Ukatili baharini: Simulizi kuhusu wavuvi waliotoswa kwenye maji na Wachina

Video inayoonesha mwili wa kijana mmoja akitoswa kikatili baharini imesababisha kufanyika kwa uchunguzi kimataifa.
Tukio hilo limeonesha kuwepo kwa viashiria vya hali ''kama ya utumwa'' inayodaiwa kuwepo kwa wavuvi wa Indonesia kuteswa na wamiliki wenye asili ya China. Simulizi hii ya familia mbili , wakiomboleza kupoteza vijana wao na kaka zao ambao walikufa wakijaribu kujenga maisha mapya.
Sepri hakuwahi kufanya kazi za majini kabla, aliposikia kuwa rafiki yake alipata fursa ya kufanya kazi katika boti inayomilikiwa na raia wa China.
Walimuahidi kumlipa pesa nyingi kijana huyo wa miaka 25, fedha ambazo alikuwa hawezi kuota kuzipata akiwa katika kijiji chake hapa Sumatra- katika kisiwa cha Indonesia.
"Alifurahia sana kuhusu suala la kupata fedha hizo nyingi kwa ajili yetu," dada yake Rika Andri Pratama anakumbuka.
Kwa kuahidiwa kupata mafunzo na kupata mshahara wa kiasi cha dola $400 (£326) kwa mwezi, aliweza kupata kundi la vijana 22 wa Indonesia katika boti hiyo ya Long Xing 629 mwaka jana mwezi Februari.
"Kabla hajaondoka, aliniazima kiasi kidogo cha fedha," alisema Rika.
"Alisema itakuwa ni mara ya mwisho yeye kuniazima fedha maana anaenda na atarudi nyumbani na fedha nyingi sana kwa ajili ya kufanyia matengenezo nyumba yao."
Lakini Sepri hakuwahi kurudi nyumbani. Hakuna fedha ambazo ziliwahi kutumwa na yeye tangu aondoke. Na Rika hajawahi kuongea na kaka yake tena.

Mapema mwezi Januari, alipokea barua. Alikuwa amekufa majini, mwili wake ulitupwa katika bahari ya Pasifiki.
"Moyo wangu uliuma sana niliposikia kuwa alitupwa baharini," alisema alizuia machozi yake kwanza.
Alikuwa anajihisi kuwa na hatia. "Kabla ya mama yetu kufariki, maneno yake ya mwisho yalikuwa nimtunze vizuri mdogo wangu'."
Vijana wengine wawili katika kundi la Waindonesia walikufa katika boti hiyo ya Long Xing 629. Sepri na mwanaume mwingine walikufa kwa kupishana siku chache mwezi Desemba,baada ya miezi 10 katika bahari. Wakati Ari, ambaye alikuwa ametoka katika kijiji kimoja na Sepri,alifariki mwezi Machi mwaka huu, muda mfupi kabla ya kikosi chote cha vijana wa Indonesia kuokolewa.
Kama Sepri, miili yao ilikuwa imefungwa katika nguo na kutupwa.
Hawakuweza kupata nafasi ya kuaga miili ya wapendwa wao kama vile familia ya Sepri ilivyoshindwa.
Mtu wa tatu ni mwanaume aliyekutwa amekata tamaa na anaugua sana, Efendi Pasaribu, hakudhaniwa kama angeweza kupona wakati aliporushwa - lakini alipona.
Kuna dalili kuwa matukio yote haya yangepita bila kugundulika -kama si vifo kadhaa zaidi baharini - visingepigwa chukuliwa picha kwa simu na kufumbua macho raia wa Indonesia kuhusu majanga yanayoendelea.

Badala yake,picha hiyo ya video imeibua mjadala kuhusu kunyanyaswa kwa wavuvi katika vyombo vya majini kutoka mataifa ya kigeni hasa Asia.
Cha kushangaza taarifa kuhusu boti hiyo ya Long Xing 629 ilikuja baada ya miaka mitano baada ya wavuvi wageni wapatao 4,000 hasa kutoka Myanmar , walipookolewa kutoka visiwa vya mbali vya Indonesia;
Na baadhi walikuwa wamehusishwa katika utumwa kwa miaka mingi.
Wakati Indonesia ilipojizatiti kukomesha unyanyasaji huu kwa wavuvi katika vyombo vya baharini vya wageni, watu waliookolewa katika boti ya Long Xing 629' walianza kuongea na ikawa wazi kuwa mabadiliko ni kidogo ndio yalifanyika.
'Kitu pekee tulichokuwa tunafanya ni kuwaonya na kusali'
Kwanza wenzetu wachache, ambao hawakutaka kufahamika majina yao bali walitumia vifupisho tu vya majina yao, walikuwa wanapigwa mara nyingi na kufukuzwa.
Hawakuwa wanaelewa ni nini ambacho mmiliki wao wa kichina alikuwa anasema na ilikuwa inawafanya wachanganyikiwe kwa kutoelewana.
Mmoja wa wavuvi hao aliiambia BBC Indonesia kuwa miili ya rafiki zake ilikuwa inatundikwa juu kabla ya kufariki.
Mwingine alisema, walikuwa wanalazimishwa kufanya kazi saa 18-kwa siku na walikwa wanapewa tu mkia wa samaki kula.
Wao [wa Wachina] walikunywa maji ya chupa, wakati sisi tulipewa maji ya bahari tu," NA mwenye umri wa miaka 20 alisema.
Ilipobainika ni wazi jinsi Sepri na wengine walivyokuwa wagonjwa, NA anasema walimsihi mkuu huyo awapeleke nchi kavu kwa matibabu.
Baada ya watu hao watatu kufariki, waliomba kuweka miili hiyo kwenye baridi ili marafiki zao waweze kuzikwa kulingana na tamaduni zao za Kiislamu mara tu watakapofika ufukweni.
Lakini mkuu huyo aliwaambia kwamba hakuna mtu atakaye wahitaji.
"Alisema kwamba kila nchi itakataa miili yao," NA anasema. "tulichoweza kufanya ilikuwa nikuosha miili yao kulingana na sheria ya Kiislamu, kusali na kisha kuwatupa baharini."
Hatimaye nahodha huyo alikubali kuhamisha watu waliobaki wa Kiindonesia kwenye chombo kingine cha Wachina ambacho kilifika Busan, Korea Kusini. Efendi Pasaribu alikuwa mgonjwa sana, lakini alikuwa hai.
Kwa maisha bora ya baadaye
Mama yake, Kelentina Silaban, aliweza kupiga simu kwa mtoto wake wakati amelala kitandani hospitalini huko Busan.
Efendi alikuwa karibu kutambulika kutoka kwa mtu mzima mwenye umri wa miaka 21 ambaye alikuwa amemuaga zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

