Mabadiliko ya hali ya hewa: Mkutano wa COP25 waanza kwa wito wa kufikiwa haraka maazimio muhimu

Chanzo cha picha, COP25
Viongozi wa kisiasa ma wanadilpomasia wa masuala ya hali ya hewa wanakutana huko Madrid kwa wiki mbili huku mabadiliko ya hali ya hewa yikiendelea kuwa tete.
Viongozi hao wanakutana katika mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa mwaka 2019 maarufu kama COP25.
Kulingana na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres bado mabadiliko yanaweza kufikiwa huku Shirika la kimataifa la Save the children likisema kuwa athari za mabadiliko hayo zimeacha mamilioni ya watu wakikumbwa na baa la njaa.
Shirika hilo limeongeza kuwa watu milioni 33 wanahitaji msaada wa dharura kwa sababu ya ukosefu wa chakula cha kutosha kuliko sabbaishwa na vibunga na kiangazi.
COP25 ni nini?

Chanzo cha picha, Reuters
Mkutano huu ulikuwa umepangiwa kufanyika Chile lakini ukafutiliwa mbali na serikali baada ya maandamano kutokea kwa wiki kadhaa.
Uhispania ilijitokeza kama mwokozi wao na kuamua kuwa mwenyeji wa mkutano huo unaohudhuriwa na viongozi 29,000 katika kipindi cha wiki mbili.
Akizungumza kabla ya mkutano huo, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema mizozo inayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa iko wazi na viongozi wa kisiasa hawana budi zaidi ya kutafuta ufumbuzi wa suala hilo.
Mkutano huu unalenga kufikia nini?

Chanzo cha picha, Save the Children
"Ni muhimu sana kufikiwa kwa maazimio ya kitaifa katika kipindi cha miezi 12 ijayo tena kwa haraka hasa kutoka kwa nchi zinazotowa kiwango kikubwa cha hewa chafuzi ili kuwezesha kufikiwa kwa dunia isiyokuwa na hewa chafuzi ifikapo mwaka 2050.
"Hatuna budi zaidi ya kusitisha shughuli za uchimbaji na kutumia njia mbadala za uzalishaji wa nishati kwa njia zengine za asilia,"Bwana Guterres amesema.
Karibia kila nchi duniani kwa sasa imetia saini na kuidhinisha makubaliano ya hali ya hewa ya Paris ambapo kila nchi itahitajika kutoa ahadi zake mpya kabla ya mwisho wa mwaka 2020.
Mkutano huu wa Madrid unaashiria kuanza kwa majadiliano yatakayofanyika kwa miezi 12 na kufikia ukomo huko Glasgow kabla ya kuanza kwa mkutano wa COP26 Novemba mwaka ujao.
Je ni nani atakayehudhuria mkutano huo?

Chanzo cha picha, Getty Images
Viongozi wa dunia karibia 50 wanatarajiwa kuhudhuria mkutao huo utakaofanyika katika mji mkuu wa Uhispania lakini Rais wa Marekani Donald Trump hatakuwepo.
Hata hivyo, Spika wa Bunge la Wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi pamoja na wajumbe wa Bunge la Congress wanatarajiwa kuhudhuria.
Huku uwepo wa Pelosi ukifurahiwa na wengi, wanamazingira wa Marekani wanataka kuona hatua madhubuti juu ya mabadiliko ya hali ya hewa zimechukuliwa.
"Japo ni vizuri kuona kwamba Pelosi anahudhuria mkutano wa Madrid badala ya Trump, kinachohitajika ni kuona hatua za vitendo zimechukuliwa", amesema Jean Su, kutoka kituo cha Marekani cha Bilolojia Anuai.
"Marekani inasalia katika historia kutokana na mchango wake katika masuala ya kutunza mazingira."
Madhumuni ya mkutano huu ni yapi?

Chanzo cha picha, Save the Children
Shirika la Kimataifa la Save the children linasema kwamba, mafuriko, maporomoko ya ardhi na vimbunga kumesababisha watu milioni 33 kuhitaji msaada wa dharura kwa ukosefu wa chakula cha kutosha huku zaidi ya nusu ya idadi hii ikiaminika kuwa watoto.
Hali hii imekuwa mbaya zaidi kwasababu vimbunga ambavyo vinasemekana kuwa vibaya zaidi vilikumba bara Afrika na kuathiri eneo hilo hilo hiyo ndani ya kipindi cha wiki mbili.
Kimbunga Idai kilikumba Msumbiji, Zimbambwe na Malawi mwezi Machi, na wiki sita tu baadaye, kimbunga Kenneth kikakumba Msumbiji na mamilioni ya watu wakaathiriwa na mafuriko.
"Mizozo inayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa inaendelea kwa sasa na kusababisha vifo, jambo ambalo limewalazimisha kuhama makazi yao na kutatiza hatma ya baadaye ya watoto," Ian Vale kutoka Shirika la Save the Children amesema.
Unaweza pia kusoma:
"Hali za dharura kama hizi zinaendelea kutatiza mfumo wa misaada ya kibinadamu hadi katika hatua ya kutoweza kudhibitiwa tena. Utokeaji wa vimbunga kunako pelekea ukosefu wa chakula kwasababu ya mabadiliko ya hali ya hewa, kunasababisha pengo kubwa kati ya ufadhili na ufikiaji na mahitaji wa misaada ya kibinadamu ambayo hayajatimizwa. Tunakaribia kufikia hali ya hatari katika eneo hili."
Nini kinatarajiwa kutoka?
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ataambia mkutano huo kwamba, kwa sasa dunia inakabiliana na athari mbaya zaidi zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Pia atahimiza mataifa mbalimbali kupunguza uzalishaji wa hewa chafuzi kwa kiwango kikubwa.
Bwana Guterres amesema ruzuku kwa vyanzo vya nishati ya kaboni vinastahili kusitishwa, na kuongeza kwamba mitambo ya uzalishaji umeme kwa kutumia makaa ya mawe inastahili kujengwa baada ya mwaka 2020.













