Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Felix Tshisekedi: Viongozi wa upinzani nchini DRC waungananisha nguvu
Chini ya mwezi mmoja kabla ya uchaguzi mkuu uliosubiriwa kwa muda mrefu nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, kiongozi mkuu wa upinzani nchini Humo Felix Tshisekedi anatarajiwa kurejea katika mji mkuu wa nchi hiyo Kinshasa ili kuzindua kampeni zake akigombea nafasi ya uraisi.
Felix Tshisekedi ni mtoto wa Etienne Tshisekedi,aliyefariki dunia mwaka jana baada ya kutumikia miongo kadhaa kambi ya upinzani nchini humo, ataingia kwenye kinyang'anyiro ya uraisi na mwenziwe Vital Kamerhe kama mgombea mwenza.
Felix Tshisekedi, kiongozi mkuu wa chama kikongwe nchini humo, UDPS pamoja na Vital Kamerhe, wa chama cha UNC,wanatarajiwa kuzindua kampeni zao kwa pamoja, baada ya makubaliano ya kuunganisha nguvu hali ambayo wengi wanaitazama kuwa italeta mgawanyiko mkuu wa kura inaweza kupasuka kura katika uchaguzi mmoja wa pande zote.
Kwa miezi minne,vyama vya upinzani pamoja na hivyo viwili vili kubaliana juu ya mgombea wa kawaida lakini baada ya Mbunge aliyekuwa hajulikani na wengi , Martin Fayulu, kuteuliwa kugombea nafasi ya uraisi kwa niaba ya muungano wa vyama vyote ,ndipo vyama vya UDPS na UNC vikajitoa kwenye muungano huo.
Tshisekedi sasa atawania nafasi ya uraisi kwa makubaliano kwamba Kamerhe atakuwa waziri mkuu wake .Wagombea 19 kwa ujumla wanawania nafasi moja ya uraisi ikiwa ni pamoja na mgombea wa chama tawala, Emmanuel Ramazani Shadary.
Taarifa kutoka ndani ya Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo, na kwa muujibu wa Mwandishi wetu Mbelechi Msochi, vyama vya upinzani vinalalama kutokuwa na pesa za kuendeshea kampeni zao, na hivyo kubana pesa ndogo waliyo nayo mpaka wiki mbili kabla ya uchaguzi ndipo watakapoingia dimbani kunadi sera zao na kisha kuingia kwenye uchaguzi.
Uchaguzi huo umechelewa kwa miaka 2 sasa, unatarajiwa kufanyika tarehe 23 Desemba mwaka huu.