Dar es Salaam: Maelfu wakusanyika wakitegemea kupokea fedha za bure

Chanzo cha picha, KWA HISANI
Si jambo la ajabu kwa watu kukusanyika katika uwanja wa mpira.
Lakini mkusanyiko wa maelfu ya watu ulioonekana hapo jana katika uwanja wa mpira wa taifa jijini Dar es salaam ulistaajabisha wengi na kuzua mjadala mkali katika mitandao ya kijamii.
Watu hawa wapatao elfu 40 ambao wengi wao walikuwa ni wanawake, waliokusanyika hapo kwa mategemeo ya kupata fedha za bure lakini mambo yalikwenda kombo.
Maswali na majibu yaliendelea kwenye mitandao ya kijamii hata kabla kikao hicho akijafika hatima yake, wengine wakidai watu hao walihaidiwa milioni 10 za kitanzania ambazo ni sawa na dola 4000 kila mmoja.
"katika dunia hii kuna mtu anaweza kutoa fedha za bure kweli?"
Kampeni mbalimbali kabla ya siku hiyo ziliwahamasisha watu kuwa kuna ugeni kutoka Korea na yuko tayari kutoa fedha za bure kwa kila atakayefika,
"Watu walikuwa wengi ila tumetoka hatujaelewa kitu kuhusu pesa walizosema watatoa m. 1 kila mtu" mmoja ya washiriki ameiambia BBC.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Miongoni mwa watu waliofika katika tamasha hilo wanasema kuwa taarifa waliyoipata ilikuwa tofauti na kile walichokikuta, " sisi ni wafanyabiashara ndogondogo na tuliambiwa tukifika huko tutapata pesa za mitaji kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza biashara lakini wakati tunaanza kusikiliza waliotualika, tunaambiwa kuwa ni tamasha la amani katika familia ,"
"Maisha magumu ndio yametufanya tuhudhurie kwa wingi, lakini kile tulichokipata kimetukatisha tamaa, tumepoteza muda wetu na kazi zetu" mshiriki mwingine aeleza.
"Tuliambiwa kufika alfajiri sana na mpaka kikao kimeisha, hakuna tulichopata wala kusikia kuhusu fedha".
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Kwa mujibu wa gazeti la The Citizen, muandaaji wa tamasha hilo kutoka taasisi ya 'Family Federation for World Peace and Unification' Stylos Simba amekanusha madai ya kuwahaidi watu fedha za bure.
Na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo lililodaiwa kuwahaidi watu fedha za bure, ameeleza katika gazeti hilo kuwa lengo la tamasha halikuwa kutoa fedha za bure lakini pia jambo hilo liwe funzo kwa kila mtu.













