Kumlaghai mwenzi wako wakati wa kushiriki ngono ni kosa kisheria

Stock image of man and woman in bed, with man holding condom

Chanzo cha picha, Getty Images

Je, uongo unaotumika na baadhi ya watu ili kumrubuni mwenzi wake kufanya mapenzi ni ubakaji?

Mwanaume mmoja alimdanganya mpenzi wake kuwa amefunga kizazi hivyo mwanamke alikubali kufanya naye mapenzi kwa ridhaa yake kabisa, lakini je uongo wa namna hiyo tunaweza kutafsiri kuwa ni ubakaji?

Tunawezaje kusema kuwa mwanamke huyo amebakwa wakati hakuna nguvu iliyotumika katika tendo hilo.

Kesi yao inakuja kwa sababu mwanamke alitaka mwenzi wake kutumia kondomu lakini mwanaume alitaka kutotumia kinga kwa madai kuwa amefunga kizazi.

Mwanamke huyo mwenye miaka 42, alikuwa mama tayari na hakutaka mtoto mwingine .

Baada ya mwenzi wake kumjulisha kuwa kile alichomwambia kuhusu kufunga uzazi si jambo la kweli, mwanamke huyo alikunywa vidonge vya kuzuia mimba lakini bado alipata ujauzito.

Wapenzi hawa ambao walifanya mapenzi mara mbili, Sally alimshtaki mwenzi wake Lawrance kwa kosa la kumbaka.

Sheria nchini Uingereza , katika makosa ya unyanyasaji wa jinsia ya mwaka 2003, inasema kuwa mtu ana uhuru wa kufanya maamuzi ya kukubali au kukataa.

Hivyo kama mwanamke au mwanaume amemlaghai mwenzie kwa kumpa taarifa za uongo ili afanye naye mapenzi basi huo ni uhalifu mkubwa mbele ya sheria.

Lawrance ni mmoja kati ya wengi wanaotumia uongo ili kupata mwanya wa kufanya tendo la ndoa.

Je, inawezekana wengine wengi wanaotumia mbinu hiyo kuweza kuadhibiwa?

Je, kuvua kondom katikati ni ubakaji?

Stock image of condoms

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wanaume wengi huwa wanakwepa kuvaa mpira wa kondomu kwa madai kuwa inaondoa ladha

Kelly Davis, ni profesa msaidizi wa chuo kikuu cha at Arizona ambaye alifanya utafiti kwa wanawake na wanaume wa kati ya miaka 21-30 kuhusu matumizi ya kondomu.

Njia gani watu huwa wanatumia kukwepa kutumia kondomu wakati wenza wao wanataka kutumia.

Kati ya wanaume 313 , asilimia 23.4 ya wanaume hao wanatumia uongo ili kukwepa kutumia tangu wakiwa na miaka 14.

Asilimia ishirini huwa wanadanganya kuwa hawatamwaga shahawa ndani ya uke lakini wanajikuta wanashindwa kufanya hivyo.

Huku wengine huwa wanadanganya kuwa wamepima afya zao na hawana magonjwa ya zinaa.

Dkt.Davis na watafiti wengine waliwatafiti wanawaangazia wanaume wenye umri mdogo, vijana wengi wanadhani kutumia nguvu ndio kunaonekana kuwa ni ubakaji.

Kati ya wanawake 530 waliofanyiwa utafiti, asilimia 6.6 walianza kutumia uongo tangu wakiwa na umri wa miaka 14, na mbinu yao kubwa ni kuwa wamejizuia kupata ujauzito.

Dkt Davis na watafiti wengine waliwafanyia utafiti vijana wanakubaliana kutumia kondomu lakini katikati ya tendo mmoja anaitoa kabla ya kumaliza tendo.

Utafiti kati ya vijana wenye umri wa miaka 21-30 ulionyesha tena kuwa karibu asilimia kumi ya watu 626 walikiri kuwa walikuwa wanatumia mbinu hiyo tangu wakiwa na miaka 14.

Je kama mwanaume asipomwaga shahawa nje ni ubakaji?

Man and woman sitting on bed

Chanzo cha picha, Getty Images

Katie Russell, mtaalamu wa kesi za ubakaji anaamini kuwa kumwaga shahawa ndani ya uke ni ubakaji.

Kama watu wamekubaliana kushiriki tendo la ngono kwa makubaliano fulani na endapo makubaliano hayo hayataafikiwa basi huo ni ubakaji kisheria.

Sheria hiyo inawahusisha hata wanandoa kama mume na mke wamekubaliana namna ya ufanyaji mapenzi kuwa mume anapaswa kumwaga nje shahawa na endapo makubaliano yakienda tofauti basi huo ni ubakaji.

Je, kudanganya kuhusu hali ya kiafya ni ubakaji?

Man holding arm after blood test

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Vijana wengi huwa wanadanganya kuwa wamefanya vipimo vya magonjwa ya zinaa

Watu wanaodanganya kuwa wamepima magonjwa ya zinaa ni ubakaji kwa sababu unaweza kumuhatarisha mwingine kiafya kwa sababu ya uongo.

Je, kama mwanamke amedanganya kuwa anatumia vidonge?

Woman holding contraceptive pills and a condom

Chanzo cha picha, Getty Images

Je endapo mwanamke atadanganya kuwa anatumia dawa za kuzuia mimba ni kosa kisheria pia hata kama uongo aliosema unaweza kumuathiri yeye mwenyewe .

Suala hilo limelinganishwa na wanaume kudanganya kufunga kizazi.

Mtaalam anasema, mwanamke mara nyingi ndio anakutana na athari katika uongo hivyo kama atadanganya, matokeo hasi yatakuwa upande wake ndio maana kudanganya kutumia vidonge sio ubakaji.

Ulaghai mwingine wa kimapenzi?

Man removing wedding ring behind his back

Chanzo cha picha, Getty Images

Watu wengine huwa wanadanganya kuwa hawapo katika mahusiano wakati wameoa au wameolewa, huo pia ni ubakaji ingawa kesi nyingi za namna hiyo huwa hazipelekwi mahakamani.

Presentational grey line