Caster Semenya: Uamuzi wa kesi yake dhidi ya IAAF huenda ukatoa muelekeo kwa wanariadha wengine

Caster Semenya

Chanzo cha picha, Reuters

Huenda ikawa mojawapo ya kesi muhimu katika sekta ya michezo hii leo ambapo uamuzi mkuu unatarajiwa katika mji wa Uswisi Lausanne hii leo Jumatano.

Mahakama ya kutatua mizozo katika michezo (Cas) inatarajiwa kuamua haki ya mwanariadha huyo nyota kushiriki mashindano kama mwanamke.

Caster Semenya ni nani?

Caster Semenya ni mojawapo wa nyota maarufu katika riadha.

Mshindi mara mbili wa dhahabru katika mahsindano ya olimpiki na bingwa wa mara tatu wa dunia katika mbio za mita 800, mwanariadha huyo raia wa Afrika ksuinimwenye miaka 28 ameshinda mbio 29 katika umbali huo.

Hatahivyo tangu kuchipuka kwake, kufuatia ushindi wa dunia mnamo 2009, jinsia yake, na manufaa ya utofauti wa bayolojia mwilini mwake umekuwa ukichunguzwa.

Matokeo ya utafiti wa jinsia uliofanywa miaka 10 iliopita bado hayajatangazwa hadharani, licha ya kwamba vyombo vya habari vimetuhumu kwamba ana sifa za kike na kiume ikiwemo kiwango kikubwa cha homoni za kiume testosterone.

Semenya

Chanzo cha picha, Getty Images

Shirikisho la riadha duniani IAAF lilipendekeza sheria kuzuia viwango vya homoni hiyo ya testosterone inayoruhusiwa kwa wanariadha wanawake katika masindano ya 400m na maili. Semenya alipinga uamuzi huo mahakamani ya kutatua mizozo katika michezo.

Uamuzi huo unatarajiwa leo Mei Mosi mwendo wa saa 11:00 BST.

Nini matatizo ya kijinsia (DSD)?

Wanariadha walio na DSD - hali inayowafanya kukuwa pasipo viwango vya kawaida vya homoni kwa jinisa zao.

Homoni, jeni, na sehemu zao za siri huenda vimechanganyika kwa sifa za kike na kiume.

Neno 'tatizo' linapingwa huku baadhi ya walioathirika wakipendelea kutumia "watu walio na jinsia mbili" na kuitaja kuwa hali ya "kuwana tofuati katika kukuwa kijinsia".

Nini hufanyika baada ya kutambuliwa?

Watu wengi walio na hali hii hushia kuwa na jinsia waliochaguliwa walipo zaliwa. hatahiyvo, wengine wanaohisi kwmaba jinsia waliochaguliwa haimbatani na namana wanavyojihisi , huamua kubadili jinisa zao.

Waathiriwa wa hali hii huenda wakapoteza uwezo wa kuzaa na wanahitaji matibabu ya homoni na ushauri nasaha kuwasaidia kukabiliana na hali walio nayo.

Ni kwanini kesi hii ni muhimu?

Kwa miaka mingi michezo imegawanyika katika kitengo cha wanaume na wanawake, lakini kesi ya Semenya na sayansi iliyojitokeza inaonyesha kwamba kuna tofauti inayoweza kuwepo.

Imependekezwa kwamba iwapo IAAF itashindwakatika kesi hiyo, huenda kukaidhinishwa kitengo cha 'wazi' ambapo kimsingi wanaume na wanawake wataweza kushindana pamoja na kitengo kitakacho ruhusiwa kutokana na vipimo vya homoni kwa mwanariadha na sio jinsia zao.

Je hatma ni ipi kwa Semenya iwapo atapoteza kesi hii?

Mwanasayansi mashuhuri wamichezo amependekeza atapungua kasi kwa kati ya sekundi tano mpaka saba hivi katika mashindano ya mbio za 800m akipunguza kiwango cha homoni ya testosterone kama ilivyopendekezwa.

Anaweza kuishia kukimbia mbio za masafa marefu. Amewai kukimbia mbio za 5,000m mara mbili msimu huu, na akashinda kila wakati.

Sheria inasemaje?

Wanariadha wanawake wanaotaka kushindana wanalazimika kupata dawa kwa kipindi cha miezi sita kabla ya kuingia mashindanoni, na kuhakikisha kuwa kiwango cha homoni hizo kinashuka.

Ikiwa mwanariadha wa kike hatataka kutumia dawa, wanaweza kushindana kwenye:

  • Mashindano yeyote ya kimataifa isipokuwa mbio za mita 400 na maili moja
  • Michuano yeyote ambayo sio ya kimataifa
  • michuano ya wanaume katika ngazi yeyote
  • michuano inayohusisha watu wenye jinsia mbili
  • Wanaotaka kushiriki michuano hawatakiwi kufanyiwa upasuaji .

Taarifa ya IAAF imesema sheria hizo ''hazina lengo la kuwahukumu au kuhoji jinsia ya mwanariadha''.