Fursa ya kulala seli ya Nelson Mandela yashutumiwa Afrika Kusini

Utalipa dola 250,00 kulala gereza alimofungwa Mandela?

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mandela alifungwa Kisiwa cha Robben kwa miaka 18

Makumbusho ya Kisiwa cha Robben nchini Afrika Kusini imeshutumu vikali shirika ambalo lilikuwa linafanya mnada wa kununua nafasi ya kulala seli alimofungwa Nelson Mandela.

Kiongozi huyo wa zamani wa Afrika Kusini alikaa katika gereza hilo kwa miaka 18.

Shirika la hisani la CEO Sleepout ambalo huchangisha pesa za kuwasaidia watu wasio na makao lilikuwa limeanzisha mnada mtandaoni ambapo yule ambaye angelipa peza Zaidi angepata fursa ya kulala usiku mmoja katika chumba hicho.

Shirika hilo tayari limeahirisha mnada huo.

Kituo cha habari cha EWN News kinaripoti kuwa afisa wa makumbusho hayo Morongoa Ramaboa anasema ingawa CEO Sleepout walikuwa wamewasiliana nao kuhusu mpango huo, hakukuwa na makubaliano yoyote.

Aidha, anasema hakukuwa na maafikiano ya iwapo chumba halisi alimofungwa Mandela ndicho kingetumiwa.

"Tunashutumu sana mpango huo wa kutoa fursa kwa atakayetoa pesa nyingi zaidi kulala katika seli ya Nelson Mandela kisiwani humo. Tunasikitika kwamba historia ya maisha ya Nelson Mandela inatumiwa vibaya hivi kwa manufaa yakifedha," anasema.

Waliokuwa wanataka kulipia fursa hiyo sasa wanapewa fursa ya kulala katika shamba la Liliesleaf ambalo lilimilikiwa na rais huyo wa zamani aliyepigana dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Ukurasa uliokuwa na mnada huo mtandaoni sasa unawalekeza watu kwa shamba hilo la Liliesleaf.

Kiasi cha chini kwenye mnada huo sasa ni $11,000 (£8,300), na shirika hilo linasema shamba hilo linaweza kuwahudumia watu hadi 400.

Kisiwa cha Robben sasa ni kituo cha kitalii
Maelezo ya picha, Kisiwa cha Robben sasa ni kituo cha kitalii

Operesheni ya maafisa wa utawala wa ubaguzi wa rangi iliyofanywa kwenye shamba hilo lililotumiwa kama maficho na wanachama wa ANC ilipelekea Kesi za Rivonia ambapo baada yake Mandela na wanaharakati wengine waliokuwa wakipambana na ubaguzi wa rangi walifungwa jela.

Shamba hilo lilifunguliwa kwa umma mwaka 2013 kama makumbusho.

Maisha ya Nelson Mandela miaka 27 gerezani

"Nilienda likizo ndefu ya miaka 27," Nelson Mandela wakati mmoja alisema kuhusu miaka yake gerezani.

Maneno kwanza ya mlinzi wa gereza wakati Nelson Mandela na wenzake wa ANC walifika yalikuwa ni: "Hiki ni kisiwa, Hapa ndipo mtafia."

Walipitia maisha mabaya kwenye gereza hilo jipya lililojengwa kuwazuia wafungwa wa kisissa. Kila mmoja alikuwa na chumba chake ya futi saba mraba na kilizungukwa na ua uliojengwa waka saruji. Kwanza hakuruhusiwa kusoma chochote.

Maisha katika kisiwa cha Robben yalikuwa magumu
Maelezo ya picha, Maisha katika kisiwa cha Robben yalikuwa magumu

Walivunja mawe kwa nyundo kutengeneza kokoto na walilazimishwa kufanya kazi kwa timbo lililokuwa na mwangaza mkali.

Mfungwa mwenzake Walter Sisulu alingumza kuhunu kuibuka kwa uongozi wa Mandela miongoni mwa wafungwa kauanzia uasi kwenye matimbo.

Mfungwa nambari 46664 jinsi alivyofahamika - mfungwa wa 466 kuwasili mwaka 1964 - akawa wa kwanza kuasi kupinga kutendewa vibaya na mara nyingine alitenganishwa na wafungwa wengine kama adhabu.

Wakati wa miaka ya kwanza kwanza, kutengwa ilikuwa kawaida. Tulihukuiwa kwa makosa madogo na kutengwa, aliandika kwenye kitabu chake, The Long Walk to Freedom. Mamlaka ziliamini kuwa kutengwa ilikuwa jibu kwa uasi wetu.

Chuo ndani ya gereza

Baada ya miezi michache ya kwanza kwenye kisiwa cha Roben, maisha yalirudi kuwa ya mpangilio.

"Maisha ya gerezani na mpangilio: kila siku ni sawa na iliyopita, kila wiki ni sawa na iliyotangulia na hivyo miezi na miaka huingiliana, Mandela aliandika.

Muda ulivyopita na kulingana ni alikuwa akisimamia gereza, mambo kadhaa yaliruhusiwa. Wale waliotaka walituma maombi ya kusoma.

Lakini masomo mengine kama ya siasa na historia ya jeshi vilikuwa haramu. Robben Island ikaja kufahamika kama "chuo ndani ya gereza."

Wakati Mandela alizungunzia maisha yake huko Robben baada ya kurudi huko mwaka 1994 alisema: "Vidonda ambavyo havionekani, ni vichungu sana kuliko vile vinavyoweza kuonekana na kutibiwa na daktari. Moja ya nyakati zenye husuni zaidi wakati wa miaka yangu gerezani ulikuwa wakati wa kifo cha mama yangu. Wakati mwingine ni wakati wa kifo cha mtota wangu wa kwanza wa kiume aliyefariki kwenye ajali ya barabarani." hakuruhusiwa kuhudhuria mazishi yote hayo.