Ndege ya United Airlines yalizimika kutua kumuoka abiria aliyekwama chooni

Chanzo cha picha, Getty Images
Ndege ya United Airlines ililazimika kugeuza mkondo kati kati ya safari baada ya mmoja wa abiria wake kukwama chooni.
Ndege hiyo iliyokuwa safarini kutoka Washington DC kuelekea San Francisco, ililazimika kubadili mkondo na kutua katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Denver siku ya Jumatano.
Mlango wa choo "ulikataa kufunguka" ndege ilipokua angani, msemaji wa shirika la ndege la United Airlines aliimbia BBC.
Abiria huyo -wa kike - aliokolewa baada ya ndege kutua. Bila kujeruhiwa, shirika hilo la ndege lilisema..
Kanda ya video inayomuonesha makanika akijaribu kufungua mlango wa choo hicho imesambazwa katika mtandao wa Twitter.
"Tunajitahidi kufungua mlango mami; tutakusaidia usiwe na hofu," mtu mmoja alisikika akisema katika kanda hiyo.
Jennifer Gettman, mmoja wa abiria waliokua ndani ya ndege hiyo, ameiambia KPIX- TV kuwa mwanamke huyo alionekana kuwa mtulivu alipotoka ndani ya choo hicho.
"Kila mmoja alipiga makofi , mwanamke huyo alipofanikiwa kutoka ndani ya choo hicho huku wengine wakimsikitikia," Bi Gettman alisema. "Kwa kweli sijui alikua katika hali gani ndege ilipotua akiwa chooni, lakini alikuwa sawa."

Chanzo cha picha, @taylorkkimber
Abiria wanasema mwanamke huyo alikwama ndani ya ndege kwa karibu saa moja. "Tupatieni vichekesho vya bafuni," abiria mwingine aliandika kwenye.
Ndege hiyo yenye nambari ya usajili 1554 ilitarajiwa kutua mjini San Francisco muda mfupi baada ya saa mbili na nusu za usiku kwa saa za huko ambayo ni sawa na saa (03:38 GMT) lakini ilitua Denver saa moja na dakika ishirini na moja.
Ndege hiyo iliondoka San Francisco karibu masaa mawili baadae.
United Airlines imesema kuwa imewaomba radhi "abiria waliokua kwenye ndege hiyo pamoja na mwenzao aliyekwama ndani ya choo cha ndege hiyo".














