Miungu wa kesho: Ipi hatma ya dini siku zijazo?

Chanzo cha picha, Getty Images
Miaka karibu 3,500 iliopita, Iran ilikua na dini yake iliyofahamika kama Zoroaster ambayo inasadikiwa kuwa dini ya jadi ya Uajemi.
Zoroaster ilikuwa imani rasmi ya Dola kuu ya Uajemi, na hekalu lake la moto lilihudhuriwa na mamilioni ya wafuasi.
Maelfu ya miaka baada ya ufalme wao kuanguka, wafuasi wa Zoroaster waliteswa hadi wakajiunga na dini mpya ya washindi wao, Uislamu.
Miaka 1,500 baada ya imani ya Zoroaster kupotea moto wake unaoaminiwa kuwa mtakatifu huhifadhiwa na wafuasi wachache.
Tunachukulia tu kwamba dini huzaliwa, hukua na kufa - lakini pia tunapuuza ukweli huo.
Lakini sisi pia tunahadaiki kirahisi.
Mtu anapoanzisha dini mpya mara nyingi hupuuzwa kuwa dhehebu lakini imani yake ikitambuliwa tunachukulia mafundisho na itikadi zake kama kitu kitakachodumu milele.
Na dini inapokufa, inakuwa hadithi, na madai ya utakatifu wake unaisha sawa na hadithi za watu wa asili ya Wamisri, Wagiriki na Waorse amabo sasa hadithi zao sio maandishi takatifu.
Hadi wa leo madhehebu makubwa ya kidini yamekua yakibadilika katika historia.
Katika dini ya Kikrsto kwa mfano Kanisa la kwanza lilikua kubwa: Hati za zamani zilijumuisha maisha ya familia ya Yesu na ushuhuda kwa ukuu wa Yudasi.
Ilichukua karne tatu kwa kanisa la Kikristo kujumuisha maandiko - na ilipofika 1054 ikagawanyika katika makanisa ya Orthodox na Katoliki.
Kutoka wakati huo, Dini ya Kikristo iliendelea kukua na kugawanyika katika makundi mengi ambayo yanadai kuwa ya kipentekoste.
Lakini ukiamini kuwa imani yako iko pale pale basi huenda usione mabadiliko hayo hata kidogo.
Historia inaonesha kuwa hata imani yetu iwe imara kwa kiwango kikubwa leo huenda siku zijazo imani zetu zikabadilika, kubadilishwa na vizazi vyetu vijavyo au kupotea kabisa.
Ikiwa dini zilibadilika zama za kale kuna uwezekano hali kama hiyo ikajirudia siku zijazo?
Je kuna ukweli wowote kuwa imani ya miungu nayo itapotelea mbali?
Na kadri maendeleo yetu na teknolojia zake zinavyozidi kuwa ngumu zaidi, Je kuna uwezekano wa kuibuka kwa aina mpya za ibada?
Kujibu maswali haya ni vyema kujiiliza: Kwa nini tuna dini?

Chanzo cha picha, Getty Images
Mfaransa huyo alikuwa anahoji juu ya imani ya watu kwa Mungu kama inafanya kazi kiufasaha.
Kama Mungu hakuruhusu makanisa mengi iweje kila kukicha yanafunguliwa.
Wanafunsi wa dini ya sasa walikubaliana naye kuwa wazo la imani linapaswa kuzingatiwa na dini zote katika utendaji wake.
Kuna matajiri wengi wanatumia dini kukandamiza watu maskini wakidai kuwa wanataka kuwasaidia kumbe ni uongo.
Lengo la dini ni kuwajumuisha watu waishi pamoja kwa amani na upendo lakini si kutumia dini kuunga mkono itikadi za siasa au kutoa matumaini ambayo utekelezaji wake ni hafifu.
Wamekuwa wakianzisha imani zao huku wakichanganya tamaduni mbalimbali.

Chanzo cha picha, Getty Images
Msimu wa sikukuu za dini kama Krismasi na pasaka, viashiria vingi vya upagani vimejumuishwa katika sherehe hizo za dini jambo ambalo si sawa.
Mpaka leo hii jamii yetu imechanganya imani ya dini na tamaduni mbalimbali na idadi ya watu wanaodai kuwa hawana dini inazidi kuongezeka.
Wanasayansi nao wanataka watu waeleze namna nyingine ya ulimwengu.
Licha ya kupotea kwa idadi ya pamoja kwa namba.
Mwaka 2015, watafiti walibaini kuwa dini kubwa duniani huwa zinaegemea kwenye mifano, uhamiaji na mawasiliano.
Pamoja na kushuka kwa imani ya watu , waumini wapya wataongezeka kutoka asilimia 84 mpaka 87% ifikapo mwaka 2050.
Waislamu pia idadi yao itakuwa na kulingana namba ya wakristo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mabadiliko kama hayo ndio baadi ya mabo waanzilishi wa baadhi ya makundi mapya ya kidini wanataka kuona.
Suala la kuzifanya makundi hayo kuwa rasmi sio muhimu cha msingi ni kupata uungwaji mkono na wafuasi wengi katika harakati zinazopiganiwa katika jamii.

Chanzo cha picha, Getty Images
Baada ya kutumia miongo kadhaa kutafuta suluhisho la kiuhandisi la kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa mwanzilishi wake Olya Irzak alibaini kuwa suluhisho halisi halipo katika juhudi za kiufundi bali ni kutafuta uungwaji mkono na jamii.
"Uungwaji mkono huo ni sawa na kuwaongoza watu katika dhehebu la kulinda mazindira ?" anasema. "ni dini inayokabiliwa na changamoto kubwa."
Miaka mitatu iliopita Irzak na mararafiki zake waliongana kuanzisha dhehebu hilo na wanasema hawakuona haja ya kuingiza suala la Mungu katika mradi huo.
Wafuasi wa ''dhehebu''hilo la kutunza mazingira hukutana mara kwa mara kusherhekea siku kuu ya kuadhimisha ufanisi wa kazi yao.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wanaohudhuria sherehe hiyo hupanda miti badala ya kukata miti wakati wa makumbusho ya kuyeyoka kwa barafu maarufu ''Glacier Memorial Day'', huku wakishuhudia miamba ya barafu ikiyeyuka chini ya jua la California.
Huu ni mfano mzuri wa kutunza mazingira kupitia matukio yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa- lakini wanaojiunga na vugu vugu hili wanastahili kuhamasishwa kuhusu umuhimu wake.
"Tunatumai kuwa watu watapata thamani ya kuhifadhi mazingira ili kujilinda dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi," anasema badala ya kulalamika mazingira yalivyochafuliwa.
Hivi karibuni watafiti waliangazia tamaduni zingine ulimwenguni ikiwa ni pamoja na sherhe za kidini zinazofanywa katika maeneo ya Mashariki ya Kati na sehemu za Kati za Bara Asia.
Waligundua utamaduni wa kutupa vitu kwenye moto na kisha kuruka moto h uo kama sehemu ya kujitakasa imekua ikiendelea.
Utamaduni huo huenda ilitarajiwa kuendelea kwa maelfu ya miaka ijayo sababu utamaduni huo bado unatekelezwa kila mwaka mpya wa Nowruz na waumini wa dini ya jadi Zoroaste nchini ya Iran.
Huenda ni kweli dini zisitoweke lakini tatizo ni madhehebu ya kidini yanayoibuka huenda hayana mashiko kama tunavyofikiria.
Lakini wadadisi wa masuala ya kidini wanasema madhehebu mengine makubwa yataendelewa kuanzishwa.













