Mauaji ya watoto Kenya: 'Niliambiwa nimuuwe mwanangu mlemavu'

Lydia Njoki na mwanawe Samwell
Maelezo ya picha, Lydia Njoki inimojawapo ya wanawake wengi Kenyan aliyeripoti kukabiliwa na shinikizo za kitamaduni
    • Author, Anne Soy
    • Nafasi, BBC News, Kenya

Mtoto wa mwisho wa Lydia Njoki Samwell, anayeugua kifafa na ulemavu , hangekuwa hapa leo iwapo ingekuwa ni uamuzi wa baadi ya jamaa zake.

Nyanyake au bibi yake mwenyewe alifikia kupendekeza namna ambavyo Lydia angeweza kumuua mtoto wake.

"Aliniambia nishindilie sindano katika mishipa ya Samwell - kwamba zingemuua taratibu, na hakuna atakayejua kilichofanyika," alisema.

Mama huyo mwenye umri wa miaka 56 aliye na watoto wanne anaishi katika kaunti ya Narok Kenya.

"Watu walisema nimelaaniwa, ndio sababu nimepata mtoto mlemavu," Bi Njoki ameeleza.

Alikesha usiku mwingi akilia kila anapokwenda kulala: "Nilijichukia na nikamuuliza Mungu, mbona iwe mimi?"

Photograph of Samwell
Maelezo ya picha, Samwell ni mtoto wa mwisho kati ya watoo wanne

Florence Kipchumba alikabiliwa na shinikizo kama hilo - familia yake ilimuambia ni lazima mtoto wake auawe.

"Meshack alikuwa akilia saa alipokuwa mchanga, na wakati familia yangu ilipochoka walinitimuwa nyumbani," alisema.

Rafiki yake alimpokea, lakini hata na yeye mwezi mmoja baadaye akampendekezea amuue. "Aliniambia nimtilie tindi kali kwenye chakula chake, ila afe. lakini nikakata na nikaondoka nyumbani kwake."

Uamuzi wa kukaidi shinikizo la kumuua mtoto umekuwa na athari kubwa ya maisha kwa Bi Kipchumba. Alilazimika kuitoroka jamii yake, na sasa anaishi na mwanawe katika nyumba ya mabanda akitafuta vibarua kujikumu kimaisha.

Meshack alipokuwa mdogo, uti wake wa mgogo ulikuwa dhaifu na hakuweza kukisimamisha kichwa wima. "Nilikuwa nachimba shimo chini ya ardhi, namlaza ndani na nilikuwa natumia mchanga kumzuia ubavuni mwake," alisema.

Florence holding her child in her arms
Maelezo ya picha, Florence Kipchumba akimbeba mwanawe, Meshack

Anasema hajutii hata kidogo uamuzi wake kutomuua mwanawe. Meshack ana miaka mianane sasa na anaweza kukaa na kutembea kwa hatua ndogo , japo kwa matatizo.

Bi Njoki na Bi Kipchumba hawapo peke yao. Utafiti mpya Kenya unaonyesha kuwa 45% ya akina mama waliohojiwa na shirika kuu la msaada wanakabiliwa na shinikizo la kuwaua watoto wao walemavu.

Utaifiti huo umegundua kuwa hali ni mbaya zaidi katika maeneo ya mashinani - ambako huenda idadi ikawa kubwa zaidi kiasi cha kudhihirika kwa akina mama wawili kati ya watatu.

Chimbuko la kitamaduni

Wanawake wengi waliohojiwa na shirika la Disability Rights International wamesema watoto wao walionekana ni kama ''wamelaaniwa, au wamerogwa" na kwamba kuna imani kwamba mama wa watoto hao wanaadhibiwa kwa dhambi walizotenda ikiwemo "uzinzi au kuwadanganya waume zao".

Mauaji ya watoto yanatokana na utamaduni wa jadi na imani. Mkunga mmoja mkongwe wa Narok - kuisni magharibi mwa mji mkuu Nairobi - ameiambia BBC kwamba kwa mujibu wa utamaduni wa jamii yake, watoto walemavu huuawa kutokana na kuwapenda.

"Kilichowashinikiza watu kufanya hivyo, ni kushindwa watawasaidia vipi," anasema Timpiyan enole Koipa, akiwa amekaa katika nyumba yake ya udongo huku akiwa amejitanda shuka yake na amevaa shanga shingoni.

