Virusi vya Corona: Makosa yanayofanywa na watu wanaovaa barakoa za vitambaa

Chanzo cha picha, Reuters
Katika vita dhidi ya virusi vya corona , kuna suala ambalo linazidi kuibua mjadala kuhusu iwapo raia wanapaswa kujifunika uso na pua kwa kutumia barakoa?
Shirika la Afya Duniani WHO limesisitiza siku ya Jumatatu kwamba kunapaswa kuwa na ushahidi kwamba utumizi wa mask au barakoa, pamoja na maelezo mengine unasaidia kupunguza mlipuko huo. Hakuna jibu la moja kwa moja , wala kiini macho.
'Mask' pekee haziwezi kuzuia mlipuko huo , alisema mkurugenzi wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus , akitoa wito kwa maelezo mengine kama vile yale ya kuosha mikono kuendelea kutekelezwa.
Kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa nchini Marekani CDC kilisema kwamba kulingana na utafiti wa hivi karibuni , walipendekeza kujilinda uso katika maeneo ambayo watu wanakaribiana zaidi .
CDC inapendekeza matumizi ya barakoa za vitambaa kujilinda uso katika maeneo ya umma ambapo maagizo mengine ya kutokaribiana ni vigumu kutekeleza, ilisema taasisi.

Katika maeneo ya umma kama vile kwenye maduka ya jumla , ama yale ya kuuza dawa inaweza kua vigumu kutekeleza agizo la kutokaribiana hivyobasi kuna hatari ya maambukizi miongoni mwa watu.
Hatahivyo kupitia mask ama barakoa zilizotengenezwa nyumbani ama hata kupitia barakoa zilizothibitishwa na maafisa wa afya , kuna maelezo ambayo iwapo yatapuuzwa yanadhoofisha utumiaji wa vifaa hivyo.
Kununua mask wakati huu sio rahisi kwa kuwa mahitaji yake yapo juu sana.
Hatahivyo lazima uangalie makosa yanayofanyika sana wakati wa matumizi yake kulingana na CDC na WHO.
Dhana ya kuwa barakoa ni kinga ya kiwango cha juu
Mojawapo ya onyo kutoka mamlaka za Afya sio kudhania kwamba barakoa iliotengenezwa kwa kitambaa ina uwezo wa kukulinda kama ile ya N95 katika matumizi ya kimatibabu.
Kimatibabu N 95 ni vifaa vinavyohitaji kutumiwa na maafisa wa Afya, hivyobasi hazifai kutumiwa na raia wa kawaida ili kuzuia uhaba.
Barakoa zilizotengezwa na vitambaa kulingana na CDC hupunguza kasi ya virusi vya corona na husaidia watu ambao huenda wameambukizwa kutowaambukiza wengine.

Chanzo cha picha, Reuters
Kwa upande mwengine, barakoa za N95 ambazo zimeidhinishwakimatibabu ni vifaa vinavyohitajika kutumiwa na maafisa wa Afya, hivyobasi hazifai kutumiwa na raia wa kawaida ili kuzuia uhaba wake.
Kutoosha mikono na kukaribiana na watu wengine
WHO na CDC zinakubaliana kwamba matumizi ya kinga hii ni mojawapo ya maelezo ambayo kila mmoja anapaswa kufuata ili kuzuia maambukizi.
Kutokaribiana, kuzuia mikutano ya zaidi ya watu 10 pamoja na kuosha mikono kwa mara kwa mara kunasalia kuwa nguzo ya CDC katika kinga ya kibinafsi hata iwapo mtu amaevalia barakoa.

Kufunika mdomo pekee
Kosa jingine linalofanywa na watu wengi wakati wa utumizi wa barakoa ni kufikiria kwamba wanaweza kuziba mdomo pekee.
Maeneo yoyote yanayotumika kupumua mwilini yanafaa kufinikwa , hivyobasi barakoa zilizotengenezwa na vitambaa zinafaa kuziba mdomo na pua kwa kuwa ndizo zinazotumika kwa maambukizi.
Vilevile barakoa hizo hazifai kuwekwa karibu na watoto chini ya umri wa miaka 2 ama watu wenye matatizo ya kupumua ama watu ambao hawawezi kuzivua bila usaidizi, imeonya CDC.
Kutoosha barakoa zilizotengenezwa na vitambaa baada ya matumizi.
Barakoa zilizotengenezwa nyumbani kwa kutumia vitambaa zinaweza kutumika kwa mara nyengine iwapo maelezo ya usafi wake yatatimizwa.
Kutoziosha baada ya matumizi kunaweza kusababisha maambukizi. CDC inasema kwamba kuziosha na kuzikausha inatosha.
Barakoa zilizoidhinishwa kimatibabu hazifai kutumika mara ya pili.
Kushika barakoa bila kuosha mikono
Kwa kuwa barakoa huwa na vimelea wakati zinapotumika , ni muhimu kutozishika na iwapo hilo litafanyika ni muhimu kuosha mikono.
Vievile kabla ya kuvaa na kuvua pia unapaswa kuosha mikono yako.
Wakati ambapo haitumiki barakoa iliotenegenzwa kwa kutumia kitambaa inafaa kuwekwa mahala pasafi, ndani ya mfuko uliofungwa.

Chanzo cha picha, EPA













