Mugabe kuzikwa nyumbani kwao

The body of former Zimbabwean President Robert Mugabe arrives at the Blue Roof, his residence in Borrowdale, Harare, Zimbabwe, on 11 September 2019

Chanzo cha picha, Reuters

Muda wa kusoma: Dakika 2

Mwili wa rais wa rais wa kwanza wa Zimbabwe, Robert Mugabe utazikwa nyumbani kwao, baada ya serikali kubadili msimamo wake wa awali kuhusu mazishi hayo.

Mugabe alifariki mwezi mapema mwezi huu akiwa na miaka 95 na ibada ya mazishi kufanyika katika mji mkuu wa Harare.

Serikali ilikua imepinga ombi la familia yake la kumzika kiongozi huyo katika eneo la Zvimba, na kushinikiza azikwe katika makaburi ya mashujaa wa kitaifa.

Familia yake hatimae ilikubali lakini serikali ikabadilisha msimamo huo siku ya Alhamisi.

Haikubainika ni nini kilichosababisha mipango ya awali ya mazishi ya Mugabe kubadilishwa.

Familia ya Mugabe ilikubali azikwe katika makaburi ya Heroes Acre baada ya makubaliano kufikiwa kuwa mnara wa makumbusho utajengwa kumuenzi kiongozi huyo wa kwanza wa Zimbabwe.

Katika taarifa iliochapishwa Alhamisi, Waziri wa Mawasiliano Nick Mangwana alisema mabadiliko hayo yanazingatia sera ya "kuheshimu uamuzi wa familia ya marehemu".

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Mugabe alifariki Singapore alipokua anapokea matibabu yasaratani na mwili wake kusafirishwa nyumbani Zimbabwe.

Baada ya kifo chake familia yake ililamika hadharani kuwa haikushauriwa kuhusu mipango ya mazishi yake ya kitaifa.

Katika taarifa familia hiyo iliilaumu serikali kwa kutumia nguvu kupanga mazishi ya Mugabe katika makaburi ya mashujaa kinyume na "matakwa yake [Mugabe]".

Taarifa hiyo aidha ilisema kuwa ombi lake la mwisho lilikua la mke wake , Grace Mugabe, kutoondoka kando ya jeneza lake hadi atakapozikwa.

Mama Taifa wa zamani Zimbabwe, Grace Mugabe

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Inaaminiwa kuwa Mama Taifa wa zamani Zimbabwe, Grace Mugabe, alikuwa amrithi mume wake

Familia yake inasemekana kughabishwa na jinsi kiongozi huyo alivyong'olewa madarakani na mshirika wake, wa zamani Rais Mnangagwa, miaka miwili iliyopita- halia mbayo huenda imesababisha mvutano kuhusu mahali atakapozikwa.

Bw. Mnangagwa alipendekeza kiongozi huyo azikwe Heroes Acre.

Mugabe, alikua Rais wa kwanza wa Zimbabwe baada ya nchi hiyo kupata uhuru 1980.

Miaka ya awali ya uongozi wake, alisifiwa kwa kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya na elimu kwa waafrika walio wengi

Maelezo ya video, Enzi ya kisiasa ya Mugabe

Lakini baadae utawala wake ulikumbwa na mzozo mkubwa wa kiuchumi na ukandamizaji wa wapinzani wake.

Alikuwa madarakani kwa karibu miongo minne kabla ya kuondolewa kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 2017 na wadhifa wake kuchukuliwa na Rais wa sasa Emmerson Mnangagwa.