Mkataba wa Kinyuklia wa Iran upo katika hali mahututi - Je unaweza kuokolewa?

Chanzo cha picha, EPA
Imechukua takriban mwaka mmoja tangu serikali ya Trump kujiondoa katika mkataba wa kinyuklia wa Iran kwa jina JCPOA'.
Uamuzi wa Iran wa kukiuka kiwango cha kilo 300 cha uzalishaji wa madini ya Uranium ni mojawapo ya vitu ambavyo inatishia kufanya, hatahivyo Tehran inasisitiza kuwa haitaki kukiuka makubaliano ya mkataba huo .
Inataka kuangaziwa sawa chini ya masharti yake.Iran inasisitiza kuwa muda wote huo imeafikia masharti ya mktaba huo. Na tabia hiyo nzuri ya Iran imethibitishwa na shirika la kinyuklia duniani IAEA.
Lakini sasa Iran inasema imetosha. Imejaribu kuzingatia masharti iliowekewa lakini Marekani haikujiondoa tu pekee bali pia imeiwekea vikwazo na kujaribu kulifanya taifa hilo kuwa vigumu kwa taifa jingine lolote kushirikiana nalo kibiashara.
Sera hiyo ya kuiwekea shinikizo kali Iran inatambulika sawa na utawala wa rais Donald Trump.
Lengo lake, msemaji wake anasisitiza ni kuilazimu Iran kurudi katika meza ya mazungumzo ili kujadiliana kile ambacho Marekani inasema ni ''mkataba nzuri''.
Lakini wakosoaji wa rais Trump wanahoji kwamba kile ambacho utawala wake unataka ni kuonyesha ubepari badala ya majadiliano.
Kuna maono ya kutaka kuubadilisha utawala wa Iran miongoni mwa washauri wa rais Trump.

Athari za kuishinikiza Iran ni kubwa
Iran-inapokubali kwamba ndio iliotekeleza mashambulizi ya hivi karibuni katiika Ghuba kama vile Marekani inavyosisitiza- tayari ni wazi kwamba imekataa kusukumwa na Marekani.
Na ina njia nyingi za kupinga shinikizo kama hizo. Hofu ni kwamba iwapo makubaliano hayo ya mpango wa kinyuklia wa Iran yatatupiliwa mbali yatalifanya taifa hilo kurudia kuunda silaha za kinyuklia mbali na kuhatarisha vita katika eneo la Ghuba kwa kukusudia ama kwa njia nyengine.
Hivyobasi athari za mpango wa kinyuklia wa Iran ni kubwa.Hatua hiyo zitayalazimu mataifa mengi zaidi kujibu kile kinachoendelea.
Tayari kuna tofauti kati ya Washington na washirika wake wa Ulaya-Uingereza, Ufaransa, Ujerumani ambao bado wanaendelea kuunga mkono mkataba huo wa kinyuklia na wanataka uendelee kuheshimiwa.
Ni kweli kwamba washirika hao wa Ulaya wana wasiwasi kuhusu vitendo vingi vya Iran katika eneo hilo mbali na kukubaliana na utawala wa Trump kuhusu mpango wa silaha wa Iran.
Lakini wanaamini kwamba mkataba huo , licha ya kuwa na kasoro una faida fulani.
Ulifutilia mbali swala la utengenezaji wa silaha za kinyuklia hadi siku za usoni.
Haukutatua mgogoro kuhusu vitendo vya zamani vya Iran lakini ulizuia mgogoro.
Kumbuka kwamba kabla ya mkataba huo kuafikiwa 2015 kulikuwa na hofu kuhusu ya shambulio la miundombinu ya Iran kutoka kwa Israel ama Marekani.

Chanzo cha picha, EPA
Sasa itakuwaje?
Iran inawasilisha hoja. Inasema kuwa ukiukaji wa kiwango cha uzalishaji wa madini ya Uranium yanayotumika kuunda silaha za kinyuklia sio kinyume na mkataba wa JCPOA.
Katika makubaliano hayo-Iran imesisitiza kuwepo kwa maneno kwamba iwapo wengine watakiuka maamuzi yake bado Iran pia haina budi kukiuka. Hilo hatahivyo sio vile linavyochukuliwa na waliotia sahihi mktaba huo.
Wanaweza kuhoji kwamba unaweza kuwepo ama kutokuwepo kabisa katika makubaliano hayo - kama ilivyofanya Marekani.
Shinikizo ya kimkakati ya Iran inalenga kuyasukuma mataifa ya Ulaya kupunguza athari za vikwazo vya Marekani dhidi yake.
Muungano wa Ulaya tayari umezindua mfumo wa malipo kwa jina INSTEX - ili kujaribu kusaidia biashara ya mahitaji ya kibinaadamu ambayo, imekuwa vigumu kutekelezwa kutokana na hatua ya benki nyingi kukwepa vikwazo vya Marekani.
Lakini INSTEX haitasaidia katika sekta muhimu za uchumi wa Iran ambazo zinaathirika pakubwa , kama vile sekta ya mafuta.
Urusi na China pia hazipendelei uamuzi huo wa Marekani na wangependelea mkataba huo wa Kinyuklia kusalia.
Hivyobasi Marekani haina marafiki zaidi ya Saudia na Israel, mataifa ambayo yana uhasama na Iran.

Chanzo cha picha, AFP
Tatizo jingine linaweza kujitokeza chini ya wiki moja wakati Iran itakapotishia kuchukua hatua zaidi ili kukiuka makubaliano ya mkataba huo.
Imedaiwa kwamba mojawapo ya hatua hizo ni kuongeza uzalishaji wa madini ya uranium kutoka asilimia 3.6 hadi 20. Madini hayo hutumika katika utengenezaji wa silaha za kinyuklia.
Unapoongeza uzalishaji wa madini hayo hadi kufikia asilimia 20 utakuwa umefikia asilimia 90 ya vifaa vinavyotumika kutengeneza bomu.
Kuna mambo mengine ambayo Iran inaweza kufanya lakini uzalishaji wa madini hayo hadi asilimia 20 utatoa vitisho kwa dunia nzima na itakuwa vigumu kwa muungano wa Ulaya kuendelea kuunga mkono mkataba huo.
Mgogoro nchini Syria pia ni swala jingine. Israel imehusika katika kampeni za kushambulia kambi za majeshi ya Iran nchini humo hususan katika miji ya Homs and Damascus.
Chochote kitakachofanyika kimakosa , ama ongezeko lolote la wasiwasi linaweza kuzua mjadala mwengine kuhusu silaha za kinyuklia, Iran inaamini kwamba shinikizo inaweza kuondolewa kwa njia moja ama nynegine - lakini sivyo.
Rais Trump anajaribu uwezo wake kuhakikisha kuwa mkataba huo unaangamia.
Mkataba huo wa Iran unakabiliwa na changomoto kali na hatua itakayochukuliwa na Iran katika kipindi cha wiki moja ijayo inaweza kuamua hatma yake.













