Fahamu Makanisa yaliyobadilishwa kuwa misikiti na Misikiti iliobadilishwa kuwa makanisa duniani

Jumba la Hagia Sophia lina muhimu mkubwa kidini na kisiasa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jumba la Hagia Sophia lina muhimu mkubwa kidini na kisiasa

Kumekuwa na mjadala mkali kuhusu jumba la Aya- Sufiya ambalo lilibadilishwa na kuwa msikiti baada ya takriban miaka 90 likiwa makavazi.

Viongozi wa kisiasa na wale wa kidini walitoa maoni yao , lakini rais wa Uturuki Erdogan alitetea uamuzi uliotolewa na mahakama.

Hivyobasi tunaangazia kuhusu majumba matano ambayo yalikuwa misikiti na kufanywa makanisa ama yale yaliokuwa makanisa na kubadilishwa kuwa misikiti.

1- Hagia Sophia - Uturuki

Makavazi hayo maarufu mjini Istanbul - yamebadilishwa na kuwa msikiti. Jumba hilo lilikuwa kanisa la Orthodox.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alitangaza uamuzi huo baada ya mahakama kuamuru kwamba kania hilo ni jumba la kumbukumbu.

Eneo hili ni mojawapo ya maeneo yanayowavutia sana watalii nchini Uturuki

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Eneo hili ni mojawapo ya maeneo yanayowavutia sana watalii nchini Uturuki

Hagia Sophia ilijengwa kama hekalu la Wakristo karibu miaka 1,500 iliyopita na baadae kugeuzwa kuwa msikiti baada ya mapinduzi ya Ottoman ya mwaka 1453.

Hekalu hilo lililotambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Unesco kama eneo la kihistoria duniani liligeuzwa kuwa makavazi ya kitaifa mwaka 1934 chini ya mwanzilishi wa nchi ya Uturuki padre Ataturk.

Lakini mapema wiki hii mahakama nchini Uturuki iliamuru kuondolewa kwa hadhi ya makavazi katika jengo hilo, ikisema matumizi yake mengine zaidi ya kuwa msikiti "haiwezekani kisheria".

Papa Francis alisema maneno machache kuhusu suala hilo: "Mawazo yangu yawafikie wakaazi wa Istanbul. Nifikiria kuhusu Santa Sophia nahisi uchungu sana."

Rais Recep Tayyip Erdogan amesema ibada ya kwanza ya Kiislamu itafanyika Hagia Sophia Julai 24.

Wengi wanataka haki ya kufanya ibada katika eneo hilo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wengi wanataka haki ya kufanya ibada katika eneo hilo

Historia ya eneo hilo la kihistoria duniani

  • Historia ya Hagia Sophia ilianza miaka 537 wakati wa utawala wa ukoo wa Justinian ulipojenga built kanisa kubwa ambalo urefu wake uliangalilia chini forodha ya Golden Horn.
  • Kutokana na mnara wake mkubwa, iliaminiwa kuwa kanisa na jengo kubwa zaidi duniani
  • Ilisalia mikononi mwa remained in Byzanite kwa Karne kadhaa isipokuwa mwaka 1204 wakati wanaharakati walipovamia mji huo.
  • Mwaka 1453, katika tukio ambalo lilikua pigo kubwa kwa Wabyzantine, Ottoman Sultan Mehmed II aliteka mji wa Istanbul (uliokuwa ukijulikana kama Constantinople) na kufanikiwa kusali ibada ya Ijumaa katika hekalu la Hagia Sophia
  • Ottomans baadae waligeuza jengo hilo mkuwa msikiti, na kuongeza minara mingine iliyofunika na kubadili muonekano ulioashiria lilikuwa kanisa kwa kuandika maneno ya kiarabu.
  • Baada ya karne kadhaa ya kuwa kati kati ya utawala wa Kiislam wa Ottoman, iligeuzwa kuwa makavazi mwaka 1934 katika juhuza za kuifanya Uturuki kuwa nchi isiyoegemea msingi wa dining moja.
  • Leo hii Hagia Sophia ni eneo maarufu zaidi nchini Uturuki, ambalo linavutia zaidi ya wageni milioni 3.7 kwa mwaka.

2- Msikiti wa Babri , Ayodhya - India

Mwaka 2019, jumba lililokuwa likipiganiwa la msikiti wa Babri uliopo katika eneo la Ayodhya kaskazini mwa India , lilibadilishwa na kuwa hekalu kupitia agizo la mahakama.

Wanasema kwamba msikiti huo awali ulikuwa hekalu na wakati Waislamu walipolichukua 1592 lilibadilishwa na kuwa msikiti.

Mahakama kuu ya India mjini Delhi ulitoa uamuzi huo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mahakama kuu ya India mjini Delhi ulitoa uamuzi huo

Kesi hiyo iliozua utata ilichukua muda mrefu kukamilika. Utata uliogubika kesi yote ni kuhusu nani kati ya Waislamu na Wahindu waliokuwa wamiliki wa kweli wa jumba hilo.

