Simu ya Trump nchini Ukraine: Je kashfa hii inahusu nini?

Kuna mgogoro wa kisiasa nchini marekani unaomuhusu rais Donald Trump, raia wa kigeniu, maswala kuhusu maadili na madai kuhusu wapinzani wa kisiasa na yote haya yamesababisha kushtakiwa bungeni kwa rais Trump. Habari hii inaweza kuwa ngumu kuelewa hivuyobasi haya hapa majibu ya maswali magumu.
Kwa nini haya ni muhimu?
Wakosoaji wa rais Trump wanmtuhumu kwa kutumiauwezo wake wa urais kuilazimu Ukraini kuchunguza kuhusu habari mbaya za mpinzani wake wa kisiasa Mgombea wa chama cha Demovrat Joe Biden.
Bwana Trump na wafuasi wake wanadai kwamba makamu huyo wa rais wa zamani alitumia vibaya uwezo wake kuishinikiza Ukraine kutoshiriki katika uchunguzi ambao huenda ukampata na hatia mwanawe , Hunter.

Chanzo cha picha, Teresa Kroeger/Getty Images
Bwana Biden yuko kifua mbele kama mgombea wa chama cha Democrat kukabiliana na bwana Trump mwaka ujao.
Kwa upande mwengine , rais Trump yuko 'motoni'
Je mgogoro huu ulianza vipi?
Rais Trump na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky walifanya mazungumzo ya simu tarehe 25 mwezi Julai mwaka huu.
Katika mazungumzo hayo rais Trump anaonekana alimshinikiza mwenzake wa Ukraine kuwachunguza makamu wa rais wa zamani wa Marekani Joe Biden na mwanawe ambaye alikuwa mwanachama wa bodi ya kampuni inayomilikiwa na mfanyabiashara mmoja tajiri mwenye ushawishi wa kisiasa.
Simu hiyo ilipigwa baada ya utawala wa rais Trump kuchelewesha ufadhili wa kijeshi wa Ukraine katikati ya mwezi Septemba.
Bwana Trump pia alizungumzia kuhusu udukuzi uliofanyiwa barua pepe za chama cha Democrat katika simu hiyo ya Zelensky na kudai kwamba sava yake bado ipo mahala fulani nchini Ukraine.
Rais Trump anasema kwamba hajafanya makosa yoyote akitaja ukosoaji wake bungeni kama mzaha mkubwa.
Alikishutumu chama cha Democrat kwa kumtishia rais Zelensky kuzuia kura yao kuhusu sheria za Marekani zinazoathiria Ukraine na kusema kwamba mgogoro huo ulifanyika ili kutopatia kipau mbele mkutano wa bwana Trump katika Umoja wa matifa.
Je wanasiasa wengine wanasemaje?
Wabunge wa chama cha Democrats katika bunge la Congress wanasema kwamba simu hiyo iliofichuliwa ni thibitisho kwamba bwana Trump alitoa shinikizo kwa taifa jingine kwa manufaa yake ya kibinafsi.
Democrats wanasema rais alitaka Ukraine kuanzisha uchunguzi kuhusu ufisadi kwa kuwa hatua hiyo itaharibu sifa ya bwana Hunter na babake.
Wanachama kadhaa wa chama cha Republican walijitokeza kumtetea Trump .
Hii inaonyesha jinsi swala hilo lilivyochukua mirengo ya kichama na kugawanya watu kisiasa.
Hatahivyo mwanachama mmnoja wa Repoublic amesema kwamba anataka kujua zaidi.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe

Je mfichuzi alitoa malalamishi gani?
Kulingana na habari kutoka kwa zaidi ya maafisa 12 , mfichuzi huyo ambaye hajatajwa anadai kwamba rais Trump alitaka usaidizi kutoka Ukraine katika uchaguzi wa 2020.
Hati hiyo yenye kurasa tisa inataja simu hiyo ya rais Trump iliopigwa kwa rais wa Ukraine tarehe 25 Julai ambapo rais Trump alidaiwa kumshinikiza rais Zelensky kuchunguza vitendo vya familia ya Biden na kutoa ripoti ya sava zozote zinazomilikiwa na kamati kuu ya chama cha Democrat.
Mfichuzi huyo anadai baada ya kugundua uzito wa mazungumzo hayo, maafisa wa Ikulu ya Whitehouse walijaribu kuficha maelezo ya simu hiyo kwa kupelekea hati ya simu hiyo katika mfumo mwengine ili kuhifadhi maelezo muhimu.
Wakili wa bwana Trump, Rudy Giuliani alidaiwa kuhusika pakubwa katika juhudi za kuishinikiza Ukraine kuhusu mahitaji ya Trump na kukutana na maafisa kadhaa wa Ukraine kama mjumbe wa kibinfsi wa rais Trump.

