Jumba la mateso la Nigeria: Shule ya Kaduna ilikuwa 'kama moto wa jahanamu'

Baadhi ya mateka hao walikuwa na majeraha yaliokuwa yalionekana kutokana na mateso

Chanzo cha picha, Nigerian Police

Maelezo ya picha, Baadhi ya mateka hao walikuwa na majeraha yaliokuwa yalionekana kutokana na mateso

Manusura a 'jumba la mateso' Nigeria aliye miongoni mwa wengine waliookolewa na maafisa wa polisi ameeleza yaliomsibu wakati wa kizuizi chake kuwa kama 'kuishi katika moto wa jahanamu'.

"Ikiwa unaswali watakupiga. Ukiwa unasoma watakupiga," Isa Ibrahim, mwenye umri wa miaka 29, ameiambia BBC.

Takriban watu 500 wanaume na wavulana wameokolewa kutoka katika jengo moja kaskazini mwa mji wa Kaduna , ambapo waliokuwa wakizuiliwa walikuwa wakinyanyaswa kingono na kuteswa kulingana na maafisa wa polisi wa Nigeria.

Watoto wadogo wa hadi miaka mitano ni miongoni mwa wale waliokuwa wamefungwa na nyororo hizo katika kile kilichodaiwa kuwa shule ya Kiislamu, maafisa wanasema.

Afisa wa polisi wa Kaduna Ali Janga aliambia BBC kwamba jumba hilo lilivamiwa kufuatia habari kutoka watu wasiojulikana kufuatia vitendo vyenye shauku.

Isa Ibrahim says he tried to escape the day before the police raid
Maelezo ya picha, Isa Ibrahim anasema laijaribu kutoroka siku moja kabla ya uvamizi wa Polisi

Masaibu yaliomkuta Isa Ibrahim

Ibrahim anasema alipelekwa katika jumba hilo wiki tatu zilizopita na familia yake, katika kilichotarajiwa kuwa ni 'kuirekebisha tabia yake'.

Anasema alijaribu kutoroka siku moja kabl aya uvamizi wa polisi.

anaeleza kwamba alifungwa kwenye jenereta la zamani na kukabiliwa na adhabu za kikatili, inayofahamika kama "Tarkila", ambapo mikono yake ilifungwa juu na akiachwa kuning'inia kutoka kwenye paa.

"Nina majeraha. karibu sehemu nzima ya mwili wangu," anasema. "hata ukilala - wanatumia fimbo kukuamsha."

Anasema aliachwa na njaa na alipewa wali mkavu kla. watu wanaozuiwa katika kituo hicho huwa 'wanapoteza nguvu kabisa', anaongeza.

Watoto walio na umri wa hadi miaka mitano walikuwa ni miongoni mwa waliookolewa kutoka jumba hilo linaloaminika kuwa limekuwa likiendehswa kwa miaka kadhaa.

Baadhi ya wanaume na wavulana wanatoka sehemu ya kaskazini mwa Nigeria lakini inaarifiwa wawili walitoka Burkina Faso.

Maelezo ya video, Jumba la mateso Kaduna: Polisi wawaokoa watu 500 waliofungwa na kunyanyaswa Nigeria
Presentational white space

Waliokuwa wakizuiliwa walisema kwamba waliteswa na kunyanyaswa kingono mbali na kuzuiliwa kuondoka katika kesi nyengine miaka kadhaa.

''Nimetumikia miezi mitatu hapa nikiwa na nyororo katika miguu yangu, Bell Hamza aliripotiwa akiambia vyombo vya habari vya Nigeria.

''Hiki kinafaa kuwa kituo cha kiislamu, lakini unapojaribu kuondoka hapa utavutia adhabu kubwa; Wanawafunga katika paa la nyumba."

Jina la shule hiyo ni Ahmad bin hambal for islamic Teachings

Chanzo cha picha, Nigerian Police

Maelezo ya picha, Jina la shule hiyo ni Ahmad bin hambal for islamic Teachings

Baadhi ya watoto waliambia maafisa wa polisi kwamba ndugu zao waliwapeleka huko wakiamni kwamba jumba hilo ni la shule ya Quran.

Watoto wawili walioachiliwa na maafisa wa polisi walisema kwamba wazazi wao waliwatuma Burkina Faso. Polisi wanaamini kwamba waliosalia wanatoka Nigeria.

Shule za Kiislamu ni maarufu katika jimbo hilo lakini kumekuwa na madai marefu ya unyanyasaji katika baadhi ya shule huku watoto wakilazimishwa kuomba fedha barabarani.

Mzazi mmoja aliambia chombo cha habari cha Reuters kwamba hawakujua iwapo watoto wao watakabiliwa na kiwango hicho cha mazingira mabaya.

Mateka hao wamezuiliwa katika kambi moja ambayo familia zao zinawasili na kuwatambua.

Hafsat Muhammad Baba wa jimbo la Kaduna aliambia BBC kwamba serikali itaendelea kutoa matibabu kwa wanaume hao na wavulana.