China na India: Fahamu kwa nini kuna mgogoro wa kijeshi kati ya mataifa haya mawili yenye idadi kubwa ya watu duniani

Chanzo cha picha, AFP
India na China, mataifa mawili yenye idadi kubwa ya watu duniani , zikiwa na majeshi makubwa na silaha za kinyuklia zimekuwa zikikosoana kwa wiki kadhaa katika jimbo la Himalaya.
Lakini mgogoro huo ulifikia kilele chake siku ya Jumanne.
Jeshi la India linasema kwamba takriban wanajeshi 20 walifariki katika makabiliano na kwamba kulikuwa na majeruhi katika upande wa China. China haikuthibitisha walioathirika hadi siku ya Jumanne.
Hivi ndio vifo vya kwanza katika kipindi cha miongo minne ya migogoro kuhusu mpaka unaogawanya mataifa hayo mawili.
Lakini ni nini haswa kilichosababisha hali iliopo na inasukumwa na nini?
Vyombo vya habari vya India vimenukuu maafisa wakisema maelfu ya wanajeshi wa China wameingia kwa lazima eneo la bonde la Galwan huko Ladakh, katika eneo linalozozaniwa la Kashmir.
Ni wazi kwamba viongozi wa jeshi la India wanaopanga mikakati wameduwazwa na hali hiyo
Taarifa zinaonesha kwamba mapema Mei, vikosi vya China viliweka vyandarua na kuchimba mahandaki pamoja na kuweka vifaa vya kivita kilomita kadhaa ndani ya kile ambacho India inakichukulia kama eneo lake.
Hatua hiyo inawadia wakati India inajenga barabara kuu ya kilomita mia kadhaa ambayo inaunganisha kambi ya jeshi iliofunguliwa tena mwaka 2008.

Chanzo cha picha, PRESS INFORMATION BUREAU
"Hali ni tete. China imeingia eneo ambalo wao wenyewe wanakubali kwamba ni la India. Hili limebadili kabisa hali ilivyo," anasema Ajai Shukla, mtaalamu wa masuala ya kijeshi wa India ambaye alihudumu kama kanali jeshini.
China ina maoni tofauti. Inasema kwamba India ndiyo ambayo imebadilisha hali iliyokuwepo awali.
Vyombo vya habari vya India vinadai kwamba wanajeshi kutoka pande zote wamekuwa wakikabiliana katika matukio kama mawili eneo la Ladakh.
Pia makabiliano yameripotiwa katika maeneo karibia matatu: bonde la Galwan, chemichemi za maji moto na ziwa Pangong lililopo kusini.

Chanzo cha picha, AFP
Majeshi yao, ambayo ni miongoni mwa makubwa zaidi duniani, yanakutana ana kwa ana katika maeneo mengi ya eneo hilo.
Kwa sasa hivi eneo hilo la mpakani linatenganishwa kwa mstari tu. Kwa sababu ya mito, maziwa na vilele vyanzo vyenye barafu, mstari unaotenganisha wanajeshi wa nchi hizo mbili unaweza kubadilika na mara nyingi vikosi vimekuwa katika hatari ya kujikuta kwenye makabiliano.

Chanzo cha picha, Reuters
India na China zina mpaka wa zaidi ya kilomita 3,440 na zimekuwa na maeneo ambayo zote zimekuwa zikidai kuyamiliki.
Doria zao mipakani mara nyingi huwa zinaingiliana na matokeo yake ni makabiliano ya mara kwa mara lakini pande zote mbili zinasititiza kwamba hazijawahi kurushiana risasi katika kipindi cha miongo kadhaa.

