Jinsi watu wanavyosheherekea mwaka mpya maeneo mbalimbali duniani?

Watu huwa wanasheherekea mwaka mpya kwa namna mbalimbali.

Usiku wa tarehe 31 Desemba, shamra shamra huwa nyingi katika maeneo mbalimbali duniani na kwa wakati tofauti kwa kuwa saa huwa zinatofautiana kutoka nchi moja mpaka nyingine.

Wengi wetu huwa tunatumia muda wa mwisho wa mwaka kuwa karibu na marafiki, familia na ibada pia! Lakini kuna namna nyingine ambayo watu huwa wanatumia kusheherekea mwaka mpya?

Mara zote, mwaka mpya huwa unatazamwa kuwa siku njema zaidi katika mwaka.

Wakati ambao unampa mtu fursa ya kutafakari yale ambayo alifanikiwa mwaka uliopita na nini anapaswa kuanza kukifanya kwa mwaka mpya.

Wakati wa kuwa na matumaini mapya na mwanzo mpya katika maisha.

Huwa ni muda muafaka wa kujirekebisha ulipokosea kwa mwaka uliopita na kuanza hatua mpya.

Ni muda wa shukrani kwa kuwa hai na kuwa na mafanikio fulani, ndio maana watu wengi wanasheherekea wanapovuka mwaka.

Mwaka mpya huwa ni utamaduni uliobuniwa kwa kuangalia mazuri ambayo yanaweza kutokea katika siku zijazo katika mwaka.

Aina mbalimbali ambazo watu hutadhimisha sherehe ya mwaka mpya

1.Fataki nyingi huwa zinarushwa angani

Mtindo ambao watu wengi huwa wanapenda kusheherekea ni kupika fataki ifikapo saa sita usiku.

2. Wengine huvunja sahani

Maeneo mengine huwa wanavunja sahani nyingi siku ya mwaka mpya ikiwa ni ishara ya kukaribisha mwaka.

Watu wa Denmark huvunja sahani kama ishara ya jambo la kheri kwa mwaka mpya.

Hivyo mtu anaweza kwenda kuvunja sahani katika mlango wa rafiki au jirani ili kumtakia kheri kwa miezi 12 katika mwaka.

3. Kudondosha vitu

New York Marekani, watu wengi hukutana makutano ya Times Square ili kusubiri saa sita ifike.

Lakini huwa wanasubiri kitu kidondoke kutoka juu mfano; mpira udondoke kutoka juu na kuwa ishara kuwa mwaka mpya umefika.

Huko Vincennes ,Indiana, watu huwa wanasubiri matikiti maji yadondoke kutoka juu!

5. Kutembelea marafiki

Huko Uskoshi-Scotland, jambo la kwanza ambalo watu huwa wanalifanya ni kutembelea marafiki, lengo likiwa ni mtu kuwa wa kwanza kutembelea kwa rafiki au familia wakati mwaka mpya unapoingia.

sUkimtembelea mtu unaweza kupeleka na zawadi pia.

5. Kula zabibu

Huko Uhispania, Saa sita usiku ya mwaka mpya inapofika utawakuta watu wanakula zabibu.

Hii ni kwa sababu kuna utamaduni wa kula zabibu kila inapofika saa sita usiku.

Lengo ni kuleta baraka na mafanikio katika miezi 12 katika mwaka.

6. Kupiga kengele

Baadhi ya mataifa kama Japan Korea kusini, watu hupiga kengele kuashiria kuwa ni mwaka mpya.

Japan,kengele huwa zinapigwa mara 108 hivyo huwa kuna kelele nyingi!

7. Kutoa vitu wasivyotumia nje

Huko Johannesburg Afrika Kusini, Watu huwa wanapenda kuanza mwaka mpya na vitu vipya katika nyumba.

Vitu ambavyo hawavihitaji huwa wanavitoa nje.

Huwa wanavitupa vitu ambavyo hawatumii tena kupitia madirishani.

8. Kutembea na sanduku abalo halina kitu

Baadhi ya mataifa kusini mwa Amerika, huwa wanatembea na masanduku ambayo hayana kitu siku ya mwaka mpya, kama ishara ya kukaribisha mwaka.

Mabegi hayo ambayo hayana kitu huwa ni ishara kuwa kutakuwa na mambo mengi ya kuvutia katika mwaka.