alikuwa mwenye nguvu na afya wakati alipoenda baharini,
"Nilisema tafadhali, tafadhali njoo nyumbani tu, tutakuhudumia huku kijijini."
Badala yake, mwili wa mtoto wake ulirudishwa kwake. Waliambiwa alikuwa amekufa kutokana na matatizo ya figo na homa ya mapafu.
Kabla ya kuondoka katika kijiji chake alikuwa ameweka picha yake kwenye mitandao ya kijamii, akiwa ameshikilia sanduku lake la nguo akiandika "Ninaondoka ili nikatafute maisha bora ya baadae."
Efendi aliishia kuzikwa katika makaburi ya karibu na nyumba katika kijiji cha Sumatra.
"Tunatumani kuwa kifo cha ndugu yetu kitasaidia kufunua utumwa kwenye meli za uvuvi za kigeni. Tunatumani kuwa hii itachunguzwa kikamilifu," ndugu yake Rohman alisema
Majibu - sio pesa
Vikundi vya haki za wahamiaji vinaitaka serikali kufanya uchunguzi zaidi kulinda raia wao kutokana na kuwa "watumwa".
Serikali ya Indonesia inasema waokoaji wa Long Xing 269 - hakuna yeyote kati yao aliyepokea mishahara yao yote - walikuwa sehemu ya kikundi cha wavuvi 49, kati ya 19 hadi 24, ambao walilazimishwa kufanya kazi katika mazingira magumu kwenye boti za uvuvi nne zinazomilikiwa na kampuni moja ya Wachina, Dalian Ocean Co Ltd.

Ilikataa kujibu madai hayo walipo wasiliana na BBC, ikisema itatoa taarifa kwenye wavuti yake. Hakuna jibu lililotolewa.
Nchi zote mbili zinaahidi majibu ya familia. Jakarta ilivyoelezwa matibabu ya mabaharia 'ni ya "kinyama", wakati ubalozi wa China katika Jakarta ulieleza kuwa ni "tukio la bahati mbaya".
Imesema kuwa sasa wanafanya "uchunguzi wakina" kwa kushirikiana na Indonesia.
Katika Indonesia, watu watatu wametiwa mbaroni kama sehemu ya uchunguzi wa makampuni ya kuajiri vijana. Wanaweza kukabiliwa na kifungo cha miaka 15 gerezani ikiwa watapatikana na hatia chini ya sheria za usafirishaji binadamu.
"Tutahakikisha kwamba Kampuni itatimiza haki za Wafanyakazi wetu," Waziri Retno Marsudi alisema katika mkutano wa video.
"Kulingana na habari kutoka kwa wafanyikazi, kampuni hiyo imekiuka haki za binadamu," ameongeza.
Chama cha wafanyakazi wavuvi Indonesia (IFMA) waliimbia BBC Indonesia kwamba kuna mawakala wengi wanao kodisha wavuvi hawajasajiliwa kutoka serikalini.
"Kuna maombi mengi kutoka kwa vyombo vya kigeni, mashirika haya huonyesa hati zinazohitajika na kupeleka watukuchukuliwa. Hakuna udanganyifu kutoka upande wa Indonesia," makamu wa rais wa kikundi hicho Tikno

Chanzo cha picha, Getty Images
" kutokana na shinikizo la umma, serikali inasema sasa wanazingatia kuweka sitisho la miezi sita kwa wavuvi wa Indonesia wanaenda kufanya kazi kwenye vyombo vya nje.
"Hii itatusaidia sisi tuwe na wakati wakutosha kuboresha usimamizi wetu, kwa hivyo tunaweza kuweka mfumo wa kituo kimoja ambapo tunayo data yote tunayohitaji kuweza kufuatilia na kuhakikisha haki za wavuvi wetu zinalindwa," afisa wa wizara ya Zulficar Mochtar alisema.
Wakati huo huo, kampuni ya kuajiri ambayo ilimuajiri kaka wa Rika, Sepri, imeahidi kumlipa fidia ya rupia milioni 250 (pauni 13,000).Lakini yeye anataka majibu, sio pesa tu.
"Tunahitaji kujua nini kilitokea kwenye chombo hicho," alisema. "Wacha tuwe familia ya mwisho ambayo inapaswa kupata uzoefu huu.












