Mexico: Polisi waambiwa wapunguze uzani kujiunga na kikosi kipya cha ulinzi

Mexican National Guard in Chiapas State, June 2019

Chanzo cha picha, QUETZALLI BLANCO/AFP/Getty Images

Maelezo ya picha, Walinzi wa kitaifa tayari wanashika doria katika maeneo ya mpakani

Maafisa wa polisi wanaotaka kujiunga na kikosi kipya cha ulinzi wa taifa nchini Mexico wamepewa hadi miezi sita kupunguza uzani la sivyo wafutwe kazi.

Maafisa hao wamepewa agizo hilo wanapoendelea na shughuli ya kukabiliana na wahamiaji haramu.

Maafisa 625 tayari wamefeli vigezo vya kiafya vya kujiunga na kikosi hicho kitakachohudumu katika mpaka wa Kaskazini na Kusini mwa nchi hiyo kwa miezi sita au zaidi, lilisema gazeti la El Financiero katika ripoti yake.

Maafisa ambao hawatafikia vigezo hivyo watalazimika kusalia katika katia vitengo vingine vya ulinzi wa taifa lakini pia wanakabiliwa na tisho la kufutwa kazi kwasababu kuna mpango wa kuunganisha idara ya polisi na vitengo vingine vya ulinzi kufikia mwisho wa mwezi Juni.

Taarifa hiyo ilifichuka baada ya kanda ya rekodi yenye sauti ya kamanda wa polisi Raúl Ávila Ibarra, iliyovujishwa kupatikana na gazeti la El Universal,.

Katika kanda hiyo afisaa huyo wa ngazi ya juu anasikika akijaribu kuwashawishi maafisa wadogo kujiunga na na kitengo kipya cha huduma ya uhamiaji huku akiwaelezea kuwa kitengo hicho kipya kinalipa vizuri kuliko chao polisi ".

"Wengine wetu tulio na uzani mkubwa tuna hadi miezi sita kubuni mbinu ya kufukia masharti tuliyopewa," Bw. Ávila Ibarra alisikika akisema.

Mexican National Guard at border crossing, June 2019

Chanzo cha picha, Toya Sarno Jordan/Getty Images

Maelezo ya picha, Wakosoaji wanasema kikosi hicho maalum cha kukabiliana na ulinzi wa taifa kinatumiwa vibaya

El Financiero linasema kuwa maafisa wanaotoa maombi yakazi wa kitengo kipya cha ulinzi wa taifa hawatakiwi kuwa na uzani jumla wa mwili unatakiwa kuwa na BMI ya chini ya 28, hakuna kutopoa sehemu yoyote ya miwili wala kuwa na tattoos ambayo itaonekana watakapovalia sare za kazi.

Uchunguzi uliofanywa na shirika la kitaifa la takwimu na Geografia mwaka 2017 ilibaini kuwa 79 ya maafisa wa polisi walikuwa na uzani mkubwa kupita kiasi ilisema ripoti ya gazeti la Mexico News.

Lakini idara huduma ya uhamiaji haijawasaidia maafisa wengi maafisa wengi, baada ya ripoti ya Vanguardia daily kubaini kuwa baadhi ya maafisa hao wanalalamika katika mitandao ya kijamii kuwa wanafanya kazi katika mazingira magumu.

Rais Andrés Manuel López Obrador walifanikiwa kulishawishi bunge kuidhinisha kuajiriwa kwa maafisa 60,000- wa ulinzi wa kitaifa mapema mwaka huu, kama sehemu ya kutimiza ahadi yake ya uchaguzi ambapo alisema atakabiliana na uhalifu wa kupangwa na uhalifu mwingine.

Lakini wakosoaji wake wanalalamika kuwa kikosi hicho kinatumiwa kukabiliana na mzozo wa uhamiaji, huku watu katika mataifa mengine Amerika ya kati wakijaribu kuingia nchini Marekani kupitia Mixico.