Mahakama ilisema kwamba Waislamu wanaweza kupatiwa ardhi kujenga msikiti mwengine.

Wahindu wengi wanaamini kwamba jumba hilo ndio alipozaliwa mungu Ram wanayemuabudu. Waislamu wanasema kwamba wamekuwa wakifanya ibada zao katika eneo hilo kwa vizaza na vizazi.

Utata ulizuka lakini ukachukua mwelekeo wa ujenzi wa msikiti wa babri ambao ulimilikiwa na Waislamu katika karne ya 16.

1992, Wafuasi wa dini ya Hindu waliojawa na ghadhabu walivamia msikiti huo na kuuharibu. ghasia hizo zilisababisha vifo vya watu 2000.

BBC

Jumba la Dhismaha masaajidka Babri

Mahakama ilisema kwamba ushahidi uliopatikana ulionesha kwamba jumba hilo halikujengwa na Waislamu .

Uchunguzi ulifanyiwa mabaki ya msikiti huo ulioharibiwa.

Mahakama iliamuru kwamba Dhimsaha litarudishwa chini ya umiliki wa Hekalu la mungu Ram na kwamba Wasialmu watapewa ardhi kwengineko kujenga msikiti.

Hatahivyo mahakama ilisema kwamba uharibifu wa msikiti wa Babri ulikuwa haramu.

Baraza la Waislamu ambalo halikufurahishwa na uamuzi huo wa mahakama lilisema kwamba halitakata rufaa.

3- Msikiti wa Cordoba

Mwaka 2014 , mamia ya maelfu ya watu walitia saini kesi kulibadilisha jumba la Cathedral kuwa kanisa katoliki.

Mmoja ya waliowasilisha kesi hiyo mahakamani alisema, kwamba kuna jaribio la kutaka kuondoa alama za msikiti na kanisa hilo.
Maelezo ya picha, Mmoja ya waliowasilisha kesi hiyo mahakamani alisema, kwamba kuna jaribio la kutaka kuondoa alama za msikiti na kanisa hilo.

Jumba hilo awali lilikuwa likitumika kama msikiti uliojengwa na taifa la Kiislamu la Andolisia kabla ya kuwa kanisa la Cathedral katika karne ya 15.

Jumba hilo lililoanza kujengwa na Waislamu na kurekebishwa na Wakristo linamiliki alama za dini zote mbili. Jumba hilo hilo bado linazongwa na utata kuhusu umiliki wa Wakristo .

Mmoja ya waliowasilisha kesi hiyo mahakamani alisema, kwamba kuna jaribio la kutaka kuondoa alama za msikiti na kanisa hilo.

Lakini wakatoliki wamekana kwamba wanataka kubadili historia ya jumba hilo na wanaamini kwamba jumba hilo liliwahi kuwa msikiti.

''Sio rahisi kuondoa historia ya kiislamu ya jumba hili'', Kiongozi wa kanisa katoliki aliambia BBC 2014.

Jumba hilo hutembelewa na takirban watalii milioni 1.3 kutoka kote duniani.

4-Uingereza- kanisa la zamani lilibadilishwa na kuwa msikiti.

Mwaka 2007, baraza la mji mmoja wa Uingereza lilipiga kura kubadilisha kanisa la zamani kuwa msikiti. Hatua hiyo ya baraza la mji wa Clitheroe lilisababisha mgogoro mbaya , ambao uliwaruhusu Waislamu walio wachache kupata mahala pa kuabudu.

5- Msikiti wa Granada

Mwaka 2003, Waislamu nchini Uhispania walifanikiwa kudhibiti msikiti wa waislamu wa Granada , ambao ulikuwa nje ya udhibiti wao kwa takriban miaka 500.

Mji ambao msikiti huo upo ndio uliokuwa ngome ya Waislamu wa Ulaya.

Siku ya ufunguzi wake , ilihudhuriwa na Waislamu wengi na maafisa kutoka katika serikali ya Uhispania.

Kulingana na Wasialmu , ukombozi wa msikiti huo ni mwamko wa Uislam na "heshima ya historia ya Waislamu".
Maelezo ya picha, Kulingana na Wasialmu , ukombozi wa msikiti huo ni mwamko wa Uislam na "heshima ya historia ya Waislamu".

Kulingana na Wasialmu , ukombozi wa msikiti huo ni mwamko wa Uislam na "heshima ya historia ya Waislamu".

Lakini raia wengi wa Uhispania hawakufurahia. Kila mtu amenyamaza wanaogopa kuzungumza, alisema katika msikiti mmoja wa mjini.

Takriban miaka 500 iliopita, Wakristo wa Uhispania waliliteka eneo la kusini mwa taifa hilo, na hivyobasi kumaliza utawala wa miaka 800 wa Ufalme wa Kiislamu wa Maqribibi.

Msikiti huo ni eneo la ibada kwa zaidi ya Waislamu 1000 wa Uhispania wanaoishi katika eneo hilo kulingana na kiongozi mmoja wa Waislamu eneo la Granada.