Ni nani anayewapokea raia wa kigeni waliojiunga na kundi la kigaidi la Islamic State?

Mshukiwa wa wapiganaji wa IS aliyekamatwa nchini Syria mapema mwaka huu

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mshukiwa wa wapiganaji wa IS aliyekamatwa nchini Syria mapema mwaka huu

Uamuzi wa Marekani kujiondoa katika ngome zake Kaskazini mwa Syria, na vikosi vya Uturuki kuingia maeneo hayo, ambapo hatma ya maelfu ya washukiwa wa wapiganaji wa wafungwa wa kundi la kigaidi la Islamic State waliokuwa wakizuiliwa na vikosi vya Syrian Democratic Forces (SDF) haijulikani.

Wafungwa hao na familia zao- wanaoshikiliwa na vikosi vya Wakurdi - ni pamoja na raia wa kigeni kutoka sehemu tofauti duniani.

Marekani imetoa wito kwa mataifa ya kigeni kuwaondoa raia wao, huku ikilaumu mataifa ya Ulaya kwa kukataa kuchukua hatua hiyo.

Donald Trump

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Rais wa Marekani Donald Trump

Sasa ni raia wangapi wa kigeni wanazuiliwa na vikosi vya Syrian Democratic Forces (SDF) na je kuna taifa lolote lililowakubali kuwachukua?

Familia za wanamgambo wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa kundi la IS wanazuiliwa katika kambi kadhaa za wakimbizi wa ndani kwa ndani Kaskazini mwa Syria.

Kambi kubwa zaidi ni ya al-Hol. ambayo inawapa hifadhi karibu watu 70,000, zaidi ya 94% ya wakimbizi hao ni wanawake na watoto, miongoni mwao raia 11,000 wa kigeni.

Ramani Syria mwa Kaskazini
Presentational white space

SDF inasema wapiganaji 12,000 wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa IS wanazuiliwa katika magereza saba kaskazini mashariki mwa Syria.

Kati ya hao karibu watu 4000 wanakadiriwa kuwa raia wa kigeni amabo sio Wasyria au Wairaqi.

Ripoti ya Marekani iliyochapishwa mwezi Agosti ina idadi ya chini ya wapiganaji wa kigeni wanaozuiliwa Kaskazini mwa Syria na kwamba 2,000 kati yao wanatoka mataifa 50 tofauti.

Kati ya hao 800 kati yao wanatoka mataifa ya Ulaya na wengine wanatokea Mashariki ya Kati ,Afrika Kaskazini na Asia.

Kwa mujibu wa kituo cha kimataifa cha utafiti wa masuala ya msimamo mkali zaidi ya raia 41,000 wa kigeni walijiunga na IS nchini Iraq na Syria kati ya mwezi Aprili 2013 na Juni 2018.

Child after fall of IS stronghold

Chanzo cha picha, Getty Images

Je kuna mataifa lililowachukua raia wake?

Umoja wa Mataifa umesema nchi inastahili kuwajibikia raia wake ikiwa hawatafunguliwa mashitaka nchini Syria kulingana na viwango vya kimataifa.

Mataifa mengi yamekuwa yakipuuza kufanya hivyo kwa kuhofia maoni ya umma na changamoto za kisheria na raia wao waliojiunga na IS.

Shirika la kutetea haki la Human Rights Watch limetaja hatua ya kuwarejesha nyumbani raia wa kigeni kama mpango unaofanywa kwa njia ya "pole pole."

Linasema zaidi ya raia 1,200 wa kigeni - wengi wao watoto wameondolewa Syria na Iraq kwenda Kazahkistan,Uzbekistan,Urusi,Kosovo na Uturuki.

Presentational grey line

Kuna baadhi ya mataifa yaliochukua raia wao japo kidogo:

  • Ufaransa: Watoto 18
  • Marekani: Watu wazima 16 na watoto
  • Ujerumani: Hawazidi 10
  • Australia: Watoto wanane
  • Uswidi: Watoto saba
  • Norway: Watoto watano

Katika visa vingine, raia wa wameondolewa Iraq na kufunguliwa mashitaka katika mahakama ya nchi nyingine.

Mapepa mwaka huu, wanaume wanne raia wa Ufaransa walihukumiwa kifo nchini Iraq katika mchakato wa mahakama uliokosolewa vikali wakati huo.

Baadhi ya mataifa ya kigeni yamefutilia mbali urai wa watu wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa kundi la IS kurejea nyumbani- kwa mfano kesi ya Shamima Begum, kutoka Uingereza, ambaye anazuiliwa na who is katika kambi ya SDF-nchini Syria.

Idadi kubwa ya raia wa kigeni waliojiunga na IS huenda wakarudi makwao kabla ya vikosi vinavyo ongozwa na wapiganaji wa Kikurdi kuteka maeneo yaliokuwa yanakaliwa na wanamgambo hao are likely to mwezi Machi mwaka huu.