Watoto wenye miaka mitatu na minne wabakwa Somalia

Shadow

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Ripoti za ubakaji nchini Somali zinaongezeka kwa kasi siku za karibuni

Serikali ya Somalia imekemea tukio baya la ubakaji wa watoto wawili wa kike, mmoja ana umri wa miaka mitatu na mwingine ana miaka minne.

Daktari anayewahudumia sasa hospitalini anasema watoto hao wanahitaji kufanyiwa upasuaji mkubwa.

Maafisa wanasema kuwa wamewakamata watu kadhaa kufutia tukio hilo lililotokea siku ya Jumatano

Wazazi wanasema kuwa binamu hao wawili walikuwa walikuwa wakitokea shule ya jirani na nyumbani kwao, mjini Mogadishu.

Walifanyiwa unyama huo na wanaume waliowateka na kuwafanyia unyanyasaji wa kingono.

Wazazi wa watoto hao waliwatafuta watoto hao katika maeneo ya jirani bila mafanikio mpaka siku iliyofuata waliwapata watoto hao wakiwa wenyewe tu.

Mhariri wa BBC Africa Will Ross , anasema kuwa ripoti za ubakaji zinazoshangaza zimekuwa zikiongezeka nchini Somalia katika miaka ya hivi karibuni.

Na kuna uhitaji wa kuandika zaidi matukio hayo ili kuleta mabadiliko.