"Asipouawa mtoto ataishia kuteseka," anaongeza.

One of the children in the abandoned children's home
Maelezo ya picha, Wazazi wengi wanawabwaga watoto wao katika hifadhi ya watoto walemavu na hawawarudii tena

Wakati mauaji ya watoto wachanga yanashtusha mno katika ripoti hiyo ya Disability Rights International ,lakini sio jambo pekee lililogunduliwa.

Awali watafiti walikuwa wanachunguza hali katika nyumba za mayatima na majumba ya kuwahudumia watoto, ambako kuna watoto 3, 500 wanaishi nchini.

Mwandishi wa ripoti hiyo Priscila Rodriguez, ameiambiaBBC: "kinachostaajabisha ni kwamba serikali inakabidhi jukumu la watoto hawa kwa nyumba za mayatima... hawaonekani hawakumbukwi. Serikali haihitaji kuwashughulikia tena, wala kuwakimu kimaisha wala kuhakikisha usaidizi wanaohitaji wanaupata."

Walitupeleka kuona nyumba moja ya kuwahudhumia watoto walemavu, Compassionate Hands for the Disabled, iliopo mjini Nairobi. Historia ya makaazi hayo na mmiliki wake yanabaini tatizo lililopo katika jamii kuhusu walemavu.

Anne Njeri alizaliwa na ulemavu na aliamua kuanzisha makazzi ya watoto ya siku walio na matatizo ya ki akili na mwili. hakudhamiria kituo hicho kitumike kama makaazi .

"Lakini katika muda wa wiki moja, tulipokea watoto 11 waliotelekezwa, na kwa mwezi tukapokea 30," anasema.

Anne and Anne (out of focus) speak in the residential home
Maelezo ya picha, Anne sasa ana watoto wengi walemavu anaowahudumia

Aliwatafuta wazazi waliowatelekeza pasi kufanikiwa.

Sasa ana watoto 86. Kwa kumtazama anavyozungumza nao na kucheza nao, ni wazi wanampenda na yeye anawapenda vile viole, lakini anakiri kwamba wanahitajika kuwajibika zaidi.

Watafiti wanakubaliana na hilo, na wanasema wanavyoangaliwa , kufungiwa ndani na kuzuiwa kwa wingi kunahatarisha kuzidisha hali zao kuwa mbaya.

Shutuma kwa serikali

Lakini ni serikali ya Kenya wanayoishutumu zaidi

Serikali nchini Kenya haikujibu ombi letu la kutaka jibu kwa hili, licha ya kwamba inaeleweka kuwa imekiri jitihada zaidi zinahitaji kuchukuliwa.

Japo inashutusha kusikia shinikizo linalowakabili wanawake walio na watoto walemavu waliotakiwa kuwaua, inadhihirisha tu wale watoto ambao wamefanikiwa kukuwa. Hatufahamu wangapi wengine waliosalimu amri kwa shinikizo hilo.

A child in the Kenyan home smiles

Mauaji ya watoto walemavu sio jambo lisilo la kawaida Kenya, lakini ni vigumu kupata takwimu duniani.

Utafiti unatambua visa hivi vina historia ya tangu uzni za nyuma, na limesalia kuwa tatizo katika karne ya 20 na 21.

Mara nyingi visa haviripotiwi au hujumuishwana uhalifu mwingine, na nchi nyingi zinakosa taasisi zinazofuatilia mauaji ya aina hii, kwahiyo ukubwa halisi wa tatizo hili haujulikani wazi duniani.

An empty children's playground

Ripoti hiyo iliyoangazia bara la Afrika inasema "watoto waliozaliwa wasio wa kawaida" mara nyingi huishia kuuawa au kutelekezwa.

Lakini katika baadhi ya nchi, tamaduni na imani zimebadilika kutokana na ushawishi wa ukoloni. Jamii nyingine zimeidhinisha tamaduni mbadala kama kulipa faini kwa njia ya ngoma za kitamaduni na sherehe na tambiko badala ya kumuua mtoto, hatua zinazosaidia kuondosha shaka.

Sheria mpya na hatua za mashirika kuzilinda haki za watoto zimechangia pia kupungua kwa visa vya mauaji wa watoto.