Je, ni kwanini uteuzi wa Mkuu mpya wa mkoa wa Dar es Salaam umezua gumzo mitandaoni?

Makonda

Chanzo cha picha, Makonda

Muda wa kusoma: Dakika 3

Mabadiliko ya utawala wa jiji la kibiashara la Dar es salaam yameibua hisia chungu nzima baada ya aliyekuwa mkuu wa mkoa huo Paul Makonda kubwaga manyanga na badala yake kuamua kuingia katika siasa.

Makonda ambaye mtindo wa uongozi wake pamoja na matamshi yake ulizua utata ameamua kuwania kiti cha eneo bunge la Kigamboni lililoko mkoani humo.

Na kufuatia kuondoka kwa bwana Makonda rais John Pombe Magufuli aliamua kumteua mkuu mpya wa mkoa huo Aboubakar Kunenge kuchukua nafasi hiyo

Lakini maoni katika mitandao ya kijamii, hasa Twitter yanaonesha uteuzi wa Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam umeibua minong'ono mingi kumuhusu.

Hii ni kutokana na umaarufu wa Bwana Makonda, ambaye uongozi wake umezua utata na kusababisha mijadala ndani na nje ya jiji hilo.

Miongoni mwake ni kuhusu wajane waliotelekezwa, vita vya makahaba , madawa ya kulevya pamoja na wapenzi wa jinsia moja na mambo mengine mengi ambayo yaliibua hisia nyingi katika uongozi wake.Baada ya uteuzi wa mkuu mpya wa mkoa Dar es Salaam, watumiaji wa mitandao wamekuwa na maoni mbali mbali .Mmoja wao alisema:"Dar es Salaam, mmepata uhuru au?"...

'Mi nakumbuka amri yako tusifungue maduka Jumamosi mpaka saa nne kwa hiyo mikate ikabidi Ijumaa tusiwe tunanunua na kila miezi mitatu tuna kodi ya TRA hatutakusahau daima mkuu'

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Sioni haja ya watu kushangilia kutumbuliwa kwa Makonda nyakati hizi za lala salama, angetumbuliwa kipindi hicho kilipaswa atumbuliwe ingekaa poa sana, Babalie aliandika kwenye tweeter.

Huku mfuasi mwingine akihoji kuwa "Ni juzi tuu tuliambiwa ma RC na ma DC hawapaswi kuhangaika na ubunge wanapaswa kuwajibika na nafasi zao mpaka wamalizee uwajibikaji katika nafasi zao lakini nashindwa kuelewa usahaulifu wa kauli ndiyo tatizo au hakuna mawasiliano mazuri katika ngazi ya uongozi?"

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

"Hivi kwani ubunge una nini hasa mpaka mkuu wa mkoa anaacha nafasi kubwa hiyo anakimbilia kwenye ubunge?

Baadhi ya hatua kumuhusu Makonda zilizoibua gumzo:

  • Suala la ushoga:

Uongozi wa Bwana Makonda uligusa hata nyanja za kimataifa, likiwemo tangazo alilolitoa la kuwakamata na kuwashitaki mashoga, kampeni aliyoiongoza katika mkoa wa Dar es salaam. Hatua hiyo ilipingwa vikali na wanaharakati wa haki za binadamu .

Hata hivyo baadae Serikali ya Tanzania kupitia aliyekuwa waziri wa mambo ya nje, ilitangaza kujitenga na kampeni ya kuwakamata na kuwashtaki mashoga ilioongozwa na Makonda.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania iliyotolewa Jumapili, Novemba 4 ilidai kampeni hiyo ni mawazo binafsi ya Makonda na sio msimamo rasmi wa serikali.

  • Kupigwa marufuku kuingia Marekani.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Ijumaa, Januari 31 2020 iloisema kwamba marufuku hiyo pia inamhusisha mke wa Makonda Bi Mary Felix Massenge.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Makonda alishutumiwa kwa kushiriki katika ukandamizaji wa haki za binaadamu, ikiwa ni pamoja na kunyima watu haki ya kuishi, haki ya uhuru wa kujiamulia mambo na usalama wa watu.

"Wizara ina taarifa za uhakika kuwa Makonda amehusika katika uvunjifu huo wa haki kupitia nafasi yake kama mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam. Katika nafasi yake hiyo, pia amelaumiwa kwa kukandamiza upinzani , kukandamiza haki ya kujieleza, na kushambulia makundi yasiyo na sauti," iilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

  • Hatua ya kuwatetea wanawake waliotelekezwa na waume zao.

Katika hatua nyingine ya kukabiliana na mienendo ya wanaume mwanzoni mwa mwezi wa Agosti Bwana Makonda alitangaza kuwa amepanga kuzisajili ndoa zote za mkoa huo kwa ajili ya kukabiliana na wanaume wanaowalaghai wanawake kimapenzi.

Kufuatia taarifa hiyo mamia ya wanawake walijitokeza na kwenda katika ofisi yake kuelezea machungu waliyodai kupitia kutokana na kutelekezwa na waume zao.

Alisema kuna mpango wa kuanzisha kanzidata ya ndoa zote zilizopo kwenye mkoa wake ili kupunguza utapeli wanaofanyiwa wanawake kwa kudanganywa kuolewa.

Makonda alisema yuko tayari kuchukiwa na wanaume wa Mkoa huo wanaokwazika na uamuzi wake wa kuwatetea wanawake, na kwamba hawezi kukaa kimya kuangalia mateso ya wanawake yanayoweza kupatiwa ufumbuzi ikiwa wanaume watabadilika.

  • Utata juu ya mzozo wake na muhubiri pamoja na agizo la mahubiri vilabuni:

Wakati wa utawala wake amekua na mgogoro na muhubiri maarufu nchini Tanzania Joseph Gwajima kitu ambacho kiliibua majibizano ya maneno yaliyovutia mijadala kwenye vyombo vya habari.

Aidha Bwana Makonda aliibua mjadala kwenye mitandao ya kijamii miongoni mwa Watanzania, mwezi Septemba mwaka jana wakati alipotangaza kuwa anatoa kibali kwa viongozi wa dini kwenda kuhubiri kwenye kumbi za burudani usiku ili watu wasikie neno la Mungu, wasije kusema hawakusikia.

Alitoa onyo kwa wamiliki wa klabu watakaozuia watumishi hao, na kwamba yeye ndiyo Mkuu wa Mkoa

Aidha alitoa amri ya kufungwa kwa vilabu vya pombe saa sita usiku, jambo lililopingwa vikali na baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam.