Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Miaka 100 ya Mwalimu Nyerere: Mambo makuu matano aliyosisitiza katika hotuba zake
Hii leo, nchini Tanzania kunafanyika maadhimisho ya kuenzi miaka 100 ya aliyekuwa baba wa taifa hilo mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Kilele cha maadhimisho hayo kinafanyika kijijini kwake Butiama, Mkoani Mara, eneo alipozaliwa miaka 100 iliyopita na kuzikwa miongo miwili iliyopita.
Wageni kutoka kila pembe ya nchi wanahudhuria maadhimisho hayo yenye lengo la kuenzi mchango wa kiongozi huyu wa kitaifa ambaye utendaji wake na sifa zake zilitambulika ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Dr.Nyerere alizaliwa mwezi machi 1922 Butiama Tanganyika (Tanzania kwa sasa) na alikufa akiwa na miaka 77,na kuzikwa katika kijijini cha Mwitongo Butiama Kaskazini mwa Tanzania. Alifanikisha uhuru wa Tanganyika 1961 dhidi ya ukoloni wa Muingereza.
Nchi yake ilipata uhuru bila kumwaga damu , jambo alilosifiwa kama mmoja wa viongozi waliokua wana Imani ya kijamaa.
Pande zote za ulaya na Afrika sifa zake zilifana baada ya kuwa Rais wa kwanza wa Tanzania (muungano wa Tanganyika na Zanzibar), baadae alienzi utawala wa chama kimoja.
Mambo aliyosisitiza katika hotuba zake
Nyerere alifanya hotuba mbalimbali katika mikutano ya ndani na nje ya nchi wakati wa uongozi wake na hata baada ya kustaafu.
Alisisitiza mambo mengi kuanzia masuala ya uchumi, siasa na dini.
1.Ukabila, suala la ukabila ni jambo nyeti ambalo nyerere aligusia katika hotuba nyingi alizowasilisha.
''nilikutana na mama mmoja akaniambia alikua akifanya kazi jumuiya ya afrika mashariki, na sisi watu wa uganda tulikua tunajuana kwa makabila yetu , watu wa kenya walikua wakijuana kwa makabila yao, huyu mkikuyu, huyu mluhya. Lakini sisi watanzania hatujui makabila ya watu, nikawambia mama ni wakati huo, sasa hivi watanzania wanataka kujua makabila yao, ya nini, mnataka kutambika? Majirani zetu waalikua wanaiga kutoka Tanzania, sasa bila haya na sisi tunataka kuulizana makabila? Mwalimu Nyerere katika hotuba yake ya mkutano mkuu wa CCM 1995.
Nyerere alikemea suala la ukabila kila wakati alipopata nafasi ya kuzungumza na hakutaka kabisa kuwe na maswali kama wewe ni kabila gani? N katika hilo alifanikiwa kwa kiasi kikubwa, si kwa kawaida nchini Tanzania kuulizana kuhusu masuala ya ukabila.
2.Dini , ni jambo ambalo alisisiza sana katika hotuba zake, hasa kuwaasa viongozi wasitafute uongozi kwa kutumia dini.
''mambo haya ya kuchochea chuki za dini yakianza na tukayapa nafasi hayana simile, ni ikifika wakati yakashika kasi hakuna wa kuzuia''
3.Ujinga, maradhi na Umaskini, Mwalimu Nyerere alisisitiza juu ya mambo haya makuu matatu, kama na aliongeza pia kama Tanganyika na baadae Tanzania itafanikiwa kuyamaliza basi itakua miongoni mwa nchi itakayoendela zaidi duniani.
Katika suala la umskini alilipinga katika sana katika baadhi ya hotuba zake
''nchi hii ni bado ya wakulima na wafanyakazi, hatuwezi kuwa nchi ya watu wenye kudai na kudai, nawaomba ndugu zangu watanzania hatujalemaa sana, lakini kilema kipo, viongozi wetu wanadai na kudai tuu, watu ni maskini, wachache hao wana nguvu ya kuongoza nchi hii ndio wanaodai tuu'' Nyerere.
4.Uongozi, katika suala la uongozi, maadili ya uongozi ni jambo aliloliweka mbele sana, miongoni mwao ni viongozi ambao wanaweza kukidhi matarajio ya watanzania.
''watanzania wanataka mabadiliko, wasipoyapata ndani ya CCM, watayapata nje ya CCM, inatakiwa ukiulizwa swali kwamba huyu atapiga vita rushwa? Jibu litoke ndani ya moyo, nchi yetu ni maskini bado haijawa ya matajiri hivyo tunataka tuendelee kushughulika na umaskini wetu na matatizo ya wananchi, tunataka nchi yetu ipate kiongozi safi''.
5.Muungano, katika vitu ambavyo alikua akitamani sana kufanya ni kuunganisha nchi za Afrika mashariki, na kuwa na uongozi wa pamoja, ingawa hakufanikiwa katika hilo, alifanikiwa katika kuunganisha Tanganyika na Zanzibar mwaka 1994.
''matumaini yangu, ilikua kuunganisha nchi hizi za Afrika mashariki na kuwa muungano mmoja, kwa upande wa Zanzibar niliongea na Karume, akasema niko tayari ita watu wa magazeti sasa hivi, nikamwambia tufanye taratibu na tukafanikiwa. Kwa Afrika mashariki tungekua na serikali tatu za kila nchi na serikali ya muungano yani ya tanganyika na muungano''
Hayo ni baadhi tu ya mambo aliyokua akisisitiza sana Mwalimu Nyerere katika hotuba zake, hii leo nchini Tanzania wanaadhimisha miaka 20 ya kifo cha baba wa taifa hilo, lakini bado Falsafa zake zinaendelea kuishi.