Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tuna El-Gebel: Kaburi lenye miili hamsini iliohifadhiwa lapatikana Minya Misri
Miili 50 iliokuwa imehifadhiwa na inayodaiwa kutoka katika enzi za Ptolemaic (miaka ya 305-30BC imepatikana na mwanakiolojia, kulingana na wizara ya vitu vya zamani.
Miili hiyo ambayo 12 kati yao walikuwa watoto ilipatikana katika makaburi manne yenye kina cha urefu wa mita tisa katika eneo la Tuna El-gebel huko Minya kusini mwa mji mkuu wa Cairo.
Baadhi ya miili hiyo ilikuwa imefungwa ndani ya kitambaa huku mingine ikiwa ndani ya majeneza ya mawe na yale ya mbao.
Hawajatambulika ni watu gani , maafisa wanasema lakini huenda walishikilia nyadhfa za juu.