Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uchaguzi nchini DRC waahirishwa hadi 2019
Uchaguzi nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo hautafanyika hadi mwezi Aprili mwaka 2019, kwa mujibu wa tume ya uchaguzi nchini humo.
Katika taarifa tume ilisema kuwa inahitaji takriban siku 504 kuweza kuandaa uchaguzi huo mara usajili wa wapiga kura utakapokamilika
Hii ni kinyume kabisa na makubaliano kati ya Rais Joseph Kabila na upinzani, ulioongozwa na kanisa katoliki kuwa uchaguzi ungefanyika kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Uchaguzi ulipangwa kufanyika Novemba mwaka 2016, lakini ukafutwa na tume ya uchaguzi kutokana changamoto za usafiri na za kifedha.
Hii ina maana kuwa Rais Joseph Kabila amekaa madarakani kinyume na muda unaostahili kisheria.
Watu kadhaa waliuawa wakati wa maandamano.
Kulingana na shirika la habari la Reuters, mapigano katika eneo la Kasai yamechelewesha shughuli ya usajili wa wapiga kura.