Malalamishi hayo pia yanadai kwamba mapema mwezi Julai -wiki kadhaa kabla ya simu hiyo kupigwa bwana Trump aliagiza maafisa kukatiza ufadhili wa kijeshi wa Marekani kwa Ukraine bila kutoa sababu.
Katika barua hiyo, mfichuzi huyo amekiri kwamba hawakushuhudia kisa hicho moja kwa moja lakini akasema kwamba akaunti zilisozambazwa na maafisa wengine zilikuwa zinafanana.
Malamishi hayo yalitolewa kwa kamati za bunge na seneti siku ya Jumatano na ripoti zinasema kwamba majadiliano yanaendelea kumruhusu mfichuzi huyo kutoa ushahidi wake.
Joseph Maguire , kaimu mkurugenzi wa idara ya Ujasusi nchini humo amekuwa akitoa ushahidi wake hadharani kabla ya kamati ya ujasusi ya bunge.
Mapema wiki hii, rais Trump aliahidi kutoa nakala hiyo ya mazungumzo yake ya simu na Zelensky ambayo itathibitisha kwamba simu hiyo haikuwa ya kweli.
Nakala iliotolewa hatahivyo haikuwa ya simu yote, lakini maandishi ya mazungumzo yaliochukuliwa na maafisa hao yalisikilizwa.
Je rais alifanya kitu chochote kinyume na Sheria?
Madai mabaya zaidi ni kwamba rais alimshinikiza kiongozi wa taifa la kigeni kupewa habari mbaya kuhusu mpinzani wake wa kisiasa huku akitishia kusimamisha ufadhili wa kijeshi.
Je hatua hiyo ni kinyume na sheria?
Kuna mifano ya hapo awali. Swala hilo linarusidha uchunguzi wa miaka miwili uliofanywa na Robert Mueller kuhusu ushirikiano wa kampeni ya rais Trump na Urusi mwaka 2016.
Ripoti ya wakili huyo maalum ilielezea kuhusu mawasiliano ya mara kwa mara kuhusu kampeni yake na raia wa Urusi, ukiwemo mkutano wa mwezi Juni 16 kati ya maafisa wakuu wa kampeni kama vile Donald Trump Jr na maafisa kadhaa wa Urusi walio na uhusiano na ikulu ya Urusi.
Kumekuwa na mjadala kuhusu iwapo kuuchunguza upinzani kupitia taifa la kigeni ni ukiukaji wa kampeni lakini bwana Mueller alikataa kuwasilisha mashtaka dhidi ya Trump.
Wakili huyo maaluma alitamatisha kwa kusema kwamba maelezo ya sera ya idara ya mahakama yanamzuia rais aliyepo mamlakani kutoshtakiwa, hivyobasi hata iwapo rais Trump alitekeleza vitendo vya uhalifu kupitia maswala aliyotekeleza hawezi kushtakiwa kwa sasa.
Na kupitia hilo swali zuri zaidi litakuwa....
Je rais Trump alifanya makosa ya kushtakiwa bungeni?
Mchakato wa kikatiba wa jinsi ya kumuangazia rais ambaye amefanya makosa ni kupigiwa kura huku thuluthi mbili za wabunge wa seneti zikimng'oa madarakani.
Katiba ya Marekani inaelezea sababu za kumshtaki rais bungeni kuwa uhaini, ufisadi ama uhalifu wa kiwango cha juu.
Hatahivyo makosa hayo ya kumshataki rais ni kulingana na seneti itakavyosema.
Tangu kukamilishwa kwa uchunguzi wa Mueller , ngoma za kutaka kumshtaki bungeni rais miongoni mwa wanachama wa Democrats ambao wanamiliki idadi kubwa ya wajumbe imekuwa ikiongezeka.
Awali, hatahivyo uongozi wa chama cha Democrat bungeni ulikuwa tayari umepanga kufanya uchunguzi rasmi ambao ungesababisha kushtakiwa kwa rais bungeni.
Spika wa bunge hilo Nancy Pelosi alikuwa amependekeza kwamba hatua kama hiyo huenda ikaharibu matarajio ya wapiga kura wa Democrats katika majimbo ya walio na msimamo wa kadri na hiyo haitakuwa na muhimu wowote kwa kuwa wanachama wa Republican ndio wengi katika bunge la seneti hivyobasi hawatamuondoa rais.
Lakini siku ya Jumanne , bwana Pelosi alitangaza kwamba Democrats walikuwa wameanzisha uchunguzi rasmi.
Alisema kwamba rais huyo amekiuka sheria za majukumu yake na kutaka awajibishwe.
Je kuna lolote kuhusu madai hayo ya Biden na mwanawe?
Madai dhidi ya Biden yanayoshinikizwa na Trump na wakili wake aliyekuwa Meya wa Mji wa New York Rudy Giuliani yanafuatia juhudi za makamu huyo wa zamani kumuondoa mwendesha mashtaka wa Ukraine Viktor Shokin 2016.
Kuanzia mapema 2014 Hunter Biden alikua katika bodi ya kampuni moja ya kawi Burisma Holdings.
Mwaka uliofuatwa bwana Shokin alisema kwamba Burisma ilikuwa miongoni mwa kampuni alizokuwa akizilenga katika kukabiliana na ufisadi.
Kufikia 2016, kulikuwa na wasiwasi katika utawala wa Obama kwamba bwana Shokin hakufuatilia vizuri visa vya ufisadi na makamu wa rais Biden alitoa makataa kwa bunge la Ukraine kumfuta kazi bwana Shokin la sivyo likose mikopo.

Chanzo cha picha, Pool/Getty Images













