Maadhimisho ya kuachiliwa kwa Nelson Mandela: Kwanini alikuwa mtu muhimu ?

Nelson Mandela

Chanzo cha picha, Getty Images

Leo ni siku ya kumbukumbu ya miaka 30 tangu hayati Nelson Mandela alipoachiwa kutoka gerezani wakati wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika kusini. Ni siku inayotumika kumuenzi na kutambua mafanikio yake.

Mandela, aliyefariki mnamo 2013 akiwa na umri wa miaka 95, alikuwa kiongozi wa kwanza mweusi nchini Afrika kusini baada ya kutumikia kifungo cha miaka 27 gerezani, na anakumbukwa kuwa mmoja wa viongozi bora aliyewahi kushuhudiwa duniani.

Umoja wa mataifa unasema: "Kila mtu ana uwezo na jukumu la kuibadili dunia kuwa bora. Siku ya Mandela ni fursa kwa kila mtu kuchukua hatua na kuhimiza mabadiliko."

Kwanini Nelson Mandela alikuwa mtu muhimu?

Wakati Nelson Mandela alipokuwa kijana, watu weupe na watu weusi walikuwa hawaishi pamoja chini ya mfumo wa ubaguzi wa rangi uliojulikana kama apartheid.

Watu weupe, ambao walikuwa ni idadi ndogo ya raia, ndio walioidhibiti nchi.

Ilikuwa ni marufuku kwa watu weusi kwenda shule, hospitali na hata maeneo ya kubarizi kama katika fukwe za bahari sawa na watu weupe. Hali ilikuwa imeimarika zaidi katika shule na hospitali za watu weupe.

Mandela

Chanzo cha picha, Getty Images

Watu weusi pia walinyimwa haki msingi, kama vile kushiriki katika uchaguzi mkuu.

Lakini Nelson Mandela aliamini kwamba kila mtu anastahili kuchukuliwa kwa usawa.

Mandela alijiunga na chama cha kisiasa kilichojulikana kama African National Congress (ANC) na baadaye kuidhinisha tawi la vijana la chama hicho, aliongoza maandamano kupinga utawala wa ubaguzi wa rangi.

Mandela anakwenda gerezani

Robben Island

Mara nyingine kunazuka ghasia katika maandamano na mnamo 1964, Mandela alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani katika kisiwa cha Robben.

Wakati Mandela akiwa gerezani, picha zake zilipigwa marufuku na ilikuwa ni kinyume cha sheria kumnukuu hadharani.

Lakini watu kote duniani walifanya kampeni kutaka aachiliwe.

Nyimbo ziliimbwa na matamasha makubwa yaliandaliwa katika kulalamikia kufungwa kwake.

Mandela aachiwa huru

MANDELA

Chanzo cha picha, AFP/GETTY IMAGES

Hatimaye mnamo 1990, rais wa Afrika kusini FW de Klerk - mtu mweupe - alimuachia huru.

Mandela alitumikia miaka 27 gerezani na alipokewa kama shujaa baada ya kuachiwa huru.

Ana umaarufu kwa kuhimiza msamaha na usawa.

Utawala wa ubaguzi wa rangi ulifutiliwa mbali mnamo 1991, na miaka mitatu baadaye, Afrika kusini iliandaa uchaguzi wa kwanza mkuu ambapo watu weusi waliruhusiwa kupiga kura kam watu weupe.

Urais na Amani

Nelson Mandela alichaguliwa rais na akaanza kuleta umoja baina ya watu wa rangi tofuati.

Mnamo 1993, alipewa tuzo ya Nobel ya amani - ya kiwango cha juu ya aina yake - kwa jitihada zake.

Mnamo 1995, Afrika kusini iliandaa mashindano yake ya kwanza ya michezo - kombe la dunia la mchezo wa raga.

Mandela aliiunga mkono timu ya Afrika kusini, iliyojumuisha zaidi wazungu, jambo lililosaidia kuiunganisha nchi hiyo zaidi.

The Queen and Nelson Mandela met several times

Chanzo cha picha, WIREFOTO

Maelezo ya picha, Malkia Elizabeth alikutana na Nelson Mandela mara kadhaa

Alikuwa mojawapo ya viongozi maarufu duniani, huku wanasiasa na nyota wakifunga msururu kupata fursa ya kupigwa picha naye.

Licha ya kwamba Nelson Mandela aliisaidia Afrika kusini kuwa katika nafasi ilio na angalau, taifa hilo bado lina matatizo hii leo, yakiwemo umaskini, na uhalifu .

Lakini anakumbukwa kote duniani kwa ujumbe wake wa amani na umoja.