Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ndege ya Urusi iliogongana na kundi la ndege: Marubani wazungumzia wakati mgumu waliokuwa nao
Maruubani wa ndege ya Urusi ilioanguka bila ya abiria 233 kujeruhiwa katika shamba la mahindi wamepongezwa kwa kuwa mashujaa.
Ndege hiyo ya A321 ilikuwa iko angani baada ya kuondoka katika uwanja wa ndege wa Moscow wa Zhukovsky wakati kundi la ndege lilipoingia katika injini yake na kusababisha mitambo yote miwili kufeli.
Warusi wanalifananisha tukio hilo na miujiza ya Hudson, shambulio la ndege ambalo karibu lisababishe ajali kubwa ya ndege mjini New York mwaka 2009 lakini tukio hilo likawa la kufurahisha baada ya rubani kuishukisha ndege hiyo salama salmin
Je ni nini kilichofanyika na ndege hiyo?
Ndege hiyo ya Ural Airlines Airbus 321 ilikuwa ikisafiri kuelekea katika eneo la Simferopol Crimea ilipogonga kundi la ndege muda mfupi baada ya kuondoka uwanjani , hali iliyovuruga utendaji wa injini yake.
Vyombo vya habari vya taifa la Urusi vimetaja kutua kwa ndege hiyo kama "muujiza wa eneo la Ramensk".
Ilikuwa safari ya kawaida kutoka Moscow kuelekea Simferopol mjini Crimea ikiwa na abiria 226 wengi wakielekea katika likizo.
Ndege hiyo ilikuwa inapanda angani wakati injini ya kwanza ilipofeli huku nyengine ikishindwa kufanya kazi. Baada ya injini moja kutatizika walidhania kwamba wangerudi katika uwanja wa ndege, alisema rubani Yusupov.
''Tulipogundua kwamba injini ya pili pia ilikuwa ikipoteza umeme licha ya juhudi zetu zote ndege hiyo ilianza kushuka'', alisema.
''Nilibadilisha mafikira yangu mara kadhaa , kwa sababu nilitaka kupaa'', alisema.
Lakini rada ya ndege ilionyesha kwamba ndege hiyo ilikuwa imepaa urefu wa mita 243.
''Nilipanga kupaa urefu fulani , lakini nikafikiria kuhusu kufeli kwa injini , nikaamua kufanya uamuzi wa busara. Lakini nikabaini nina wakatu mgumu''.
Nahodha Yusupov na mwenzake Georgi Murzin, walifanikiwa kuzuia usambazaji wa mafuta kwenda katika injini na kuifanya ndege hiyo kuwa sawa angani na kuishukisha chini katika shamba la mahindi.
Baada ya matairi ya ndege hiyo kushuka kulikuwa na hatari ya vifaa vilivyokuwa vikiruka chini ya ndege hiyo kupasua tangi la mafuta la ndege hiyo .
Anasema kwamba alikuwa amejifunza kutua kwa dharura akifanyia kazi kampuni ya ndege ya Ural Airlines.
''Sihisi kama shujaa'' , alisema. ''Nilifanya nilichofanya , kuiokoa ndege , abiria na wafanyakazi''.
Yuri Sytnik, mmojawapo ya marubani wazuri nchini Urusi aliambia chombo cha habari cha Komsomolskya Pravda kwamba wafanyakazi walifanya kila kitu .
''Walifunga injini za ndege hiyo, na kuishukisha ndege hiyo kwa utulivu , huku ikishuka na eneo la mkia kama invyohitajika, kupunguza kasi- ulikuwa wakati mgumu huwezi kuangukia pua usikubali injini igonge ardhi kwa kishindo''.
Ndege hiyo ilikuwa na abiria 233 na wahudumu ndani yake wakati ndege waliporipotiwa kuingia ndani ya injini na rubani wake akaamua kutua mara moja.
Abiria mmoja ambaye hakutajwa jina lake ameiambia televisheni ya taifa kuwa ndege ilianza kuyumba kwa hali isiyo ya kawaida baada ya kuondoka uwanjani.
"Sekunde tano baadae, taa za upande wa kulia za ndege zikaanza kuwaka na kuzima na kulikuwa na harufu ya kuungua. halafu tukatua na kila mtu akatimua mbio kwenda mbali ," alisema.