Kwa nini kijana huyu alijiua miezi miwili baada ya kutahiriwa?

"Ni tukio ambalo lilitokea ghafla na kutushtua sana, tukio hilo lilitokea mwaka 2017 ."Lesley Roberts alikuwa anaisoma barua pepe ya mwisho aliyoandikiwa na mtoto wake Alex Hardy .

Barua pepe hiyo ilimfikia tarehe 25 Novemba 2017, saa 12 baada ya kijana huyo kujiua mwenyewe.

Chini ya saa moja kabla ya barua hiyo kumfika Lesley alifungua mlango wa mbele na kukutana na polisi akiwa amesimama nje na kuanza kumuelezea kuwa mtoto wake amefariki.

Alex alikuwa kijana mwerevu ambaye hakuwahi kuwa na historia ya matatizo ya akili.

Hivyo Lesle hakuelewa kwa nini kijana wake wa miaka 23 aliamua kujiua.

Barua pepe yake ilieleza namna alivyokuwa anapata shida kwenye sehemu yake ya siri mara baada ya kutahiriwa.

Kwa upande wake Alex aliamini kuwa jambo hilo ni sawa na kukeketwa kwa wanaume.

Alikuwa hajawahi kumwambia mtu yeyote katika familia yake au rafiki zake juu ya changamoto iliyokuwa inamkabili wakati wa uhai wake.

Na Kwanza Lesley ambaye ni mama yake alikuwa hata hajui kama mtoto wake alienda kutahiriwa.

Miezi michache baada ya kifo cha mwanae , Lesley alijaribu kutafuta taarifa zaidi juu ya mtu anapotahiriwa.

Alitaka kujua kwa nini Alex aliathirika kwa kiasi hicho mpaka akaamua kuchukua uamuzi wa kujiua kuwa ndio suluhisho pekee.

Alex alikuwa mtoto mkubwa wa Lesley kati ya watoto wake watatu, na yeye alipatikana baada ya jitihada nyingi ambazo mama alipitia ili kupata watoto.

Ndoto za Lesley zilitimia kipindi mwaka 1994 mwezi Julai ambapo alianza kuwa mama wa Alex.

"Yeye alikuwa ni kila kitu ambacho nilikuwa natamani kukipata, hivyo kuondoka kirahisi hivyo akiwa kijana mdogo inasikitisha" Lesleys alisema..

Mama huyo anasema kwamba Alex alikuwa anampenda sana mdogo wake anayemfuata, James ambaye alizaliwa wakati Alex ana umri wa miaka 13.

Ukuta wa nyumba yao ulikuwa umejaa picha za wanafamilia hiyo kila kona.

Alex alikuwa anafanya vizuri katika elimu yake na alibarikiwa kuwa na kipaji katika somo la kiingereza, Baada ya kifo chake,shule aliyosoma waliamua kuanzisha tuzo za kumbukumbu za kuenzi ubunifu wake wa kuandika kingereza.

Alex alikuwa anapenda somo la historia lakini kama mwalimu wake wa kiingereza alimuona kuwa alikuwa ana kipaji cha kuandika .

Mwaka 2015, wakati Alex alipokuwa bado anaumia mwenyewe, aliwahi kumuelezea daktari wake juu ya tatizo ambalo linamsumbua lakini baada ya wiki kadhaa alirudi tena kwa daktari kwa sababu huku akihisi tiba aliyopewa ilikuwa haifanyi kazi.

Tatizo ambalo Alex alilieleza kwenye barua yake ni jambo la kawaida kabisa kwa maisha ya wavulana wakati wanakua, kipindi ambacho ngozi ya juu ya uume inakuwa inaanza kutengana na uume (Phimosis ).

Kijana akikutana na changamoto ya aina hiyo huwa inaweza kumsababishia mtu matatizo kama maumivu wakati wa kukojoa au kufanya mapenzi.

Alex alielekezwa kwa mtaalamu wa kutahiri huko Canada.

Alex anasema kwenye barua yake kuwa "Niilipendekeza kutahiriwa na kuamini kuwa nikitoka kwa mtaalamu tatizo langu litakuwa limekwisha"

Tangu Lesley aanze kusoma taarifa juu ya tatizo lililokuwa linamsumbua mtoto wake sasa hivi anajiona kuwa amefuzu kwa kujua mengi kuhusu kutahiri.

"Nnatamani sana mpaka pumzi yangu ya mwisho pamoja moyo wangu wote kuwa mtoto wangu mpendwa asingetahiriwa" Lesley alimwambia mwandishi wa BBC

Ninamlaumu mwanangu kwa kutofanya utafiti wa tatizo lake au kutahiriwa kwa ujumla, labda kwa sababu wakati huo kompyuta yake ya mpakato ilikuwa imeharibika.

Katika barua pepe aliyoiandika, Alex alieleza tatizo lote ambalo lilikuwa linamsumbua.

Alieleza namna alivyokuwa anapata shida na uume wake wakati alipokuwa anasisimka kutoka kichwa cha uume ambacho hakikuwa na ngozi inayokilinda.

