Maoni: Syria inaweza kuwa mwanzo na mwisho wa uongozi wa Trump

US President Donald Trump

Chanzo cha picha, Getty Images

Sera za Rais Donald Trump kuhusu Syria ni janga alilolianzisha yeye mwenyewe na suala linaloweza kumgharimu kwa kiasi kubwa katika uchaguzi wa 2020, kulingana na naibu wa waziri wa zamani wa maswala ya kigeni PJ Crowley.

Hakutakuwa na nakala itakayomshtaki inayohusisha uamuzi wake wa hivi karibuni kuhusu Syria miongoni mwa baadhi ya maamuzi mabaya aliyochukua.

Lakini janga baya linaloendelea kufuatia hatua yake ya kumruhusu rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan huenda ikaadhimisha mwanzo wa mwisho wa urais wa Trump.

Trump atafanikiwa kukwepa mashtaka yaliowasilishwa bungeni dhidi yake - bunge la seneti linadhibitiwa na wabunge wa Republican licha ya kwamba anaendelea kujitia kitanzani mwenyewe.

Rais huyo anaamini kwamba mawasiliano yake ya simu na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky yalikuwa 'barabara'.

Nakala iliofichuliwa na Ikulu ya Whitehouse kuhusu mawasiliano hayo inatoa ushahidi mzito kwamba 'uhalifu ulitekelezwa'.

Syria ni tofauti, Sio suala ambalo anaweza kumsingizia Barrack Obama ama wabunge wa Democrats.

Bila kujali nia ya utawala kuiadhibu Uturuki kwa vikwazo vipya, hili ni tatizo ambalo Trump amejitakia.

Kwa Trump uamuzi wake wa kuondoa wanajeshi wa Marekani kutoka eneo hilo linalozozaniwa katika mpaka kati ya Syria na Uturuki ni sanjari na agizo lake la uchaguzi, akilitoa jeshi la Marekani kutoka kwa mgogoro mgumu na wenye gharama katika eneo la mashariki ya kati.

Alipotuma ujumbe wa twitter : Ni wakati wa sisi kujiondoa katika vita hivi visivyoisha, akisisitiza kwa herufu kubwa: 'Tutapigana pale ambapo kuna maslahi yetu na kupiga ili tushinde'.

Huku ikiwa huwezi kufutilia mbali taarifa zake nyingi nyingine zinazokanganya na machapisho yake ya mtandao wa twitter, wakati huu Erdogan alimsoma Trump kama kitabu na kumchezea shere.

Wakati Erdogan alipomwambia Trump katika mawasiliano ya simu ya hivi karibuni kwamba alikuwa na mpango wa kutuma majeshi yake Syria ili kuondoa uwezekano wa kuwepo kwa jimbo huru la Wakurdi katika mpaka na Uturuki .

Alidhania kwamba Trump atapinga wazo hilo kwa nguvu zake zote.

Hatahivyo katika mazungumzo mengine ya 2018, Trump alitoa ishara ya kutaka kuondoa vikosi vya Marekani kutoka Syria, aliripotriwa kumwambia Erdogan , Sawa fanya utakavyo.

Tumekwisha.'' waziri wa ulinzi James Mattis alijiuzulu kutokana na uamuzi huo, akiwa mmojawapo wa maafisa wakuu waliosalia kujaribu kuzuia msukumo wa Trump.

Rais Trump na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan 2018

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais Trump na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan 2018

Miezi kumi baadaye, wakati Erdogan alipoamua kuchukua hatua alijua kwamba alikuwa anasukuma mlango ambao tayari ulikuwa wazi.

Huku sera hiyo ya Trump ikizua ukosoaji wa kibinafsi, hata kutoka kwa kiongozi wa bunge la seneti la walio wengi Mitch McConnel , Wamarekani wengi wanaogopa vita vya mashariki ya kati na kuunga mkono kuwarudisha nyumbani wanajeshi.

Lakini Trump alifanya uamuzi mbaya zaidi.

Wanajeshi wa Marekani walio wachache, pamoja na wenzao wa Uingereza na wale wa Ufaransa walilenga kupunguza chimbuko la wapiganaji wa Islamic State mbali na kuwa kizuizi huku mazungumzo ya kuijenga upya Syria yakiendelea.

Licha ya msingi wake wa kibiashara, Trump alikubali kuachia uwezo ambao Marekani ulikuwa ukidhibiti ili kujenga Syria mpya.

Vikosi vya jeshi vya Syria na vile vya Urusi vilichukua nafasi ambayo ilikuwa imeachiwa na Marekani. Idadi ya wapiganaji wa Islamic State walitoroka kizuizini wakati huo kufuatia mashambulizi ya Uturuki.

Mpango wake wa kujiondoa katika mzozo huo unaingiliana na shinikizo yake kali dhidi ya Iran.

Ramani inayoonyesha hali halisi ya mzozo wa Syria
Maelezo ya picha, Ramani inayoonyesha hali halisi ya mzozo wa Syria
Presentational grey line

Kwa nini tuwe askari wa dunia?

Kwa wafuasi wengi wa Donald Trump waliohudhuria mkutano wake wa hadhara katika eneo la katikati la Minneapolis, maono yao ya mashambulizi ya Uturuki nchini Syria - yaliojiri baada ya kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani yalikuwa sawa.

''Nadhani ni bora kwamba tumewacha kuwashirikisha wanajeshi wetu katika tatizo lao la Uturuki na Syria'', alisema Alex Ledesma. 'Sisi sio vijakazi wao'

Mellissa Erra mwenye umri wa miaka 52 alisema: Kile ambacho kinaendelea huko kimekuwepo kwa miaka 100. Ni watu wetu wangapi ambao ni lazima wafariki huko , kwa kitu ambacho hatukufanya''? ''Wataendelea iwpao tupo huko ama hatupo''.

