelewe.
"Ni tatizo la kiafya ambalo lina unyanyapaa mkubwa juu yake na watu wanaruhusiwa kusema chototote juu yake na kukubagua kwa namna yoyote ile. Hii ni kama kuteguka kwa ubongo, kama kuteguka kwa fundo la mguu. Na kama mtu ameteguka fundo la mguu huwezi kumsukuma zaidi," alisema.
Jumatano, mke wake Kim Kardashian West alielezea tatizo lake kwa Umma kwa uwazi kupitia mtandao wake wa Instagram.
Ameandika: "Lakini leo, Nahisi nizungumze kitu kwasababu ya unyanyapaa na dhana potofu kuhusu afya ya akili.
"Kama wengi mnavyoweza kua mnafahamu , Kanye ana bi-polar. Yeyote mwenye tatizo hili ana mtu katika maisha yake anayefahamu jinsi lilivyo vigumu na kuumiza na la kuumiza kulielewa," aliandika.
"Wale wanaoelewa matatizo ya akili au hata tabia ya kulazimisha wanajua kwamba familia huwa haina la kufanya labda mtu awe hajafikisha umri wa kutambulika kama mtu mzima.
"Watu wasiofahamu au ambao hawajapitia hili wanaweza kuhukumu mtu na wasielewe kwamba watu binafsi lazima wazungumze katika mchakato wa kupata usaidizi hata familia na marafiki wajitahidi kwa kiasi gani."
Kardashian West aliendelea na kusema kwamba mume wake anakosolewa kwasababu yeye ni mtu maarufu na matendo yake wakati mwingine yanaweza kusababisha maoni na hisia kali", lakini akaomba watu kuwa na huruma kupita maelezo na uelewa.
Ni "mtu mzuri lakini mgumu " ambaye " maneno yake wakati mwingine hayaendani na utashi wake ", aliongeza .

Chanzo cha picha, PA Media
Zingatia unachokijua
Ujumbe mwingi kutoka kwa wataalamu wa afya ya akili ni kwamba, hakuna mtu yeyote, hata wenye taaluma, anayeweza kujaribu kubashiri kile ambacho mtu binafsi anakipitia , hata awe maaruhfu kivipi.
Tetesi hazinabudi kuepukwa, wanasema, sio tu kwa mtu mzuri machoni pa umma bali kwa uelewa mpana wa afya ya akili.
" Unapaswa kufikiria juu ya watu wotewengine duniani ambao huenda wanahangaishwa na tatizo la aina hiyo na kufikiria inachomaanisha kwa wale wanaozungumziwa machoni pa umma ," anasemavPeter Kinderman, Profesa wa tiba ya kisaikolojia katika Chuo kikuu cha Liverpool.
Profesa Kinderman anasema tabia zisizo za kawaida zinaweza kuchunguzwa lakini ni muhimu zisihusishwe na matatizo ya afya ya akili.
"Ingekua mgombea yule anayegombea urais angekuwa ana tatizo la kutoeleweka anachosema kwa mfano labda sio mzungumzaji mzuri na labda ana kigugumizi . Toa ushahidi. Kama unafikiri kuna ushahidi kwamba mtu anatoa madai ya ajabu na ambayo hayana maana, basi wanafanya maajabu hawasemi lolote la maana. Iwe ni kweli mtu anaamua kwamba hilo limetimiza vigezo kwa mtu kusemekana ana ugonjwa wa akili wa bipolar hilo ni suala jingine ."
" Zinagatia ukweli, zingatia kile ambacho watu wanafanya, na usifuate uvumi juu ya uwezekano wa sababu za kiakili kwamba ndizo zinazosababisha tabia za watu ," anasema.
Uwe mkarimu na anayejenga
Kwa mshauri wa kisaikolojia Dkt Carolyne Keenan, mtu maarufu anayetoa uelewa juu ya afya ya akili na kusababisha mjadala inaweza kuwa na athari chanya.
Lakini anasema hali hiyo inahitaji kutofautishwa na idadi
"Hatujui ni nani anadhibiti akaunti zake za mitandao ya kijamii. Kwahiyo tunakipa thamani ya kile ambacho kinatangazwa katika wavuti kwamba ni maneno yake, lakini kusema ukweli hatujui ," anasema.
" Hatumjui mwanaume huyu, mwaume halisi ambaye yuko nyuma ya sura ya mtu huyu maarufu anapitia uzoefu gani ."
"Ninadhani kila mtu - watu maarufu, wanahitaji kukumbuka kwamba hawajui hadithi kamili. Na kwa hiyo hata kutoa maoni kusema ukweli ni vigumu kwasababu hufahamu ni nini unachokizungumzia ."
"Kuzungumzia sana magumu haya yawe ni kwa watu wa kawaida au watu maarufu ni tatizo kwa kweli kwa kila mtu ambaye anapitia tatizo la afya ya akili kwasababu inatoa picha ndogo ya kile ambacho kinaweza kuwa kinaendelea ."
Watu wanapaswa kujibu kwa "udadisi na ukaribu" kama wanahisi wanahitaji kumjibu West, anasema. Au usiseme lolote kabisa
Wazo la ukarimu linaweza kuwa ni jambo lisilopendwa katika dunia ambayo mara nyingi huwa katili kwa watu maarufu na mitandao ya kijamii lakini licha ya kutuma ujumbe hasi kumekuwa na ongezeko la hofu na mjadala mpana wa masuala husika.
Baadhi ya wachambuzi waliona kuna unafiki fulani katika kuhurumia, wakielezea ujumbe wa mzaha waliokabiliana nao waimbaji Azealia Banks na Britney Spears, ambao walikabiliwa na maswali ya Umma kuhusu afya yao ya akili
Wengine walielezea hofu yao kuhusu nembo za biashara zinazowatumia.
Moja ya majibu yaliyoshirikishwa zaidi lilitoka kwa muimbaji Halsey, ambaye alitoa wito wa watu kuwa na uelewa huku akikiri mwenyewe kuwa anahangaika na tatizo hili la afya ya akili la bipolar .












