Tanzania: Waziri Jafo akana kauli yake kuhusu wagombea,asema hakueleweka

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kinamwandikia barua Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo kuacha kutumia jina na nembo ya Chama hicho kwa kuwa wamejitoa katika uchaguzi huo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo ameibuka tena na kukana kauli yake aliyoitoa awali.
Katika taarifa aliyoitoa kwa maandishi hii leo Bwana Jafo amesema kuwa kauli yake imezaa tafsiri tofauti na alichokikusudia.
''Kumekuwepo na tafsiri na uelewa na tafsiri tofauti wa maelezo niliyoyatoa jana tarehe 10 Novemba kuhusu wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa''. ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Kutokana na hali hii ambayo inadaiwa kuwa imeleta tafsiri nyingi zinazotofautiana, wizara ya TAMISEMI imetoa maelezo kwamba wagombea watakaoshiriki uchaguzi watakuwa ni wale;
- Waombaji wote ambao walichukua na kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa kugombea nafasi za Uongozi na kisha wakateuliwa na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi.
- Waombaji wote waliowasilisha pingamizi kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kuomba kuteuliwa na pingamizi zao na zikakubaliwa na
- Waombaji wote waliokata rufaa kwenye kamati za rufani za wilaya na rufaa zao kukubaliwa.
Kwa ujumla hizi si taratibu mpya, bali zimekuwa zikitumika miaka yote kwenye mchakato wa chaguzi nchini Tanzania. Kauli hii ya Jafo imeibua hisia kali.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1

Mwisho wa X ujumbe, 2
Hatua hii imekuja wakati viongozi wa baadhi ya vyama vya upinzani wakiwa wameususia uchaguzi huo uliopangwa kufanyika baadae mwezi huu wakidai kukiukwa kwa taratibu na kanuni za uchaguzi.
Naibu katibu Mkuu wa Chama upande wa Tanzania Bara, John Mnyika amesema CHADEMA imejitoa kwa sababu ya dhuluma zilizofanyika kwenye mchakato mzima kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 3
Kususia uchaguzi kuna maana gani?
Serikali Tanzania ilitangaza kuwa imewarejesha wapinzani walioenguliwa kwenye kinyang'anyiro cha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuwataka wananchi wote waliochukua fomu na kuzirejesha kushiriki kugombea. hatua ambayo hata hivyo haikuungwa mkono na upinzani wakiendelea kushikilia msimamo wao.
Said Msonga ni mchambuzi wa masuala ya kidiplomasia, siasa na kijamii , anasema ''Ususiaji huu una maana kuwa vyama vimebaini mapungufu katika zoezi hili yaliyosababisha sehemu kubwa ya wagombea wao kujikuta wameenguliwa, hivyo ni muhimu mapungufu hayo yatafutiwe ufumbuzi ili zoezi la uchaguzi lifanyike kwa uhuru na haki kwa pande zote''.
''Huu ni ujumbe ni ujumbe kwa Serikali na watendaji wake kuwa makini katika kuwasikiliza na kuwashirikisha taasisi zote za kisiasa ili mambo muhimu kama zoezi la uchaguzi lifanyike katika misingi ya uwazi, haki na usawa''. Ameeleza Msonga.
Unaweza pia kusoma