Lori laning'inia kwa njia ya ajabu kwenye daraja juu ya barabara Australia

Muda wa kusoma: Dakika 1

Lori hili lilikuwa linasafirisha bidhaa zilizotokana na mayai na nyama nyama ya kuku nchini Asutralia pale haya yalipotokea.

Loli hilo lilibaki kuning'inia kwenye daraja juu ya barabara moja katika jimvo la Victoria.

Ajali hiyo ilisababisha barabara kufungwa na madereva wengi kukwama kwenye foleni katika barabara ya Calder Freeway kaskazini mwa mji wa Melbourne.

Bidhaa zilizokuwa zinasafirishwa na lori hilo zilimwagika na kutapakaa kwenye barabara iliyoko chini.

Vyombo vya habari nchini humo vinasema dereva wa lori hilo amekimbizwa hospitalini, lakini haonekani kuwa na majeraha yanayotishia maisha yake.

Maafisa wanafanya uchunguzi kubaini chanzo cha ajali hiyo, lakini wanasema kuna uwezekano lori hilo liligonga kizuizi pembeni mwa barabara na kupinduka.