Marekani na Uchina mezani kutanzua mzozo wa kibiashara

Rais Donald Trump amesema kuwa Marekani na Uchina zitafufua mazungumzo "muda mfupi sana ujao "baada ya kuongezeka zaidi kwa uhasama wa kibiashara na utawala wa Beijing mwishoni mwa Juma.

"China iliniita jana usiku ...Ikasema turejee tena kwenye meza ya mazungumzo . Kwa hiyo tutarejea tena mezaji ," amesema .

Ijumaa Bwana Trump alipandisha juu viwango vya ushuru kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka Uchina zenye thamani ya mamilioni ya dola. Uchina haijatoa kauli yoyote, lakini awali ilitoa wito wa kuwepo kwa "utulivu " katika kutatua mzozo huo wa kibiashara.

Bwana Trump salituma jumbe zenye utata mwishoni mwa juma , kwanza akielezea kusikitishwa na viwango vipya vya ushuru vilivyowekwa na Uchina kwa Marekani, lakini baadae ujumbe huo ukatolewa na White House Jumapili.

Hata hivyo katika kikao cha mataifa yenye utajiri zaidi wa kiviwanda G7 mjini Biarritz Jumatatu alisema kuwa maafisa wa Uchina wamepiga simu mbili "Nzuri , tena nzuri sana " Jumapili usiku na kwamba Beijing ilitaka "kufanya mkataba".

Athari za mzozo wa kibiashara

Jumatatu masoko ya hisa ya Asia yalishuka kuytokana na hofu juu ya vita vya biashara , huku soko la Hong Kong la Hang Seng index likipoteza zaidi ya 3% ya hisa zake kabla ya kuanza kupanda tena baada ya taarifa za kufufuliw akwa mazungumzo.

Hata hivyo hisa katika masoko ya Ulaya zlifanya vizuri baada ya Trump, kutoa ujumbe wa maridhiniano ya kibiashara na Uchina.

Muda mfupi uliopita hisa katika soko la hisa la Ujerumani Dax zilipanda kwa 0.2% huku la Ufaransa Cac 40 likiimarika kwa 0.6% . Katika soko la London FTSE 100 lilifungwa kwa ajili ya siku ya mapumziko ya Bank Jumatatu.

Ni vipi vita vya biashara viliongezeka?

Rais Trump ameahidi ku jibu hatua ya Uchina ya kutangaza mipango ya kuweka ushuru wa 10% kwa bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 75 zinazoagizwa kutoka Marekani.

Ushuru mpya unalenga kujibu mipango aliyoichukua mwenyewe Trump ya kutoza asilimia 10% kwa mauzo ya bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 300 za Uchina

Hisa katika soko la hisa la Wall Street zilishuka baada ya rais Trump kutuma ujumbe wa twitter kwamba atajibu kuhusu ushuru mpya baadae Ijumaa.

Alisisitiza kuwa atatafuta mbadala wa soko la Uchina na kurejesha uzalishaji Marekani.

"Makampuni yetu bora ya Kimarekani yanaagizwa kuanza kutafuta maeneo mbadala ya uzalishaji unafanyika nchini Uchina mara moja , ikiwemo kuyaleta makampuni yenu nyumbani na kufanya uzalishaji wa bishaa nchini Marekani ," ali tweet . "Nitajibu kuhusu ushuru wa uchina mchana huu ."

Ushuru mpya wa Uchina kwa bidhaa kutoka Marekani utakuwa ni kati ya 5% 10% na utatozwa kw abidhaa zaidi ya 5,000 zinazotoka Marekani.

Bidhaa za kilimo, mafuta ghafi, na ndege ndogo ni miongoni mwa bidhaa nyingine zilizolengwa.

Beijing pia itaangalia upya 25% ya ushuru kwa magari ya Marekani inayoagiza ambao uliondolewa mapema mwaka 2019 kama ishara ya urafiki wakati nchi mbili zilipojaribu kujadili makubaliano ya kibiashara.

Marekani inajaribu kuilazimisha Uchina kufanya mageuzi ya namna inavyofanya biashara, ikidai kuwa viwanda vya Marekani inapata hasara kutokana na masuala kama wizi wa haki miliki ya akili

Hata hivyo ,washirika wa marekani wamemshinikiza Bwana Trump katika kikao cha G7 nchini Ufaransa , wakionya kuwa vita vya bishara vinatishia uchumi wa dunia.

Katika ujumbe wake wa Twitter Bwana Trump alisema kuwa anapanga kuyaamrisha makampuni ya Marekani yanayofanyia kazi nchini Uchina kuhamishia shughuli zao nyumbani Marekani , ingawa haiko wazi ni vipi anaweza kuyalazimisha kuheshimu amri yake hiyo.

Hatua hii inakuja baada ya Uchina kujibu vita hivyo vya biashara, na kutangaza mipango yake ya kupandisha ushuru wa bidhaa za Marekani inazoagiza zenye thamani ya dola bilioni 75.

Ni vipi hali hii imefikia hapa?

Mataifa hayo makubwa zaidi kiuchumi duniani yamekuwa katika vita vya kibishara kwa kipindi cha mwkaa mzima uliopita vilivyosababisha mataifa hayo mawili kupandishia ushuru wa bidhaa zenye thamani ya mabilioni ya dola.

Bwana Trump kwa muda mrefu amekuwa akiishutumu Uchina kwa kutoitendea haki Marekani katika biashara baina ya nchi hizo mbili , lakini nchini Uchina mtazamo ni kwamba Marekani inajaribu kuzuwia kupanda kwa uchumi wa Uchina.

Kushuka kwa thamani ya sarafu ya uchinai -yuan mapema mwezi huu kulisababisha Marekani kuoitaja rasmi Uchina kama taifa linalofanyia "mizengwe sarafu yake ", jambo liliochochea uhasama uliopo baina ya nchi hizo mbili.