Chanzo cha picha, AFP
Wasiwasi ambao umetanda kati ya majeshi ya nchi hizo mbili sio tu kwamba ni katika eneo la Ladakh pekee. Wanajeshi kutoka pande zote mbili pia wanakutana ana kwa ana katika mpaka wa China na kaskazini mashariki mwa India jimbo la Sikkim.
Awali mwezi huu ilisemekana kwamba walikabiliana katika mapigano.
Na kuna mzozo juu ya ramani mpya iliyotolewa huko Nepal, ambayo pia inashtumu India kwa kuingilia eneo lake kwa kujenga barabara kuu inayounganisha nchi hiyo na China.
Kwanini wasiwasi umeongezeka?
Kuna sababu kadhaa, lakini chanzo ni malengo ya kimkakati na pande zote mbili zinataka mwengine achukue jukumu.
"Mto wa Galwan kwa sasa hivi umekuwa angalizo kuu kwasababu uko karibu na barabara mpya iliyojengwa na India katika mto Shyok hadi kambi ya jeshi ya Daulat Beg, eneo la kijijini na lililo katika hatari kubwa ya kuathirika huko Ladakh, "anasema Shukla.

Umauzi wa India wa kuongeza miundo mbinu unaonekana kwamba ulikasirisha China.
Chombo cha habari vya China, Global Times: "Bonde la Galwan Valley ni eneo la China, mamlaka ya eneo inayodhibiti mpaka huo ilikuwa wazi kwa hilo."
"Kulingana na jeshi la China, India ndio ambayo imeingia kwenye eneo hilo kwa nguvu . Kwa hiyo India inabadilisha ile hali iliyokuwepo katika eneo hilo na hilo limekasirisha China" anasema dkt. Long Xingchun, rais wa Taasisi ya Chengdu ya Masuala ya Dunia (CIWA) ambayo ni jopo la ushauri.

Chanzo cha picha, AFP
Je hali inaweza kuwa mbaya kiasi gani?
"Mara nyingi majeshi ya pande zote mbili huwa yanashika doria katika eneo hilo. Na mara nyingi matukio kama hayo huwa yanatatuliwa katika kiwango cha jeshi la eneo.
Lakini safari hii, kumekuwa na wanajeshi wengi, " anasema aliyekuwa mwanadiplomasia Stobdam, mtaalamu eneo la Ladakh katika masuala ya China na India.

