Hillary Clinton: Urusi inaandaa mgombea wa Democrat atakayemsaidia Trump

Hillary Clinton

Chanzo cha picha, Zach Gibson/Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 3

Mgombea wa zamani wa chama cha Democrat nchini Marekani Hillary Clinton amesema kwamba Urusi inamuandaa mgombea wa kike wa chama cha Democrat katika uchaguzi wa 2020.

Amesema kwamba taifa hilo linataka mgombea huyo kuwania kama mgombea wa tatu ili kugawanya kura na kusaidia kuchaguliwa tena kwa rais Trump.

Bi Clinton hakumtaja mgombea huyo, lakini anaaminika kuzungumzia kuhusu mbunge Tulsi Gabbard. Bi Gabbard alidaiwa kutaja madai ya bi Clinton kama ya 'uoga'.

Katika mahojiano na makao makuu ya mshauri wa rais wa zamani Barrack Obama David Plouffes, Bi Clinton ambaye yeye mwenyewe ni mwanachama wa Democrat alisema kwamba Urusi inamlenga mtu ambaye kwa sasa anaendelea na kampeni zake na kwamba wanamuandaa kuwa mgombea wa tatu.

Tulsi Gabbard

Chanzo cha picha, SAUL LOEB/Getty Images

"Anapigiwa upatu na Urusi,'' bi Clinton alisema, bila ya kumtaja. Wana mitandao chungu nzima na njia nyengine za kumuunga mkono kufikia sasa.

Hatahivyo Bi Gabbard alijibu akimshutumu bi Clinton kwa kuanza kampeni za kumharibia sifa yake.

Alimpatia changamoto mgombea huyo wa zamani kujiunga katika kinyanganyiro cha Ikulu badala ya kujificha nyuma ya wengine.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Presentational white space

Bi Gabbard ni mwanajeshi mkongwe na mgombea ambaye ameitaka Marekani kutojifanya kama polisi wa duniani.

Katika mjadala wa moja kwa moja akishirikiana na wagombea wengine 11 siku ya Jumanne, alisema kwamba madai ya vyombo vya habari vya Marekani kwamba anasukumwa na Urusi hayafai hata kidogo.

Bi Clinton pia alimshutumu mgombea wa chama cha Green Party Jill Stein kwa jina kwa kuwa msaliti.

Alizua uwezekano wa kwamba bi Stein anaweza kugombea kama mtu wa tatu kwa kuwa pia naye anasukumwa na Urusi.

''Ni kweli yeye anatumika na Urusi ,namaanisha kaabisa'', aliongezea Clinton. ''Wanajua kwamba hawawezi kushinda bila kuweka mgombea wa tatu''.

Siku ya Ijumaa , Bi Stein alimjibu bi Clinton akisema kwamba anajaribu kuukabili upinzani.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Presentational white space

Kampeni za Bi Stein za mwaka 2016 zilipata kura milioni 1.5.

Idadi ya kura alizopigiwa bi Stein katika majimbo matatu ambayo yalijitokeza yalikuwa muhimu kwa matokeo yote kwa jumla - Michigan, Pennsylvania na Wisconsin - zilizidisha ushindi wa Trump dhidi ya bi Clinton.

Hatahivyo kuna mjadala kuhusu iwapo bi Stein alisaidia katika uchaguzi wa bwana Trump kwa kuwa data zinasema kwamba sio wapiga kura wote wa Stein wangempigia kura bi Clinton ama chaguo lao la pili ama hata kupiga kura kabisa.

Stakhabadhi kutoka kwa uchunguzi wa wakili maalum Robert Mueller unaonyesha kwamba raia wa Urusi na mshirika walifanya kazi kuimarisha kampeni ya Bi Stein katika juhudi ya kuchukua kura kutoka kwa Bi Clinton.

Mwaka 2018 , bi Stein alitambua hatua ya rais kuingilia kati uchaguzi wa Marekani lakini akaongezea kwamba Marekani pia iliingilia uchaguzi ughaibuni.

''Kuingilia uchaguzi ni makosa na ni shambulio dhidi ya demokrasi na kwamba suala hilo linafaa kufuatiliwa'', aliambia CNN.

Lakini Marekani inapaswa kulichukulia kana kwamba inalijua jambo hilo.

Mgombea wa chama cha Green Party Ralph Nader mwaka 2000 alilaumiwa katika ikulu ya Whitehouse kwa kumsaidia George W Bush , kutoka chama cha Republican , kupata ushindi katika jimbo la Florida na hivyobasi Urais wa Marekani kwa Jumla.

Presentational grey line

Je ni nani atakayeshindana na Trump 2020?

Wagombea

Siku ya uchaguzi iko zaidi ya mwaka mmoja ujao lakini ushindani wa kuwa mgombea wa Democrat dhidi ya Trump tayari umeanza.

Kura ya maoni inasema kwamba Bi Warren na Bwana Bidden ndio wagombea walio kifua mbele huku bwana Sanders akiwa mgombea maarufu pia.

Wagombea wengine hawajulikani nje ya mji mkuu wa Washington.