Maelezo muhimu kuhusu mkataba wa nyukilia wa Iran

(From kushoto kwenda kulia) Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi, Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius, Waziri wa mambo ya nje ya Ujerumani Frank-Walter Steinmeier, mwakilishi wa umoja wa Ulaya kwa masuala ya mambo ya nje na sera za usalama Federica Mogherini, Waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif, Mkuu wa shirika la nguvu za atomiki nchini Iran Ali Akbar Salehi, Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov, Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Philip Hammond, Waziri wa mambo ya nje wa Marekani US, John Kerry na waziri wa nishati wa Marekani Ernest Moniz wakiwa kwenye picha ya pamoja mjini Vienna Austria mwaka 2015.

Chanzo cha picha, AFP

Mwaka 2015,Iran iliingia kwenye makubaliano kuhusu mradi wa nyukilia sambamba na mataifa yenye nguvu duniani-Marekani,Uingereza, Ufaransa,China,Urusi na Ujerumani.

Hatua hii ilikuja baada ya kuwepo kwa mzozo kuhusu jitihada za Iran za kutengeneza silaha za nyukilia. Iran imesisitiza kuwa mradi wa nyukilia ulikuwa wa amani, lakini Jumuia ya kimataifa haikuamini.

Ndani ya mkataba huo,Iran iliridhia kupunguza shughuli zake na kuruhusu wakaguzi wa kimataifa kukagua vinu vyake ili iweze kuondolewa vikwazo vya kiuchumi.

Kurutubisha madini ya Urani

Wafanyakazi

Chanzo cha picha, Getty Images

Hifadhi ya madini ya urani ilipunguzwa kwa asilimia 98, mpaka kilogramu 300 kiasi ambacho hakitakiwi kuongezeka mpaka mwaka 2031. madini yanayotakiwa kurutubishwa yanapaswa kuwa asilimia 3.67.

Mwezi Januari mwaka 2016, Iran ilipunguza uzalishaji kwenye vinu vyake vya Natanz na Fordo, na kusafirisha tani chache za madini ya urani kwenda Urusi.

Hakuna shughuli yeyote ya urutubishaji itakayoruhusiwa kwenye vinu vya Fordo mpaka mwaka 2031, na eneo hilo litabadilishwa kuwa kituo cha nyukilia, fizikia na teknolojia.Kutazalishwa kemikali kwa ajili ya kutengeneza dawa kwa ajili ya kilimo,viwanda na sayansi.

Eneo la Arak Iran

Chanzo cha picha, AFP

Iran imekuwa ikitengeneza kinu chake cha nuklia katika mji wa Arak.

Mataifa yenye nguvu duniani awali walitaka Arak isiendelee na shughuli hiyo,kwa sababu ya ongezeko la hatari.Chini ya mkataba wa nyukilia waliokubaliana mwaka 2013, Iran ilikubali kutoendelea na uzalishaji.

Iran iliahidi kubadili mfumo wa vinu vyake ili visiweze kutengeneza silaha zozote mpaka mwaka 2031.

Ofisa wa tume ya kimataifa ya nguvu za Atomiki akiwa kwenye vivu vya Natanz nchini Iran mwaka 2014

Chanzo cha picha, AFP

Wakati wa makubaliano, rais wa Marekani wa wakati huo, Barack Obama alieleza matumaini yake kuwa Iran itazuiwa kutengeneza mradi wa nyukilia kwa siri.Iran ilisema imeridhia kukaguliwa na kutazamwa kwa karibu namna wanavyotekeleza makubaliano hayo.

Waangalizi wa Shirika la nguvu za Atomiki duniani, wameendelea kuifuatilia Iran na maeneo wanayofanyia kazi za urutubishaji na kujiridhidha kuwa hakuna madini yanayopelekwa kwenye sehemu nyingine kwa siri kutengeneza bomu.

Mpaka mwaka 2031, Iran itakuwa na siku 24 za kukubaliana na maombi ya IAEA kufanya uchunguzi wao, ikiwa itakataa tume yenye wanachama wanane -ikiwemo Iran- itatoa uamuzi kuhusu suala hilo.Na itaamua kuhusu hatua za kuchukua, ikiwemo kuiwekea vikwazo tena.

Kabla ya mwezi Julai mwaka 2015, Iran ilikuwa na kiasi kikubwa cha madini ya urani, yanayotosha kutengeneza tani nane mpaka 10 za mabomu, kwa mujibu wa serikali ya Obama.

Wataalamu wa nchini Marekani walikisia kuwa ikiwa Iran itaharakisha kutengeneza bomu, itachukua miezi miwili mpaka mitatu kuwa na uwezo wa kutengeneza silaha za nyukilia.

Iran pia iliamua kutokujihusisha kwenye shughuli kama za utafiti ambao unaweza kuchangia kwenye utengenezaji wa bomu la nyukilia.

Mwezi Desemba mwaka 2015, bodi ya magavana wa IAEA walipiga kura kumaliza shughuli za uchunguzi wa miaka 10 kuhusu mradi wa nyukilia wa Iran.

Kuondoa vikwazo

Meli ya kubeba Mafuta ikitoka kwenye Bandari ya Abbas, kusini mwa Iran mwaka 2012

Chanzo cha picha, AFP

Vikwazo awali viliwekwa na Umoja wa Mataifa, Marekani na Umoja wa Ulaya kujaribu kuishinikiza Iran kuachana na urutubishaji wa madini ya urani hali iliyodhoofisha uchumi wa nchi hiyo.

Vikwazo vilifanya sarafu ya Iran kushuka thamani, kupanda kwa gharama za bidhaa, pia wawekezaji wa kigeni waliondoka nchini humo, pia yalizuka maandamano.

Mwaka 2019 mwezi Mei Iran ilikiuka makubaliano na kutoa muda wa siku 60 kwa wanachama wa mataifa yenye nguvu duniani kuilinda Iran dhidi ya vikwazo vya Marekani, vinginevyo itarejea kwenye uzalishaji mkubwa wa madini ya urani.

IAEA imesema kuwa Iran tayari imeongeza uzalishaji-lakini haijulikani ni kwa kiasi gani.

Ikiwa tume itashindwa kumaliza mgogoro huu, suala hili litawasilishwa kwenye baraza la usalama la umoja wa mataifa.