Chanzo cha picha, AFP
"Makabiliano yanatokea katika maeneo ambayo ni ya kimkakati ambayo ni muhimu kwa India.."
"Ikiwa watadhibiti ziwa Pangong, eneo la Ladakh haliwezi kulindwa. Ikiwa jeshi la China litaruhusiwa kukita kambi katika eneo la kimkakati la binde la Shyok, basi huenda hata bonde la Nubra na Siachen yakaathirika'', anasema.
Kulingana na taarifa za vyombo vya habari vya India, wanajeshi nchini humo walizidiwa na kuzingirwa pale China ilipojumuisha wanaume na mashine katika zoezi la kijeshi eneo hilo la mpakani.
Hatua hiyo ilizua wasiwasi huko Delhi, na India ina nafasi finyu ya kukabiliana na hali hiyo.
Inaweza kushawishi China kupitia majadiliano ya kuondoa wanajeshi wake au kujaribu kuwaondoa kwa lazima.
Kati ya machaguo hayo hakuna ambalo ni rahisi.
"China ni ya pili kwa wanajeshi wengi zaidi duniani. Kiteknolojia, inashinda India. Miundo mbinu yake kwa upande mwengine, imeendelea mno," anasema Ajai Shukla.
"Kifedha, China inaweza kugawanya raslimali zake kufikia malengo yake ya kijeshi huku uchumi wa India ukiwa umekuwa ukipitia shinikizo kubwa katika miaka ya hivi karibuni na janga la virusi vya corona limezorotesha kabisa hali hiyo," anaongeza.
Nguvu ya kimataifa dhidi ya nguvu ya kikanda
Uchumi wa China ni mara tano zaidi ya ule wa India na unashindana na ule wa Marekani..
India kwa upande mwengine, ikijiandaa kuwa mojawapo ya mataifa yenye uwezo mkubwa duniani ambapo inatumai kuwa na jukumu muhimu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wanasiasa wa India na wachambuzi mara nyengine huzungumza kana kwamba India na China zina uwezo sawa bila ya kukiri kwamba Beijing imepiga hatua kubwa .
Agosti iliopita , India iliamua kukamilisha umiliki wake wa maeneo ya Jammy na Kashmiri , na kuchora ramani mpya, uamuzi uliopingwa na Beijing.
Hatua hiyo ilisababisha kuundwa kwa jimbo jipya la Ladakh ambalo linashirikisha Aksai Chin, eneo linalodaiwa na India lakini linadhibitiwa na China . Hapo ndipo mgogoro ulipoanzia.
Umuhimu wa Pakistan na mzozo wa Tibet
India haiamini uhusiano wa miaka mingi wa China na Pakistan, ikilaumu China kwa kuisaidia Pakistan kujihami na silaha za kinyuklia na teknolojia mpya ya makombora.
Viongozi wakongwe wa chama tawala cha Hindu nationalist Government BJP pia wamekuwa wakizungumzia kuhusu kulidai eneo la Kashmir linalomilikiwa na Pakistan.
Barabara kuu ya karakoram, inapitia eneo hilo ambalo linaunganisha China na Pakistan.
Beijing imewekeza US $ 60 billion katika miundo mbinu ya Pakistan kama mojawapo ya mradi wa kiuchumi wa China na Pakistan, ambao ni pamoja na mpango wa ujenzi wa barabara mpya ya Silk Road inayokuzwa na serikali ya China.
Barabara hiyo kuu ni muhimu katika usafirishaji wa bidhaa kuingia na kutoka katika bandari ya kusini ya Gwadar nchini Pakistan., Bandari hiyo inaipatia China fursa ya kuingia katika bahari ya Arabuni.
India inahofia hivi karibuni kwamba bandari ya Gwadar huenda ikatumika kusaidia operesheni za wanamaji wa China baharini.
Tibet ni eneo jingine linalozozaniwa.
China ina wasiwasi kuhusu uhusiano kati ya serikali ya India na Dalai Lama, kiongozi wa kidini wa Tibet aliyetorokea nchini India baada ya kufeli mapinduzi maarufu ya 1959 huko Tibet.
India imekataa kutambua serikali ya Tibet iliopo mafichoni . lakini kiongozi wake mkuu ni miongoni mwa orodha ya wageni wakati wa kuapishwa kwa waziri mkuu Modi mwaka 2014.

Uhusiano mbaya uliopo kati ya mataifa hayo mawili umeifanya China kuona kana kwamba India ndio nchi inayoweza kushirikiana na wapinzani wake wakuu kama vile Marekani Japan na Australia.
New Delhi hivi majuzi ilibadili sheria kuzuia kampuni za China kuuza kampuni za India kutokana na hasara zilizosababishwa na mlipuko wa corona , kitu ambacho Beijing inapinga.
Licha ya hayo yote, China inasalia kuwa mshirika wa pili wa kibiashara wa India .

Chanzo cha picha, Getty Images
Mazungumzo
Katika siku za hivi karibuni, doria za mipakani katika mataifa yote mawili zimekumbwa na migogoro zaidi ya mara mia moja kila mwaka.
Mwaka 2013 na 2017, hii ilisababisha mgogoro ambao ulitatuliwa baada ya wiki kadhaa za mazungumzo ya kidiplomasia na kisiasa.
Kufuatia tukio kubwa la mwaka 2017, Modi na rais wa Xi Jinping walifanya vikao viwili visivyo rasmi ili kuzungumzia tofauti yao
India na China kwa mara nyengine zimeanza mazungumzo ya kutatua mzozo huo. Maafisa wakongwe wa jeshi walikutana juni sita na tena siku ya Jumanne, baada ya tukio hilo lililorekodiwa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mzozo wa hivi karibuni ulifanyika wakati wa doria katika eneo la Galwan 14 , karibu na eneo ambalo waathiriwa walipatikana.
Bila shaka , mzozo huu utaongeza kutoaminiana kati ya mataifa hayo mawili hatua ambayo itahitaji muingiliano wa kisiasa katika ngazi za juu kuzuia hali kutodhibitika.