Lakini mwanajeshi wa zamani wa Marekani Eric Radziej alikuwa na msimamo tofauti.

''Nilidhania ni makosa kuondoka nchini Afghanistan haraka. Lakini iwapo mambo yatakuwa mabaya hatujasema kwamba hatutarudi''.

''Nchini Afghanistan tulisubiri muda mrefu zaidi kurudi''. Aliongezea: Kuna washirika wengine ambao wanaweza kwenda. Hatuwezi kubeba uzani wa ulimwengu mzima kila mara''.

Presentational grey line

''La muhimu zaidi , ni kwamba uaminifu na utegemeaji wa Marekani kama mshirika ni swali la wazi katika eneo la mashariki ya kati na zaidi''.

Trump alifutilia mbali umuhimu wa uhusiano wa kivita uliojaribiwa ambao umeendelea kati ya wanajeshi wa Marekani na wale wa Kikurdi wakati wa kampeni dhidi ya uongozi wa Islamic State.

Wapiganaji wa Kikurdi ndio waliokuwa wakiongoza vita hivyo ardhini ambapo waliteka mji wa Raqqa pamoja na ngome nyengine kuu za Islamic State.

Wanajeshi wa Marekani na Uturki katika doria ya pamoja kaskazini mashariki mwa Syria mwezi Oktoba

Chanzo cha picha, Handout

Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Marekani na Uturki katika doria ya pamoja kaskazini mashariki mwa Syria mwezi Oktoba

Kuna mengi ya kuangaziwa. Baadhi ya Wakurdi walipigana katika vita vya pili vya dunia, lakini hakukuwepo kwa taifa huru la Wakurdi wakati huo ama hata kwa sasa.

Ujerumani na Japan ambao wote ni washirika wakuu wa Marekani walikuwa wapinzani wakuu.

Wengine wanadhania kwamba Korea Kusini na Israel tayari yalikuwa maeneo yanayokaliwa na hayakuwa mataifa huru.

Japan na Korea kusini zina wasiwasi kwamba mpango wa Trump kutafuta muafaka na Korea Kaskazini huenda ukashindwa kuangazia matakwa yao ya usalama na suala la haki za kibinadamu.

Mtazamo wa Trump kuhusu Wakurdi utazidisha tu wasiwasi huo.

Hakuna taifa lililo na uhakika wa kutosha miongoni mwa washirika wa Marekani ambao pia ni wanachama wa Nato ama taifa lolote katika eneo la mashariki ya kati ambalo hutegemea Marekani kwa usalama wake.

Tayari Saudia ilivunjika moyo kuhusu hatua za rais Trump kubadilisha maamuzi yake kuhusu Iran - ikiangazia mashambulizi ili kujibu kuangushwa kwa ndege yake isiokuwa na rubani kabla ya kubadilisha uamuzi na kuamua kufuatilia njia ya mazungumzo na Iran .

Badala ya kuitenga Iran, Trump ameamua kumhusisha kila mtu katika jimbo hilo.

Lakini suala hilo huenda likazua tatizo mjini Jerusalem, Syria inaileta Iran hadi katika mlango wa Israel.

Jinsi Israel inavyoendelea kuhisi kwamba imeachwa kuishambulia Iran pekee, ndio hatari ya vita vya moja kwa moja ambavyo vitaivutia Marekani.

Obama na wenzake wa Ulaya walidhani walikuwa wamefurahishwa na makubaliano ya nyuklia ambayo Trump aliyaadhibu.

Ushirikiano wa Marekani na mataifa mengine ni muhimu sana kwa usalama na uthabiti wake wa kimataifa.

Huku akiwa hajaweka siri kuhusu jukumu lake kwa taifa la Marekani, Syria inaonyesha jinsi Trump anavyoshindwa katika kazi yake ya pili kama askari wa dunia, akiweka mbele maslahi ya Marekani na washirika wake muhimu.

Wanajeshi wa Marekani na wapiganaji wa Kikurdi wakionekana karibu na mpaka na Uturuki 2017

Chanzo cha picha, DELIL SOULEIMAN/AFP/Getty Images

Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Marekani na wapiganaji wa Kikurdi wakionekana karibu na mpaka na Uturuki 2017

Kuna gharama kubwa ya uamuzi wake wa kuondoka kwa vikosi vya Marekani na kuiachilia dunia ijitunze yenyewe. Habari nzuri ni kwamba sio uamuzi unaoungwa mkono na Wamarekani wengi.

Katika kongamano la hivi majuzi kuhusu maswala ya ulimwengi lililofanyika mjini Chicago, raia wengi walipendelea Marekani inayojihusisha katika maswala mbalimbali ya dunia , kuwasaidia washirika wake na umuhimu wa biashara ya kimataifa.

Lakini uamuzi huo wa Trump ni kinyume na nguzo muhimu za sera yake ya kigeni.

Syria pekee pamoja na jinsi anavyoichukulia Urusi inaonyesha wazi jinsi anavyoshindwa kusimamia uhusiano wa kimataifa.

Pia amepoteza mwelekeo kuhusu maslahi ya taifa na kuamua kufuata maslahi yake ya kisiasa.

Hayo yote yakijumlishwa huenda yakamkosesha urais bwana Trump.

Habari mbaya ni kwamba wapiga kura wa Marekani watalazimika kusubiri hadi mwezi Novemba kuchagua rais mwengine mbali na sera nyengine ya kigeni.

PJ Crowley ini naibu waziri wa zamani wa Marekani .