Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 01.09.2019:Neymar, Eriksen, Pogba, Sane, De Gea, Foden na Hernandez

ney

Chanzo cha picha, Getty Images

Mpango wa Neymar kurudi Barcelona umepiga mwamba baada ya mshambuliaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 27 ameamua kubaki kwa mabingwa wa ligue 1 Paris St- German.(Sun)

Matokeo yake kiungo wa Denmark mwenye miaka 27 ,Christian Eriksen aliyetaka kutoka Tottenham kwa paundi milioni 72 kwenda PSG imeshindikana.(Football.London)

erik

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati huo huo uhamisho wa kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen wa dau la Pauni milioni 72 kujiunga na PSG umeshindikana.(Express)

Lakini Eriksen bado ana nafasi ya kuondoka Spurs, Juventus wakijaribu kumyakua dakika za mwishoni.(Express)

Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 27

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 27

Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 27 anaweza kukataa kusaini mkataba mpya na Manchester United ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kusajiliwa Real Madrid. (Mirror)

Ingawa meneja wa Unites Ole Gunnar Solskjaer amedai kuwa Pogba atasalia Old Trafford.(Express)

Bayern Munich inataka kumsaini winga wa Mancity Leroy Sane licha ya kwamba winga huyo mwenye umri wa miaka 23 atauguza jeraha la muda mrefu(Mirror)

Manchester United inawania kumuuza golikipa wake David de Gea mwenye umri wa miaka 29, na kusajili golikipa mpya mwezi januari . (Sun)

Rangers na Roma wanawania kumsajili kwa mkopo kiungo wa Manchester City Phil Foden, 19(Mirror)

Mamia ya mashabiki wa klabu ya Butty watahudhuria mechi itakayochezwa katika uwanja wa Gigg lane siku ya jumamosi baada ya kupigwa marufuku.

avier Hernandez

Mshambuliaji wa West Ham na Javier Hernandez, 31, ametuma maombi yake ya kuhamia Sevilla.(Mail)

Alexis Sanchez, 30,amejiunga na Inter Milan katika mkataba wa muda mrefu wa mkopo baada ya meneja wa Manchester United, Solskjae kumwambia kuwa mchezaji huyo anaweza kuchezea mashindano ya vikombe na ligi ya ulaya.(Sun)

Meneja wa Ranger Steven Gerrard amekata tamaa kumsajiri Ryan Kent, 22, kutoka klabu yake ya zamani ya Liverpool. (Express)

Mshambuliaji wa inter Milan Mauro icardi 26 ametishia kuishtaki klabu hiyo ya ligi ya serie A kwa kuwa mchezaji kiungo wa Argentina hana raha kuondolewa katika kikosi cha Kwanza cha timu hiyo.

Kiungo wa kati Ureno, Bruno Fernandes mwenye umri wa miaka 24 ,amekubali kuhamia Tottenham kutoka klabu ya sporting lisbon lakini klabu hiyo ya ligi ya uhispania imezuia uhamisho huo.

Mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala, 25, hataondoka klabu hiyo kabla ya dirisha la jumatatu halijafungwa, mwenyekiti wa klabu alisema.(Goal)

Golikipa wa Hispania Sergio Rico, 25, yuko mbioni kutoka Sevilla kuhamia Paris St-Germain .(Le Parisien)

Klabu ya ujerumani ya Borrusia Dortmund ndio klabu ya hivi karibuni kuonyesha hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Bobby Dancun 18 huku klabu hiyo ya bundesliga ikifikiria kuwasajili wachezaji zaidi wa Uingereza pamoja Jadon sancho

Tetesi Bora Jumamosi

Mshambuliaji wa Ivory Coast forward,Wilfried Zaha

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mshambuliaji wa Ivory Coast forward,Wilfried Zaha

Mwenyekiti wa Crystal Palace Steve Parish amesema atamruhusu mshambuliaji wa Ivory Coast forward Wilfried Zaha, 26, kuondoka klabu hiyo msimu ujao wa uhamisho wa wachezaji- ikiwa dau lililotangazwa na Arsenal na Everton litafikiwa. (Daily Mail)

Parma wamekubali mpango wa kumsajili beki wa Manchester United Matteo Darmian kw euro milioni 1.4 (Sky Sports)

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amekasirishwa na hatua ya viongozi wakuu wa klabu hiyo kushindwa kumsajili Paul Pogba,26, kutoka Manchester United. (Sports)

Neymar ameifahamisha Paris St- Germain kuwa yuko tayari kurudi chini na kuboresha uhusiano wao endapo atakosa nafasi ya kuhamia Barcelona ama Real Madrid kabla dirisha la uhamisho wa wachezaji Ulaya kufungwa msimu huu.( Independent)

Neymar, nyota wa soka wa kimataifa wa Brazil

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Neymar, nyota wa soka wa kimataifa wa Brazil

Huku hayo yakijiri, mkurugenzi wa kiufundi wa Paris St-Germain Leonardo amesema mabingwa hao wa Ufaransa hawajakaribia kufikia makubaliano na Barcelona kumhusu Neymar. (Marca)

Meneja wa klabu ya Barcelona Ernesto Valverde amesema kuwa amechoshwa na mashauriano yanayozunguka uhamisho wa Neymar kuja klabu hiyo (Standard)

Mkufunzi wa Arsenal Unai Emery amesema kuwa mlango upo wazi kwa kiungo wa kati wa klabu hiyo Mesut Ozil kurejesha hadhi ya mchezaji nyota wa Gunners.(Mirror)

Paris St-Germain wamewatambua wachezaji kiungo wa kati wa Tottenham Christian Ericksen 27, na mshambuliaji wa Juventus Paulo Dybala,35,kama wachezaji wawil8 watakao chukua nasi ya Neyma endapo atahamia Barcelona (Le Parisien kwa kifaransa)

Atletic Madrid wanatafakari uwezekano wa kusajili kwa mkopo mshambuliaji wa Inter Milan Mauro Icadi na baadae kumnunua kwa euro milioni 70 (ESPN)

Real Madrid imekubali kuiuzia Paris St-Germain kipa wake Keylon Navas,32, ikiwa klabu hiyo itakubali kumuachilia Alphonse Riola kujiunga nao kwa mkopo (Star)

Mshambuliaji wa zamani wa Tottenham Fernando Llorente,34, amekubalia kutia saini mkataba wa miaka miwili na Napoli inayoshiriki Ligi Kuu ya Italia, Serie A (Sky Sports)

Kiungo wa Kati wa Sportings Bruno Fernandes aliyehusishwa na tetesi za uhamisho kwenda Manchester United na Tottenham msimu wa joto hatimae ametua Real Madrid baada ya kutiavsaini mkataba wa euro milioni 63 (Mail)