Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Jinsi umasikini unavyochochea mimba za utotoni DRC
Kiwango cha wasichana wanaojifungua mapema kimeongezaka Jijini Kinshasa hususani katika mitaa ya mabanda, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na mashirika yasiokuwa ya kiserikali.
Hali hiyo, kwa mujibu wa mashirika hayo imesababiswa na ukosefu wa elimu sahihi na uhamasishaji kuhusu ngono kwa wasichana wanaovunja ungo, pamoja na kwa kiasi kikubwa umaskini wa wazazi.
Mwandishi wa BBC jijini Kinshasa, Mbelechi Msoshi ametembelea Kinseso, miongini mwa maeneo masikini zaidi ya Kinshasa, na kukutana na baadhi ya wasichana ambao walizaa wakiwa na umri wa chini ya miaka 18.
Wasichana hao waliangua kicheko kusikia shirika lisiokuwa la kiserikali maarufu Foundation KENGE, linazunguza nao kuhusu matumizi ya mipira ya kondomo kama njia ya kujikinga mangojwa ya zinaa na kuepuka kuzaa mapema.
Kicheko kililipuka kwa sababu ni swala la aibu eneo hilo.
Georgettte ana miaka 16, lakini ana mtoto wa miaka miwlili sasa, alipata ujauzito siku chache baada ya kupata hedhi kwa mara ya kwanza.
"Nilizaa nikiwa mtoto, mwili wangu ulipokuwa unahitaji mwanaume nikiwa na umri mdogo, nilikuwa sijaelimishwa kuhusu ushiriki wa ngono ya mapema, lakini hivi nimefundishwa nimekuwa makini, nitazaa mtoto mwingine wakati maisha yangu yakiwa mazuri," aneleza Georgette.
Kwa mujibu wa Borah Kenge, ambaye ni mratibu wa shirika hilo ambalo kwa sasa linaanza uhamasishaji katika eneo hili maskini, umefika wakati sasa kwa mashirika yote yasiyo ya kiserikali kulivalia njuga suala hilo kwa pamoja.
"Vijana wote wanahitaji ushauri kuhusu ngono, kama sisi tunashindwa kujibu mahitaji na maswali yao kuhusu shughuli za ngono; tutakuwa na vijana ambao wanazaa kiholela na kutoa mimba, na takwimu za maafa zitaongezeka."
Hali hio pia imesababishwa na umaski, Helene ni mama mzazi wa Georgette: "Hapa hakuna shuguli zingine kama sio za ngono, utaona msichana wa miaka 10 tayari ameshaanza kufanya mapenzi. Hata kondomu hawataki kutumia. Kwasababu tu yule kijana alimpa samaki na mkate, basi anakubali na mimba inaingia, kulingana na umaskini wa sisi wazazi wao, nadhani ni vema kuangalia namna gani ya kuwafungulia vituo vyamafunzo ili wawe na kazi fulani ambayo itawasadia kimaisha."
Masina Ngango, kiongozi wa shirika litwalo muungano kwa ajili ya maendeleo ya Kisnseso , kuna zaidi ya wasichana 2,000 ambao walizaa kabla ya miaka 18.
"Kweli kuna wazazi ambao hawana ajira, sisi upande wetu tulijaribu kufungua vituo vya mafunzo kwa ajili ya wasichana hawa, nilikuwa nadhani nitapokea tu wasichana 20 ambao walizaa wakiwa na umri mdogo. Nikapokea wasichana zaidi ya 100, na hapo sikuwa na jinsi ya kuendesha shughuli hiyo, nikafunga kituo."