Kylie Jenner: Forbes yamuondoa kwenye orodha ya mabilionea

Chanzo cha picha, Getty Images
Jarida la Forbes limemuondoa nyota wa kipindi cha TV na mfanyabiashara Kylie Jenner katika orodha ya mabilionea na kushutumu familia yake kupandisha thamani ya biashara yake ya vipodozi.
Jarida la Forbes limesema kuwa familia yake ilienda mbali zaidi kwa kumuwakilisha kuwa ni tajiri mdogo zikiwa ni tofauti na uhalisia wenyewe.
Katika ujumbe wake wa Twitter, Jenner alikanusha makala hiyo kuwa haikuwa imetoa taarifa sahihi na kudai kuwa hayo ni mawazo yasiyo na udhibitisho wowote.
"Sijawahi kutaka wadhifa wowote au kudanganya kufika nilipo kwa namna yeyote," aliandika.
"Ninaweza kuweka orodha ya vitu 100 muhimu kwa sasa tofauti na kudanganya kuhusu utajiri nilio nao," aliongeza.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe

Hatua hiyo imefanya jarida la Forbes kurudi nyuma kwa kile ilichoandika kuhusiana Jenner mwaka 2019, wakati ambao alijitangaza mwenyewe kuwa ni bilionea.
Maelezo yake yanazua sintofahamu, watu wakikosoa maelezo yake ya zamani ambayo alisema mwenyewe na yaliyotajwa na familia yake ya Kardashian kipindi cha Televisheni.
Jarida la Forbes, ambalo linajulikana duniani kwa kutaja orodha ya mabilionea liliandika kuwa Jenner amefanikiwa kwa kuwa na kampuni ya vipodozi ambayo aliianzisha mwaka 2015 na kujumuisha na vipodozi vya Kylie.
Mwaka jana Jenner alitangaza kuwa anauza asilimia 51 ya hisa za kampuni yake kubwa ya Coty kwa dola milioni 600.
Forbes ilisema mhasibu wa familia alitoa ushuru na kuenekana kwamba kampuni hiyo ilikuwa imetengeneza mauzo ya zaidi ya dola milioni $300 mwaka 2016 na kudaiwa kuwa mauzo ya mwaka uliofuata yalikuwa dola milioni 330.
Lakini taarifa kutoka kwa kampuni ya Coty, ambazo zinaenea sana zinaonesha kuwa kampuni ya Jenner ni ndogo na iso na mafanikio makubwa tofauti na ambacho kimekuwa kikisemwa na familia yake kwenye vyombo vya habari iikiwemo jarida la Forbes, kile ambacho inataka wao waamini", jarida la Forbes limesema.
Taarifa za kampuni ya Coty kwa wawekezaji kuhusu biashara ilionesha kwamba kampuni hiyo ilikuwa na mauzo ya dola milioni 125 pekee kwa 2018.
"Kama vipodozi vya Kylie vilikuwa na mauzo ya dola milioni 125 mwaka 2018, inawezekanaje kwamba ilikuwa na mauzo ya dola milioni 307 kwa mwaka 2016 au dola milioni 330 mwaka 2017?" Forbes ilihoji katika makala hiyo.
Pamoja na kwamba jarida hilo limeshusha thamani yake kwa kipimo cha utajiri duniani chake, Jenner imemuuna moyo sana na kwa sasa hivi utajiri wake uko chini ya dola milioni 900".
Waandishi wa Forbes awali waliwahi kuwashutumu mabilionea wengine kwa kudanganya utajiri walionao akiwemo rais wa Marekani Donald Trump na mfanyabiashara maarufu Wilbur Ross.












