Tuna El-Gebel: Kaburi lenye miili hamsini iliohifadhiwa lapatikana Minya Misri

Egyptian mummies

Chanzo cha picha, AFP

Miili 50 iliokuwa imehifadhiwa na inayodaiwa kutoka katika enzi za Ptolemaic (miaka ya 305-30BC imepatikana na mwanakiolojia, kulingana na wizara ya vitu vya zamani.

Miili hiyo ambayo 12 kati yao walikuwa watoto ilipatikana katika makaburi manne yenye kina cha urefu wa mita tisa katika eneo la Tuna El-gebel huko Minya kusini mwa mji mkuu wa Cairo.

Baadhi ya miili hiyo ilikuwa imefungwa ndani ya kitambaa huku mingine ikiwa ndani ya majeneza ya mawe na yale ya mbao.

Hawajatambulika ni watu gani , maafisa wanasema lakini huenda walishikilia nyadhfa za juu.

Eeneo la Tuna El-Gebel

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Eneo la Tuna El-Gebe llililopo Minya, kusini mwa mji wa Cairo
Miili iliofungwa ndani ya kitambaa ikiwa na vipande vipande vya michoro.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Vipande vipande vya mawe vilvyochorwa vilikuwa ndani ya miili hiyo.
Miongoni mwao ni fuvu hili la kichwa liliofungwa ndani ya kitambaa

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Miongoni mwao ni fuvu hili la kichwa liliofungwa ndani ya kitambaa
Watoto ni miongoni mwa miii iliopatikana huko Minya

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Watoto ni miongoni mwa miii iliopatikana
Baadhi ya miili hiyo ilipatikana ndani ya majeneza ya mawe

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Baadhi ya miili hiyo ilipatikana ndani ya majeneza ya mawe
Wizara ya vitu vya zamani nchini Misri inasema kuwa miili hiyo huenda inatoka kwa watu wa familia zinazojiweza

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Wizara ya vitu vya zamani nchini Misri inasema kuwa miili hiyo huenda inatoka kwa watu wa familia zinazojiweza