Mahakama ya rufaa imetengua uamuzi wa mahakama kuu uliozuia wakurugenzi kusimamia uchaguzi Tanzania

Chanzo cha picha, Thinkstock
Mahakama ya rufaa ya Tanzania imetengua uamuzi wa mahakama kuu uliowazuia wakurugenzi wa manispaa, wa miji na wilaya kusimamia uchaguzi mkuu.
Uamuzi huo unakuja mwaka moja kabla ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo ambapo ilielezwa kuhusika kwa maafisa, walioteuliwa na rais - ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha siasa, kuwa ni hatua inayohatarisha uchaguzi kutokuwa wa huru na haki.
Uamuzi huo ulitokana na uamuzi wa mahakama kuu uliotolewa na jopo la majaji watatu, Dk Atuganile Ngwala, Dk Benhajj Masoud na Firmin Matogolo uliobatilisha kifungu cha 7(1) cha Sheria ya uchaguzi kinachoipa mamlaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwateua wakurugenzi wa miji, manispaa na wilaya kuwa wasimamizi wa uchaguzi.
Pia mahakama ya rufaa imebatilisha kifungu cha 7(3) kinachoipa NEC mamlaka ya kuteua mtu yeyote miongoni mwa watumishi wa umma kuwa wasimamizi wa uchaguzi.
Katika hukumu hiyo mahakama imeeleza kwamba vifungu hivyo ni kinyume cha katiba ya nchi, ikibainisha kuwa wakurugenzi hao huteuliwa na rais aliyeko madarakani ambaye hutokana na chama tawala na kwamba wengine ni wanachama wa chama cha mamlaka inayowateua, jambo ambalo huathiri utendaji wao katika kutenda haki.
Pia ilisema kwamba sheria haijaweka ulinzi kwa tume ya NEC kumteua mtumishi yeyote wa umma kuhakikisha kuwa anakuwa huru katika kutekeleza majukumu yake.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Uamuzi una maana gani?
Uamuzi huo wa mahakama kuu umetokana na kesi iliyofunguliwa na mashirika kadhaa ya wanaharakati kupitia kwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Bob Wangwe, akitetewa na Wakili Fatma Karume.
Wakili wa Wangwe, Jebra Kambole akizungumza na BBC amesema wana mpango wa kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo hivi karibuni.
"Ni jambo la kukatisha tamaa kwa wengi nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na wanaharakati wa haki za binadamu, wanasiasa na wale wanaotamani uchaguzi wa Tanzania. Njia ya mbele itakuwa kukaa chini na kujadili athari za uamuzi huo na kuchukua njia nyingine.
"Lakini tunaamini kwamba korti ya rufaa ya Tanzania sio korti ya mwisho. Tutafikiria njia ya kwenda kwenye vikao vya kimataifa, na tunafikiria kupeleka kesi hiyo katika Korti ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu. Hiyo ndio tunafikiria njia ya mbele katika kulinda haki za binadamu nchini Tanzania. Na tunaamini kwamba tutafanya uamuzi sahihi kutoka kwa kiwango cha Kiafrika badala ya kuendelea na mapambano ndani ya nchi "
Hukumu hiyo imeondoa matumaini miongoni mwa wanasiasa wa upinzani na wafuasi nchini.
Walikuwa wamekaribisha uamuzi wa Korti Kuu ya kuwazuia maafisa wakuu walioteuliwa na serikali kufanya kazi kama maafisa wa kurudi katika uchaguzi kama hatua kuelekea mfumo ulioboreshwa wa uchaguzi nchini.
Tanzania imeweka uchaguzi mkuu mwaka ujao wakati wapinzani na wanaharakati wa haki wanaendelea kulalamikia kile wanachokiona kama ukosefu wa maboresho katika nafasi ya kisiasa nchini.













