Uchaguzi Uganda 2021: Je ni kweli kampeni za kutumia redio zitaufungia upinzani Uganda?

Viongozi wa upinzani Kizza Besigye kulia na Bobi Wine Kushoto

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Viongozi wa upinzani Kizza Besigye kulia na Bobi Wine Kushoto

Kupigwa marufuku kwa mikutano ya kampeni nchini Uganda wakati taifa hilo likielekea kufanya uchaguzi mkuu mwezi Januari 2021 kunaweza kunufaisha chama tawala zaidi kuliko upande wa upinzani.

Hii ni kwa sababu radio ndio itaweza kuwa ndio njia bora zaidi ya kufikisha ujumbe huku wamiliki wa vyombo vyingi vya habari Uganda wakiwa wanasiasa wa chama tawala.

Ingawa chombo cha habari cha umma, Taasisi ya habari ya Uganda (UBC), inatumia lugha nyingi za nchi hiyo na kufika maeneo mengi, vituo vingi vya FM ni vya binafsi.

Hoja kubwa hapa ni kuwa wagombea wa chama tawala watakuwa na fursa ya kupata muda mwingi kuongea redioni tofauti na upande wa upinzani.

Mwanasaiasa wa upinzani Kizza Besigye aliwashtaki UBC baada ya uchaguzi wa mwaka 2016, kwa kukataa kumpa muda wa kuongea redioni - na mahakama ilitoa hukumu dhidi ya chombo hizo.

Taasisi ya Utangazaji ya taifa inapaswa kutoa muda sawa kwa sawa kwa wagombea wote wa siasa, lakini kiuhalisia jambo hilo halitendeki.

Zamani, Vituo vya redio katika maeneo ya vijijini vilikuwa vikisimamiwa na wakala wa usalama ambao walikuwa wanazima vipindi wakati wanasiasa wa upinzani wakiwa hewani.

Mikutano ya kampeni imesitishwa kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Wagombea watakuwa huru kutumia mitandao ya kijamii kufanya kampeni zao lakini si kila mtu anaweza kupata mitandao.

Haijajulikana iwapo rais Yoweri Museveni, atagombea nafasi ya urais kwa mara nyingine.

Uganda kuwagawanyia raia wake radio na televisheni

Baadhi ya wadadisi wanadhania mpango huo unasukumwa na mwongozo wa uchaguzi mkuu, ambao unatarajiwa mapema mwakani.
Maelezo ya picha, Baadhi ya wadadisi wanadhania mpango huo unasukumwa na mwongozo wa uchaguzi mkuu, ambao unatarajiwa mapema mwakani.

Serikali ya Uganda inapanga kutumia dola 100 milioni, kununua redio milioni 10 na televisheni 140 elfu, kugawanywa vijijini.

Baadhi ya wadadisi wanadhania mpango huo unasukumwa na mwongozo wa uchaguzi mkuu, ambao unatarajiwa mapema mwakani.

Lakini serikali inasema mpango huu wa redio na televisheni kugawiwa vijijini, ni sehemu ya hatua za kuwawezesha watoto nchini kote kuendelea na masomo yao, shule zikiwa bado zimefungwa ili kuzuia maambukizi ya Covid-19 tandavu.

Shule kufungwa, zaidi ya siku 80 zilizopita, ilikuwa kazi rahisi, wakiathirika jumla ya wanafunzi 15m, tangu vichekechea hadi wazamili vyuo vikuu.

Kuzifungua ni muhali, shauri ya kitisho bayana cha covid-19 tandavu.

Hivi sasa Uganda ina wagonjwa 705 wa Covid 19, kwa mujibu wa wizara ya afya - karibu 300 wamepona na bado hakuna kifo cha corona Uganda.

Hata hivyo licha kunasa wagonjwa wapya, kupitia upimaji, idadi ya wagonjwa inapanda kila kukicha.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni alieleza shule na vyuo vikuu kama nyasi kavu mbele ya moto wa corona. ''Suluhu ya masomo kwa sasa, ni teknolojia kupita kisomo cha mbali'' alisema.

Mwanamke akisiliza redio

Bw. Museveni aliongeza kuwa masomo ya mbali huenda yakawa bora zaidi, kwa sababu wasomaji wengi wanaweza kunufaika, kwa waalimu wachache bora zaidi, ambao wanaweza kuwafikia wanafunzi wengi kupitia redio na televisheni.

Kwa mujibu wa takwimu za sensa, mwaka 2014, nchini Uganda kulikuwa na televisheni milioni na redio milioni tatu unusu tu.

Idadi ya raia wa nchi hiyo sasa inazidi Waganda milioni 40, wakishi katika vijiji karibu elfu 70.

''Ikiwa tutakuwa na televisheni mbili kwa kila kijiji, hio ina maana televisheni 140 elfu, ambazo watoto wanaweza kuona na kujifunza masomo.

Halafu kuna suala la redio; redio ni rahisi zaidi, unaweza kuipa kila kaya redio yake inayotolewa na serikali. Kuna zaidi ya kaya au maskani milioni 7 nchini. Baadhi ya changamoto ni nishati au betri kuendeshea vyombo hivyo.

Lakini kuna nguvu za jua kwa televisheni, na redio za kutia ufunguo. Juu ya hayo serikali inataka redio na televisheni hizo zitengenezwe nchini humo, chini ya sera Nunua Uganda, Jenga Uganda - maarufu kama BUBU.

Watu wakitazama runinga

Inakisiwa, ili mpango huo kufanikishwa, itaigharimu hazina karibu $102m. Kama sehemu ya masomo ya mbali, Wizara ya elimu ya Uganda, imezindua vifaa vya masomo kwa wanafunzi milioni mbili unusu, hasa wa kidato cha sita.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Alex Kakooz, amesema kwa mara ya kwanza wanafunzi watapata tini zilizopangwa vizuri, kuwasaidia kwa masomo yao na kufikia kiwango kinachotakiwa.

Wanafuzi wa kidato cha sita, ni miongoni mwa wanafunzi 2.5m, watoto wa darasa la saba, kidato cha sita, wanaomaliza shada ya kwanza na uzamili vyuovikuu, ambao Rais Museveni, alighairi kuwaruhusu warejee masomoni, mapema mwezi huu, katika hotuba yake Juni Mosi, hadi mapema Julai.