Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je ni kweli Jumatatu ni siku ''isiyofurahisha''?
- Author, Na Dinah Gahamanyi
- Nafasi, BBC News Swahili
- Muda wa kusoma: Dakika 4
Jumatatu ni siku ya kwanza ya mwanzo wa wiki na mara nyingi siku hii imekuwa ni adui wa wengi ambaye hazungumziwi hususan baada ya wengi kufurahi na kujivinjari katika siku zao za wikendi
Hata hivyo katika enzi hii ya mitandao ya kijamii wengi wamekuwa wakipeleka hisia zao juu ya siku ya Jumatatu kwenye mitandao ya kijamii chini ya #MondayBlues...ikimaanisha #Huzuni ya Jumatatu na #MondayMotivation, ikimaanisha #MotishaJumatatu na Hashtag hizi hujitokeza kila Jumatatu.
Ni ukweli kwamba hatuwezi kuiepuka siku ya Jumatatu miongoni mwa siku za wiki, watu wanahitaji kuamka mapema kutoka kwenye vitanda vyao na kujikokota na kuanza kazi zao za siku.
Jumatatu asubuhi huwa ni kipindi ambacho hakipendwi zaidi na wengi, kwani ni ishara ya mwanzo mpya wa kazi ya wiki na kwamba lazima tuseme kwa heri raha na mapumziko ya Jumamosi na Jumapili.
Mfano kupitia #Huzuni ya Jumatatu Naina kwenye ukurasa wake wa Twitter ameonyesha hisia alizokuwa Jumatatu akiendesha gari kuelekea kazini:
Sherry Al Khanjir pia ni mmoja watu wanaopata hisia ya huzuni kila inapofika siku ya Jumatatu, na kupitia #MondayBlues ama #Huzuni ya Jumatatu ameonyesha hali yake kupitia picha hii kwenye twitter
Sijui utakubaliana nae au la, Peace Pill yeye anasema inafaa hali ya huzuni ya Jumatatu alikabiliana na kinywaji hiki baridi kinachoitwa Kokum Kolsch!:
Kupitia #MotishaJumatatu watumiaji wa mtandao wamekuwa wakijaribu kupeana ujumbe wa motisha juu ya mtizamo ambao mtu anaopaswa kuwa nao kuihusu siku ya kazi ya Jumatatu.
kawangware Finest TM kwenye ukurasa wake wa Twitter kupitia #MondayMotivation ama #MotishaJumatatu anashauri kwa hali yoyote uliyonayo chaguo liwe ni furaha. Akielezea hisoa hizo kupitia video hii:
Klabu ya Arsenal pia haikubaki nyuma kutoa motisha kwa wachezaji wake kupitia Hashtaginayotoa Motisha kwa siku ya na mashabiki ikisema Wiki mpya imeanza - na tunahesabu siku kuelekea mechi ya kaskazini mwa London
Wanasaikolojia wanasema nini juu ya hali hii?
Wanasaikolojiwa wa masuala ya kijamii wanashauri kuwa usikubali hali hii inayokukera kuhusishwa na Jumatatu.
Wanasema siku za Jumatatu zinapaswa kukaribishwa kwa shauku kubwa , matumaini na nguvu za kutosha.
Mwanasaikolojia Rosemary Nyambura kutoka Kenya anasema hisia za mchoko unapoanza siku ya kazi ya Jumatatu zinategemea ni kazi gani unayoifanya jumatatu: ''Ni maumbile ya kawaida ya mwili wa binadamu kutaka kuendelea kufanya kile ambacho umekuw a ukikifanya kwamuda, mfanyo kama umekuwa katika hali ya sherehe, kunywa pombe au hata kupumzika wakati wa wikendi basi mwili utataka uwe na mwendelezo huo huo'', anasema na kuongeza kuwa mwili huwa hautaki mabadiliko.
Bi Nyambura anasema kila binadamu hukosa nguvu za kukabiliana na msukumo asilia wa mwili wa binadamu unaomtaka aendelee na maisha ambayo amekuwa nayo kwa kipindi fulani kikiwemo kipindi cha mwishoni mwa juma ambacho watu huingia katika utaratibu tofauti na maisha yao ya kikazi na badala yake kupumzika.
''Hali hii inatuathiri kama binadamu hasa kwa wale wanaofanya kazi kwasababu ukiwa na hali ya muendelezo wa maisha ya wikendi huwezi kufanya kazi ipasavyo kama inavyotakiwa , kwasababu huajaondoka kutoka maisha ya wikendi , ndio maana utakuta baadhi ya watu Jumatatu hawatimizi malengo ya majukumu yao na hivyo kukosana na waajiri ama viongozi wao, anasema mwanasaikolojia Rosemary Nyambura.
Kulingana na Bi Nyambujra hali hii huwafanya baadhi ya watu kuwa wakimya na kutokuwa na mawasiliano mazuri na wafanyakazi wenzao siku za Jumatatu na hali hii kupungua katika siku nyingine za juma.
Unaweza vipi kuepukana na hali ya kujiskia mchovu Jumatatu?
- Kulingana na Mwanasaikolojia Rosemary Nyambura, watu waepuke kufanya mambo kupita kiasi siku za wikendi mfanyo kunywa pombe kupindukia na kuzurura kupindukia
- Anashauri kila tunachokifanya basi kiwe ni kwa kiasi ili kuepuka kuuchosha mwili.
- Watu wawe na matarajio ya mambo wanayopanga kuyafanya Jumatatu na wiki nzima inayokuja na wapange jinsi ya kuyatekeleza.
- Badala ya kulala na kukaa tu ndani ya nyumba zetu, tufanye mambo tunayoyapenda kwa kiasi, tuepuke pia kulala kupita kiasi kulala tu, kupanga muda wakati wa wikendi.
- Tubadili mtizamo kuihusu siku ya Jumatatu, tutambue kuwa Jumatatu ni siku tu kama siku nyingine za wiki.
- fanya kitu una
- Tufikirie juu ya matarajio tunayoweza kuyapata kuanzia Jumatatu kwasababu Jumatatu ni siku ya kwanza ya wiki.