Je ni kweli uchaguzi wa Marekani ndio uliomzuia Trump kuishambulia Iran?

Chanzo cha picha, Getty Images
Je rais Donald Trump amekuwa akikosa msimamo mara kwa mara wakati anapokabiliana na Iran?
Hivi ndivyo seneta mmoja wa chama cha Democrat Tammy Duckworth , alitaja misimamo kuhusu operesheni zake .
''Anahatarisha taifa letu na usalama wetu wa kitaifa''.
Ukweli ni kwamba Trump hakuwashauri viongozi wa bunge la Marekani iwapo alipaswa kujibu mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya Iran baada ya taifa hilo kuitungua ndege isio kuwa na rubani ya Marekani wiki iliopita.
Alipata ushauri mzuri kutoka pande zote mbili huku mbunge wa chama cha Republican Michael Mccaul ambaye alikuwepo akielezea mkakati wa Marekani kuwa wa kivita.

Chanzo cha picha, Getty Images
Rais huyo pia alipata ushauri kutoka kwa majenerali wake wa jeshi pamoja na mshauri wake mkuu kuhsu maswala ya usalama wa kitaifa.
Na kulingana na gazeti la The New York Times pia alipata ushauri kutoka kwa mtangazajii ,mmoja katika runinga ya Fox News.
Iwapo Trump angeanza vita dhidi ya Iran pengine huenda ndio ingekuwa mara yake ya mwisho kushikilia wadhfa wa urais nchini humo.
Je hiyo ndio sauti iliomrai Trump kusitisha mashambulizi hayo? nani anayejua?

Chanzo cha picha, Getty Images
Bwana Trump alisema kuwa wasiwasi wake mkubwa ulikuwa idadi ya watu ambao wangefariki kutokana na shambulio la Marekani.
Lakini zaidi ya swala jingine lolote la usalama wa kitaifa, swala hili limemfungua rais Trump na mapenzi yake ya kutaka kuonekana mkali mbali na kusita kujihusisha na vita vya ugenini ,
Aliwaaahidi kwamba hatopigana.
Lakini huku akisherehekea kujizuia kwake , na hata kufutilia mbali vitendo vya Iran amekuwa akituma barua za kutumia nguvu iwapo zitahitajika ili kujibu mashambulizi ya Iran iwapo itashambulia.
Kwa ufupi kumekuwa na kiwango cha Trump kurudi nyuma ama kubadili misimamo

Chanzo cha picha, Getty Images
Lakini swala jingine kuhusu ishara hizi kuhusu sera ya Iran: Mshauri wa kitaifa wa bwana Trump John Bolton na waziri wa maswala ya kigeni Mike Pompeo wanaonekana kuwa na ajenda tofauti na yake.
Rais Trump huzungumzia sana kuhusu mpango wa kinyuklia wa Iran ambao alijiondoa , kuhusu vile ulivyokuwa mbaya na mdhoofu , vile mtangulizi wake Barak Obama alishindwa kujadiliana kuhusu mkataba huo na kuamua Iran kuwa mshindi.
Pia amekuwa akitangaza mara kwa mara vile anavyoweza kufanya majadiliano ya mkataba huo yatakayoipatia ushindi Marekani.
Ameitaka Iran kumpigia simu na hata kutoa nambari yake ya simu kupitia mpatanishi.
Huo sio msimamo tunaopata kutoka kwa wizara ya maswala ya kigeni ya Marekani.

Chanzo cha picha, Getty Images
Bwana Pompeo huzungumzia kuhusu majadiliano, lakini zaidi yeye husisitiza Iran kuwekewa shinikizo zaidi : Vikwazo vya mafuta na vile vya kifedha vinvyoathiri taifa hilo kiuchumi.
Tofauti kati ya utawala huu na uliopita ni sawa na usiku na mchana ambapo siki za nyuma wakati wnahabari wetu walikuwa wakiangazia mkakati wa kuondoa vikwazo kupitia kuifanya Iran kukubali viwango vya mpango wake wa kinyuklia .
Mara ya kwanza zilikuwa habari njema kumuona waziri wa maswala kigeni wa Marekani John Kerry na mwenzake wa kigeni kutoka Iran Javad Zarif hadi likawa jambo la kawaida.
Bwana Pompeo pia anasisitiza kuwa vikwazo hivvo vitasalia hadi pale Iran itakapokubali kuafikia masharti12.
Masharti hayo yanashirikisha makubaliano ya kinyuklia na maswala mengine kama vile kupunguza mpango wake wa kutengeza silaha mbali na kuondoa ushawishi miongoni mwa vikosi vya wapiganaji inaowaunga mkono katika eneo hilo.

Waziri wa maswala ya kigeni ametaja hatua hiyo kama kujaribu kuilazimu Iran kubadili tabai zake, ili kuendeshwa kama taifa jingine la kawaida.,
Wakati huohuo amekiri kwamba haamini kwamba utawala huo utabadilika ili kuafikia matakwa ya Marekani.
Amesema kuwa Iran haina viongozi wenye msimamo wa wastani, akifutilia mbali tofauti iliopo kati ya wale wenye msimamo mkali pamoja na wale wanaounga mkono ambao walihusika katika kuweka mkataba wa makubaliaino hayo ya kinyuklia.
Wakati huohuo amekiri kwamba haamini utawala huo unaweza kubadili jinsi Marekani inavyotaka.

Chanzo cha picha, Getty Images
Washirika wa Marekani na wabunge wake wanakubaliana kwamba tabia ya Iran katika eneo la mashariki ya kati ni haribifu na hatari. Na inahitaji kuzuiwa.
Lakini wakosoaji wanasema kuwa mahitaji 12 huenda yakaibadili Iran kubadili sera yake ya kigeni kwa vitu vinavyoonekana muhimu kwa usalama wake wa kitaifa.
Na hilo halitafanyika. Lengo mojawapo ya utawala huo ni kuinyima Iran mapato ya kujiimarisha katika sera yake ya kigeni kulingana na mjumbe wa Iran Brian Hook aliyeliambia bunge la Congress wiki iliopita
Lakini malengo yake ni nini haswa? Mpango mpya wa kinyuklia? ama kuubadili utawala wa taifa hilo?
Utawala huo una mpango mmoja , kuiwekea Iran shinikizo kali. Haina mkakati wa kuirudisha Iran katika meza ya majadiliano, alisema seneta Bob Menendez - kiongozi mkuu wa democratic katika bunge la seneti anayehusika na maswala ya mahusiano ya kigeni.
''Lakini mtu anapoweka shinikizo sana na akakosa njia ya kutorokea, kibofu hupasuka''.

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images
Kuna hofu kwamba rais Trump anaweza kuharibu mambo zaidi bila ya kutafuta idhini kutoka kwa bunge katika vita vyovyote vipya hatua anayopewa haki kutekeleza.
Chini ya katiba ya Marekani, bunge la Congress lina uwezo wa kuitisha vita , ndio? swali hilo liliulizwa mara kwa mara na mbunge wa Democrat Ted Lieu. Bwana Trump na Pompeo hawakujibu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Raia wengi nchini marekani sasa wanahofu kwamba mtu huyu aliyetwa rais wa ajali huenda akasababisha vita vya ajali katka eneo la mashariki ya kati.













