Uzinduzi wa reli mpya ya SGR 'isioelekea kokote' wazua maswali

Kenya imezindua awamu ya pili ya ujenzi wa gari moshi ya kisasa ya standard GAUGE itakaogharimu dola za kimarekani bilioni 1.5.
Reli hiyo ya abia itaanzia safari zake kutoka Nairobi kwenda eneo la Bonde la Ufa huko mjini Naivasha .
Kwa mujibu wa mamlaka za Reli nchini humo, ujenzi wa awamu nyingine ya reli hiyo kwa ajili ya mizigo utafanyika hapo baadae kufuatia kuchelewa kwa marekebisho ya reli ya zamani kuelekea Uganda na bandari ya nchi kavu katika eneo la Naivasha.
Kuna hofu huenda uzinduzi huo ukawa mwisho wa mradi huo mkubwa zaidi baada ya China kukataa kuufadhili.
Awamu ya pili ya ujenzi wa reli hiyo ilitarajiwa kuendelezwa hadi mpaka wa Kenya na Uganda (Malaba).
Wataalamu wanautaja kuwa usafiri usioelekea kokote lakini Serikali inashikilia kuwa mradi huo mpya utakuwa na manufaa makubwa.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Tofauti na uzindizi wa reli ya kutoka Mombasa hadi Nairobi, ilivvyozinduliwa kwa mbwembwe mwaka 2017, uzinduzi wa reli hii mpya haujapewa umuhimu mkubwa.
Wachambuzi wanasema Serikali inakabiliwa na wakati mgumu kuelezea faida za kiuchumi za mradi huo kwa sababu baadhi ya vituo havina shughuli nyingi katika mkoa wa bonde la ufa.
Mpango wa kuendeleza ujenzi wa reli hiyo hadi Kisumu, kupitia ziwa Victoria, hadi Uganda umekatizwa na hatua ya China kujiondoa katika ufadhili wake.
Katika kongamano la viongozi wa bara la Afrika na China mjini mataifa ya Afrika mjini Beijing, Serikali ya ilisema itafadhi miradi iliyo na manufaa ya kiuchumi pekee.

Ujenzi wareli hiyo uligharimu dola bilioni 1.5 sawa na (euro bilioni 1.1).
Huduma ya wateja inatarajiwa kuanza wakati wowote huku ile ya mizigo ikifuatia baadae japo haija bainika inaanza lini.
Uzinduzi wa reli ya kati ya Mombasa na Nairobi pia ilizua suala la faida yake kiuchumi kwa taifa la Kenya.