"Pata picha tu pale ambapo kope imeingia katika jicho lako ungejisikiaje?"

"Sijui ni maumivu kiasi gani alikuwa anayapitia ambayo yalikuathiri hata shughuli zake za kawaida."

Ngozi ya juu katika kichwa cha uume ni sehemu nyeti sana.

Lakini vilevile mtu anapotaihriwa wakati mwingine sio lazima mtu kushindwa kufurahia kufanya mapenzi."

Lakini Alex aliona kuwa ngozi yake ya juu ya uume iliyotolewa ilikuwa muhimu.

Lesley alikuwa hafahamu kama mtoto wake alifanya mapenzi baada ya kutahiriwa au la.

Lesley ni miongoni mwa watu wengi ambao walikuwa hawana ufahamu juu kutahiri kabla ya mtoto wake hajafariki.

"Sikuwa nnafahamu chochote zaidi ya kufahamu kuwa huo ni utaratibu wa kawaida wa upasuaji".

Idadi ya watu wanaotairiwa inatofautiana duniani ikiwa inategemea utamaduni wa sehemu ambayo mtu amekulia.

Shirika la afya duniani (WHO) linasema kuwa asilimia 95 ya wanaume wanatairiwa nchini Nigeria huku ni asilimia 85 ya wanaume wanatairiwa nchini Uingereza.

Wanaume wengi ambao wamaetahiriwa nchini Uingereza ni waislamu au wayaudi, kwa sababu kutairi ni sehemu muhimu katika katika imani yao.

Sensa ya mwaka 2011, idadi ya waislamu waliotairiwa ilikuwa asilimia 4.8 ya watu wanaoishi Ungereza na wayaudi walikuwa asilimia 0.5.

Watu ambao wanahoji kuhusu kutahiriwa wakati mwingine wanakuwa wanashutumiwa kuwa wanapinga imani hizo lakini kwake Lesley hakuwa na lengo hilo zaidi ya kujua ukweli kuhusu kifo cha mwanae.

"Kwangu mimi, dini haina uhusiano wowote . Ninaheshimu imani za watu sana kama Alex alivyoheshimu " Lesley alisema.

Nchini Canada, eneo ambalo Alex alitahiriwa, asilimia 32 ya watu walikuwa wametahiriwa.

Alex alihisi kuwa kutahiriwa ni jambo la kawaida ambalo lilikuwa haliwezi kufanya watu kuhoji , huku ukeketaji kwa wanawake unakatazwa katika nchi mbalimbali duniani.

Yeye aliona kuwa kutahiriwa ina bidi kufahamike kama ukeketaji kwa wanaume, na kampeni za kupinga jambo hilo uanze.

"Kama ningekuwa mwanamke kutoka nchi za magharibi, jambo hili ni kinyume na sheria na upasuaji huo ungemfanya daktari kuwa hatiani," Alex aliandika.

"siamini katika kupambania jinsia moja au nyingine lakini ninajiona kuwa shujaa kuwa usawa wa jinsia upatikane kwa wote ."

Kuna watu ambao wanafanya kampeni kuwa si vyema kutairi watoto wadogo kwa sababu mtoto hawezi kutoa idhini yake na kinyume cha haki za binadamu.

Lakini kuishi na uume ambao una ngozi inayotakiwa kutolewa mpaka miaka 21, Alex aliamini kuwa angetahiriwa akiwa mtoto mdogo asingeweza kuhisi hivyo kwa asilimia 75.

Ingawa, wanaume wanaotahiriwa wakiwa na umri mkubwa huwa wanakutana na changamoto zinazotofautiana.

Baadhi uona bora wangoje kufanya ngono kwa muda , kipindi ambacho maumivu yanakuwa yameisha.

Ripoti nyingine zinasema kuwa kutahiri huwa kunapunguza hamu ya kufanya mapenzi

Huku baadhhi ya ripoti zinasema kuwa kutahiri huwa kunabadili namna ambavyo wanaume wanavyofurahia tendo la ngono na hata namna ya kusisimka.

Baadhi ya wanaume wanafurahia maauzi ya kutahiriwa.

Lakini baadhi kama Alex wanajuta au kujilaumu kwa nini walienda kutaihriwa.

"Siwezi kusema kuwa kutahiri ni jambo baya kwa sababu sio baya," Lesley alisema.

Mtaalamu anasema kama kuna umuhimu wa kutahiri basi ni muhimu kujua madhara ambayo yanaweza kujitokeza mtu akifanya upasuaji huo.

Haswa upasuaji huo kama utafanywa wakati kijana akiwa na umri mkubwa, hivyo hatari ambazo zinazoweza kujitokeza ni muhimu kusemwa.

Alex alisema kuwa alikuwa anataka kuweka wazi hatari zote ambazo zinaweza kujitokeza endapo mtu atatahiriwa, na anatamani kuwa asingefanya upasuaji huo.

Si Alex peke yake ndio amekutana na changamoto ya namna hiyo lakini amewawakilisha wengine.